Kwanini Bosi wa TAKUKURU anavaa sare za Jeshi? Nini taswira ya Utawala wa Kiraia?

Hata kama hujastaafu, na umepewa kazi ya umma, hufai kuvaa hayo ma combat ukiwa kazini. Kama uko kambini na unafanya kazi ya kijeshi, hapo sawa lakini public office, haileti shangwe.
Mfano, tuna mmoja ameandikwa huku KE anasimamia development ya CBD(Nairobi) na kusema kweli, yule jomba na ukubwa wake jeshini, sijawahi muona na combat tangu apewe kazi ile, na ukumbuke bado ni active member of defense forces, hujastaafu na hajafika kustaafu. Akimaliza kazi aliyopewa na rais, anarudi kambini kama kawaida.
✌️
 
Hili halina muda... Kuna mabadiliko mengi makubwa yanakuja... Jeshi litatengwa na shughuli na siasa na utawala libaki na dhima yake ya ulinzi na usalama

Hakuna tatizo lolote kwa active servicemen and women kufanya kazi zisizokuwa za kijeshi wakati wa amani. Huu sio utamaduni mpya. Hili limefanyika wakati wa tawala zote zilizopita. Isitoshe ni fursa muhimu kwa wanajeshi wetu kupata uzoefu mwingine tofauti na wa kazi ya ulinzi. Mwisho wa siku, na wao ni raia wa Tanzania wenye haki ya kushiriki kuijenga nchi yao kwa namna yoyote ambayo haikinzani na dhamana yao ya msingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…