Mama ni moyo ana mapenzi ya dhati yaliyovuka mipaka kwa mwanae, leo hii hata mama yako ukimwambia unataka kuwa msanii atakupa sapoti, mapenzi ya dhati kuna muda huwa yanapofusha kushindwa kuona uhalisia, hapo unakuta mtu hana kipaji wala bidii, hana connections, n.k
Baba ni kichwa, mlinzi na mtafutaji, leo hji ukimwambia unataka kuwa msanii atatafakari na kuona mbali maana ukiwatoa kina Diamond, Kiba, Harmonize na wasanii wengine wachache waliofanikiwa, kuna lundo kubwa sana la wasanii miaka nenda rudi wamesota (kwa ambao tumekaa na wasanii tunajua msoto wake), atakupa makavu na hatakusapoti, atakwambia ni bora akutafutie jembe ukalime uwe na uhakika hata wa kula na kuja kilisha familia yako.
Hapo ukitumia hisia utaona mama anakupenda ila ukitumia akili unaona baba anakujali.
ila kadri umri unavyoenda mtoto wa kiume akiacha kuwa tegemezi na kuanza kujitegemea, kuhama, kujitaftia ridhiki, kuwa na familia, n.k basi hapo ukaribu kwa baba unaongezeka maana wanaanza kufanana, mtoto na baba wote wanajitaftia ridhiki, mtoto na baba wote wameoa, mtoto na baba wote walihama kwao kujitegemea, n.k.
yote kwa yote wote wana umuhimu, ukipatwa na tatizo mama atakuwa karibu na wewe sana huku mzee akihangaika huko nje kukunasua kwenye tatizo kadri ya uwezo wake wote, hapo ndipo wengi wanakosea wanadhani mama ndie mwenye umuhimu zaidi lakini wanasahau baba yupo nje anapambana ili kuwanasua kwenye matatizo ya ujinga kwa kuwapa mahitaji ya elimu, kuwaondolea njaa kwa kuwalisha, kuwasitiri kwa kuwavisha, kuhakikisha hamlali nje kwa kulipia kodi ya nyumba au kujenga, kuwatoa uvivu kwa kuwapa kazi za kufanya nyumbani, kuwanusuru katika maamuzi mabaya yanayoweza kuwapeleka jela kwa kuwatia adabu tangu mkiwa wadogo, n.k. mchango wa baba ukitaka kuujua kama wewe ni mtoto wa kiume anza kujitegemea na kisha uwe na familia yako, ila kama bado unaishi kwenu bado hujawa mwanaume wa kuondoka kwenye kiota ukajitegemee hapo itakua kazi kuona mapenzi ya baba.