Kwanini Bongo movie imedorora??

Tatizo hawa watu ccm ndiyo imewapotezaaa mbaayaa kwa mtindo wanaoendesha movi zao na siasa utaachaje kuchukiwa mpaka sasa inajulikana wananchi wa nchii hii wamepambazuka hivyo kutuona sisi mazuzu mshahara wake ndiyo huo pumbafu zao bongo movi chaliiiii
 
NILIACHA KUTIZAMA BONGO MOVE PALE WALIPONUNULIWA NA CCM. NAKUMBUKA ILIKUWA MBEYA KWENYE MAAZIMISHO YA CCM. WALISOMBWA TOKA DAR NA KUVISHWA MAGWANDA YALE YANAYOFANANA NA MCHICHA. HAPO NDIPO WALIPOIZIKA BONGO MOVE.
 
yani mimi mbali na jb kidogo wengine hata huwa sielewi wanaigiza nini.
 
Tatizo kubwa liko kwa producers na directors hao ndio wenye vifaa fedha story usambazaji n.k lkn sio waigizaji kanumba alitengenezwa na 1st quality game na baada ya kutoka wahindi walimbeba japo kipaji alikuwa nacho ambacho hata waigizaji wengine wanacho.
 
Kilichoua bongo movie ni uingiaji Wa series za kikorea ambazo ni very cheep na advanced one.
 
Havana ubunifu kila movie Marylin ni yaleyale unakuta movie zote unazoangalia kwa Mwaka zinafanana
 
Si kwamba bongo movie imekufa ila iko pale² kwa taarifa yenu tatizo tu enzi hizo mlikuwa mnavutwa kwa nguvu za mungu na kuona bongo movie ni kali ila walivyobaki wasio na nguvu za mungu ndio mnaona hakuna kumbuka hata Michael Jackson ngoma zake zilihit sana baada has a.............
 
Bongo movies hazijawahi kuwa kivutio tangu awali...ilikuwa ni mass hysteria tu.Shule ni muhimu kwa kila jambo.

UDSM walaumiwe kwa kuwa na kitengo cha sanaa kinachozalisha watu wasio na ubunifu.
 
nasikia mkuu wa mkoa wa dar ameahidi kurudisha soko lao kwa kufungia uuzwaji wa movie za nje!!!
zimebaki siku ngapi sijui, wenyewe walikuwa wanahesabu huko insta!
Hajazuia bali sheria za copyright zifuatwe ili kuwepo na fair ground katika soko. Movie za nje hazilipiwa kodi wala tozo kama zile za bongo
 
wananichekeshaga wakisema MUIGIZAJI MAARUFU NA MKUBWA WA BONGO MOVIE TZ WEMA SEPETU AME ......... sasa najiuliza mtu tangu kanumba afe siju hajawahi igiza picha yoyote how comes ndo muigizaji mkubwa na maarufu sasa hao waigizaji wengine je? mtu fani uigizaji mara wanajiingiza bongo fleva tamaa na short cut tuuu,watu mwaka mzima wako kwemye kampeni za siasa afu wanataka waigize ...hahahaaa sintaangalia bongo movie ng'ooo hata hawa bongo soccer nao wajiangalie sana
 
Ndio sio wote ila wale role models katika hiyo tasnia wengi wamejikita kwenye siasa wamebaki undergrounds tu ambao wengine wamejikita kwenye Tv series
Wameanza kujikita ln na kudorora kumeanza lini? Hata hivyo hiyo sio sab ya msingi kwani diamond amepata mafanikio makubwa sana baada kuifanyia kampeni ccm
 
Movie za Tanzania naona zinakosa yafuatayo

1. Uhalisia wa kimazingira.
Hiki ni kivutio kikubwa kama kweli tunataka kupanua soko letu lifikie duniani kote.
Afrika tunafahamika kwa utajiri wa maliasili (Mbuga na wanyamapori) hivi havionekani kwenye movie zetu.
Waafrika tuna ujenzi wetu wa asili (Nyumba za tembe etc) pia hivi havionekani tunaonesha maghorofa tu
Magari tunayotumia (Tunayoita ni ya kifahari) ni models za 2012 tukijitahidi sana, huko duniani wanaonesha za 2017 na zingine wanatabiri futurr
Mavazi waafrika tuna yetu ila daily tunajaribu kuonesha ya kwao ambayo ni provocative lkini sisi tunavaa kujishtukia, kama tumeamua tuende all the way kama wao au tubaki na yetu ya asili ambayo ni mazuri zaidi na kivutio duniani

2. Uhalisia wa kiugizaji
Tunajaribu kuigiza maigizo, msanii anaigiza kuwa anaigiza hawavai uhalisia

3. Maisha binafsi ya wasanii nje ya kamera ni hovyo hovyo tu. Postings zao za Social Media ni upupu ukiangalia maandishi katika Captions zao. Wako vizuri kwenye Ubuyu na kusutana. Wanajitahidi kwenye matusi zaidi

4. Masoko

5. Vifaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…