humility21
JF-Expert Member
- Jan 8, 2021
- 448
- 622
Inasemekana pia kina mama wanawapenda zaidi watoto wao wa kiume kuliko wa kike ingawa nadhani kwenye kuzaa ni kama vile wanapenda wajifungue watoto wa kike
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu haya mambo sio kwwmba ni nature ilivyo hapanaaa hapanaaa,bali ni ATHARI ZA MALEZI YA TOKEA UTOTONI.Inatokea kwa jamii nyingi kuwa mtoto wa kiume kawaida au mara nyingi kwenye familia huwa na upendo mkubwa sana kwa mama yake kuliko kwa baba yake.
Yuko tayari kuomba ushauri au kumshirikisha mambo yake ya ndani sana mama yake kuliko kumshirikisha baba.
Kwa maisha yetu haya ya Africa baba ndo mtafuta riziki! Hii inatuweka muda mwingi mbali na familia zetu , ni katika kiipndi hiki ambapo baba tupo mbali na familia , mama naye hupata fursa ya kujenga jeshi lake hapo nyumbani, na lazima afanikiwe maana muda wote anakuwa na watoto wake,Inatokea kwa jamii nyingi kuwa mtoto wa kiume kawaida au mara nyingi kwenye familia huwa na upendo mkubwa sana kwa mama yake kuliko kwa baba yake.
Yuko tayari kuomba ushauri au kumshirikisha mambo yake ya ndani sana mama yake kuliko kumshirikisha baba.
Asante, haya ndio maelezo yaliyoshiba na ukweli mtupuMama ni moyo ana mapenzi ya dhati yaliyovuka mipaka kwa mwanae, leo hii hata mama yako ukimwambia unataka kuwa msanii atakupa sapoti, mapenzi ya dhati kuna muda huwa yanapofusha kushindwa kuona uhalisia, hapo unakuta mtu hana kipaji wala bidii, hana connections, n.k
Baba ni kichwa, mlinzi na mtafutaji, leo hji ukimwambia unataka kuwa msanii atatafakari na kuona mbali maana ukiwatoa kina Diamond, Kiba, Harmonize na wasanii wengine wachache waliofanikiwa, kuna lundo kubwa sana la wasanii miaka nenda rudi wamesota (kwa ambao tumekaa na wasanii tunajua msoto wake), atakupa makavu na hatakusapoti, atakwambia ni bora akutafutie jembe ukalime uwe na uhakika hata wa kula na kuja kilisha familia yako.
Hapo ukitumia hisia utaona mama anakupenda ila ukitumia akili unaona baba anakujali.
ila kadri umri unavyoenda mtoto wa kiume akiacha kuwa tegemezi na kuanza kujitegemea, kuhama, kujitaftia ridhiki, kuwa na familia, n.k basi hapo ukaribu kwa baba unaongezeka maana wanaanza kufanana, mtoto na baba wote wanajitaftia ridhiki, mtoto na baba wote wameoa, mtoto na baba wote walihama kwao kujitegemea, n.k.
yote kwa yote wote wana umuhimu, ukipatwa na tatizo mama atakuwa karibu na wewe sana huku mzee akihangaika huko nje kukunasua kwenye tatizo kadri ya uwezo wake wote, hapo ndipo wengi wanakosea wanadhani mama ndie mwenye umuhimu zaidi lakini wanasahau baba yupo nje anapambana ili kuwanasua kwenye matatizo ya ujinga kwa kuwapa mahitaji ya elimu, kuwaondolea njaa kwa kuwalisha, kuwasitiri kwa kuwavisha, kuhakikisha hamlali nje kwa kulipia kodi ya nyumba au kujenga, kuwatoa uvivu kwa kuwapa kazi za kufanya nyumbani, kuwanusuru katika maamuzi mabaya yanayoweza kuwapeleka jela kwa kuwatia adabu tangu mkiwa wadogo, n.k. mchango wa baba ukitaka kuujua kama wewe ni mtoto wa kiume anza kujitegemea na kisha uwe na familia yako, ila kama bado unaishi kwenu bado hujawa mwanaume wa kuondoka kwenye kiota ukajitegemee hapo itakua kazi kuona mapenzi ya baba.
Mtoto akifanya ujinga nyumbani, mama anamuambia mtoto, "akina baba yako atakuchapa" [emoji23][emoji23]Ni kweli mama zetu wanatupenda sn.
Na ndy wanaotuharibia watoto.
Mfano ,,
Baba anaweza kuchimba biti mtoto asitoke usiku kwenda club
Huku mama ndy anayewafungulia milango wakirudi.
Sasa mama kwann asipendwe?na watoto?
Big up mkuu, big up tena na tenaMama ni moyo ana mapenzi ya dhati yaliyovuka mipaka kwa mwanae, leo hii hata mama yako ukimwambia unataka kuwa msanii atakupa sapoti, mapenzi ya dhati kuna muda huwa yanapofusha kushindwa kuona uhalisia, hapo unakuta mtu hana kipaji wala bidii, hana connections, n.k