Kwanini bunge La Kenya wanaongea English?

Kijakazi

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
7,093
Reaction score
10,469
Nilikuwa napenda kujua ni kwanini Bunge la Jamhuri ya nchi ya Kenya wanatumia Kiingereza kwenye dibeti zao?
 
Kaka, English has been our official language since independence, kiswahili was recently declared an official language when the constitution was promulgated but it remained our National language since independence. kumaanisha, unaweza zungumza kiswahili ama kingereza bungeni, labda unaowaskiza sasa wana jieleza vizuri wakiongea kiingereza kuliko kiswahili.
 
Bungeni kiswahili hakitaeleweka ama kutoa matamshi ya kiswahili itakuwa vigumu...wengi bungeni wanaelewana vyema kwa kiingereza.
pili Kenya ukiongea kiswahili bungeni watu watakuona kama hukufika shuleni
 
Sasa kama ni hivyo ni kwa nini kwenye kampeni za kuomba kura kutoka kwa Wananchi huwa wanaongea kwa Kiswahili na SIYO kwa Kiingereza?
 
Bungeni kiswahili hakitaeleweka ama kutoa matamshi ya kiswahili itakuwa vigumu...wengi bungeni wanaelewana vyema kwa kiingereza.
pili Kenya ukiongea kiswahili bungeni watu watakuona kama hukufika shuleni

Labda nikuulize hivi kwani Bunge la Kenya linamuwakilisha nani? Na hizo dibeti huwa ni nani mlengwa?
 
Unaelewa umuhimu wa debate wewe, wabunge hawafanyi debate wakiwalenga wananchi, ila hujadili wao kwa wao kwa ajili ya wananchi na nchi. Hivyo umuhimu wa lugha humo ndani huwa ni kuelewana wakati wanapojadili. Inaonekana wabunge wa Tanzania huwa yao ni kuongea bungeni ili wawapendeze wananchi wanaowatazama.

Zaidi ni kwamba nchi yetu tuko huru kutumia lugha ya Kingereza na Kiswahili, na hata zetu za asili ambazo huwa tamu sana, ila Kiswahili kiofisi hakitumiki sana maana kina mapungufu mengi, hakijakomaa vizuri.
 
Sasa kama ni hivyo ina maana Mwananchi wa Kenya hana haki ya kujua Mbunge wake kaongea nini Bungeni?
 
Mwananchi ana haki ya kufuatilia ila sio jukumu la mbunge kuhakikisha kila mwananchi ameelewa kila kitu kinaoongewa humo. Jukumu la kila mbunge ni kuhakikisha anaeleweka na wale anaojadili nao.
 
Ohh kumbe ni hivyo! basi nilikuwa sijui kumbe huko Kenya ni tofauti na kwetu, hapa kwetu Mwananchi ndiyo mlengwa, na Mbunge anamwakilisha Mwananchi wake aliyemchagua hivyo ni muhimu kwa Mwananchi kuelewa Mbunge wake anasema nini!

Sababu za kihistoria zaidi..kiswahili kenya hakikupewa kipaumbele tangu enzi za ukoloni ukiachia sehemu za pwani..shuleni linafundishwa kama somo moja tu..majumbani watu wengi ni lugha mama ..ama wakichanganya kiswahili na kiingereza. ..
 
Hivi kabla havijaletwa vyombo vya habari vyenye uwezo wa kupeperusha majadiliano moja kwa moja, wabunge wenu walikua wanatumia mbinu gani kuwalenga hao wananchi. Mbona unakua mgumu kuelewa issue ndogo hivi. Wabunge huchaguliwa kuwawakilisha wananchi ili wakajadili wao kwa wao na kutunga sheria kwa ajili ya nchi, pamoja na hoja zingine.

Ni majuzi tu tumepata vyombo vinavyotuwezesha kufuatilia. Mwananchi hata akifuatilia, hana uwezo wa kuhusika na nabaki tu kuangalia yanayoendelea.
 
Poa poa usikonde, nilikuwa tu napenda kujua, na sasa nimeelewa, kwa maana nilikuwa najiuliza ni kwanini Wabunge na wanasiasa wengi wa Kenya kwenye kampeni huwa wanahutubia kwa Kiswahili halafu wakishachaguliwa na wakiwa Bungeni huongea kwa Kiingereza, au hata Raisi wa Kenya akiwa kwenye kampeni kuomba kura huomba kwa Kiswahili lkn akishachaguliwa na kuvaa suti na sasa anahutubia Nchi huongea Kiingereza sasa hapo ndio palikuwa pananichanganya, kwa maana kwa akili ya kawaida alipaswa lugha anayoombea kura ndiyo hiyo pia aitumie wakati akishachaguliwa anapohutubia nchi!
 
Mbunge akiwa anahutbuia wabunge wenzake bungeni anatumia lugha wanayoelewana, akiwa huko nje haswa vijijini anawahutubia wananchi kwa lugha wanayoelewa kwenye hafla yoyote ile. Kama nilivyosema, umuhimu wa lugha ni kuelewana na inategemea unaongea na nani na anaelewa vipi ile lugha unayotumia kumuelezea.
 
Sababu za kihistoria zaidi..kiswahili kenya hakikupewa kipaumbele tangu enzi za ukoloni ukiachia sehemu za pwani..shuleni linafundishwa kama somo moja tu..majumbani watu wengi ni lugha mama ..ama wakichanganya kiswahili na kiingereza. ..

Lakini kwenye kampeni hakuna eneo lolote ndani ya kenya ambapo mgombea anatumia lugha tofauti na kiswahili kuombea kura.
 
Naona bado hujui mambo ya Kenya vizuri. Wabunge huzunguka wakitafuta kura kwa lugha inayofahamika na wale wanao ongea nao. Kuna wakati wanaongea hadi lugha zetu za asili kule vijijini. Wakiwa mjini ndio huongea lugha hizi za kubuniwa kama Kiswahili na Kingereza.
 
Lakini kwenye kampeni hakuna eneo lolote ndani ya kenya ambapo mgombea anatumia lugha tofauti na kiswahili kuombea kura.

Wakiwa mikoani, wengi wao hutumia lugha zao za mama...mjaluo anaongea cha kwao, mkikuyu naye vile vile, mbaluya
nae pia ....ilmradi ujumbe ufike bila wasiwasi.
 
Back
Top Bottom