Bujibuji
Ukiangalia Mwanzo 1 : 27 (
Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. )
Biblia inapo sema Mungu akaumba Mtu kwa mfano wake , hapa ina maanisha ni Roho ifananayo na Mungu. Na badae ndio akafaya mtu yaani kufanya katika mwili angalia Mwanzo 2 : 7 (
Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. ). Unaona Roho na Mwili ni vitu tofauti, inapotokea Roho inauacha Mwili, ndipo utaanza kuona ishara kama za kutapatapa kuna kua na Mvutano kati ya Roho ( Maana Roho huya shuhudia inayo endana kukutana nayo, hasa kama Mtu hakua anampendeza Mungu maana yake Roho inakua inashuhudia ile adhabu so inakua inang'ang'ania mwili ili isiende kukutana na ile adhabu, huku mwili kwakua ni mwovu hugoma kuruhusu roho kuendelea kuwamo ndani yake, ndipo hapo lengo la shetani hukamilika kuziingiza roho katika adhabu ambayo nae shetani inamuhusu )