Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Asante Sana. Naendelea kupata elimu zaidi.

Barikiwa
 
Nikisoma maandiko hayo huwa napata mawazo sana. Yaani laana hadi kizazi cha 3 ama cha 4.
 
Okay upo sahihi kwa mtazamo wako ila inakuwa haijibu swali letu kwamba kwanini laana iende kwa canaan kma kwenye hilo kosa hausiki popote.... Tukijua sababu basi nadharia hizi zinakuwa hazina maana

Ok, mimi nilikiwa namuuliza namuuliza Mshana Jr na Jamaa mwingine aliyesema, Laana inaenda mpaka kizazi cha nne, ndio nikauliza hiyo laana ya kizazi cha nne anaitoa nani?, Mungu au mtu, Kama ni Mungu iweje Noah atoe laana kwa mjukuu wake?,

Back kwenye Swali lako au hoja yako, ni hoja fikirishi sana na tunasemaga mara nyingi Biblia iko coded, yaani ni fumbo so vitu vingi vinahitaji tafakari na pia kujua mapokeo ambayo mara nyingi yanasimamia kwenye tamaduni na historia ya eneo husika,

Swali la msingi nadhani linasimama pamoja na hoja yako ni kuwa, wakati Ham anamwona Baba yake akiwa uchi hakuwa mtoto mdogo, alikuwa ni mtu mwenye Mke na watoto wanne, so ni mtu mkomavu ambaye kwake isingekuwa rahisi kucheka uchi wa babake na kuwaadithia nduguze kama mambo ya kitoto vile, kitendo kilichofanywa na Kakaze cha kumfunika uchi babaye hata yeye angeweza kukifanya, iweje amwone uchi na atoke nje akimwacha uchi?

So lazima uncode filosofia iliyotumika hapo, Na kufanya hivyo kunaendana na kusoma Biblia pamoja na mapokeo mbalimbali ya kukuwezesha kujua tamadani za hayo maeneo wakati wa Noah

Ni vizuri umeiweka hapa kuna watu wanweza kiwa na uelewa wa habari ya laana ya kaanani, lakini mpaka sasa naona swali liko palepale na zinatoka haya nyingi zisizo na jibu la swali husika
 
Mtoto wa Gamba.

Kwanza sidhani asomae kama kitabu cha hadithi anaweza fikirisha akili akapata maswali ambayo hana majibu kupelekea kushirikisha wenziwe ili aeleweshwe..

Ukiona msomaji kaleta hoja kama hizi ujue hakusoma kama kitabu cha hadithi..

...
Kutokana na maelezo/hoja hizi ulizoweka hapa, Pia kuna maswali/hoja zinahitaji ufumbuzi zaidi..

Kwa Mfano:
Tumeona Ibrahim/Abraham akibarikiwa na kizazi chake.

Pia Isaka akambariki Yakobo na kizazi chake.

Swali/Hoja.
Inawezekana mtu atokae na kizazi cha Ibrahim/Abraham aje kulaaniwa na Mwanadamu au Mungu huko mbele?..
Sababu Mungu alishabariki hiki kizazi na kusema kwamba "Alaaniwe atakae Kulaani"..

....

Pia nikufahamishe kuwa watu hawana shaka na laana katika mkasa wa huu wa Nuhu..
Tatizo linakuja kwanini isianze kwa Ham na kuendelea mbele kwa uzao wake wote?..
Kwanini Canaan tu?..

Hapo ndipo panapohitaji Hekima..
Aliesoma na kufahamu, Atujuze nasi tupate kufahamu..
 
nakufuatulia mkuu"" umechambua vyema "" kwa upande wangu " mimi hayo mambo ya laana mpaka kizazi cha 4 siyaamini "" na subiri wenye imani ya hivyo vitu " wake watudadavulie lakini iwe ni kwa essay za kueleweka ""
 
Uko utaratibu wa Kiutendaji wa Kimungu. Mungu hatendi kiholela holela tu.

Mungu alimbariki Nuhu na watoto wake watatu. Na Nuhu akamlani Caanan na kusema kuwa atakua mtumwa kwa nduguze.

Kaanani alikuwa ndio lango la baraka katika uzao wa Ham. Utasema kwa nini? Jiulize kwa nini? hakuna nchi ya Ham ila iko nchi ya Kaanani? Wakati Ham ndio Baba wa uzao wake.

Ndio maana hata kwa Abraham Mtoto aliyebeba lile agano/baraka za kiroho alikuwa ni Isihaka. Tena kwa sababu hiyo Bwana Yesu/Mungu akaja ulimwenguni kupitia uzao wa Daudi ambaye ukirudi nyuma utamkuta Isack. Hakuna ukombozi mwingine kwa mwanadamu kutokana na dhambi bila kupitia kwa Bwana Yesu. Ndio ukweli mchungu huo. Huko kwengine ni kujidanganya tu, utaishia jehanamu na mabilioni tayari wamesha potelea jehanamu.
 
Mkuu nmekuelewa ila hoja yako inazidisha maswali kuliko majibu..... Sawa alilaaniwa Canaan je swali inakuja kwanini canaan na sio cush mizraim na phut??

Okay umesema mwenye taifa ni canaan ambayo si kweli..... Misri imetoka kwa mizraim na phut ilianzisha nchi ya libya na pia cush alianzisha taifa la ethiopia sasa mbona wote walikuwa na mataifa why canaan ana kipi hasa cha ajabu kuliko hao kaka zake

Hatuna shida na laana wala Yesu ila tunajiuliza Why canaan?? Tusaidie hapo kwanni unasema canaan ni mlango wa baraka
 
Tafuta semina za Mwl Mwakasege kuhusu "malango na baraka" katika ulimwengu wa Kiroho. Nimezunguza kwa Misingi ya Ukristo na Biblia tu.

Halafu unasema, "Hakuna nchi ya Caanan?" Are you kidding?

Hujui kinyume cha baraka ni laana? Baraka za watoto wa Ham zilikuwa zipitishiwe kwa Caanan. Soma Kuhusu Yusuph na Nduguze 11 Watoto wa Yakobo/Israel utaelewa maanaya mlango wa baraka. Wao 11 Acha hao 3 wa Ham, 11 na Baba yao Yakobo hawakuwa na jinsi walimfata Yusuph Misri ili waponywe na Njaa.

 
Tafuta semina za Mwl Mwakasege kuhusu "malango na baraka" katika ulimwengu wa Kiroho. Nimezunguza kwa Misingi ya Ukristo na Biblia tu.

Halafu unasema, "Hakuna nchi ya Caanan?" Are you kidding?
Nasema nchi ilikuwepo ila hata watoto wengine wote na Ham walikuwa na nchi ambazo kwa nyakati tofauti ziliwahi kutawala dunia hii kuanzia misri mpaka ethiopia so sioni big deal canaan kuwa na nchi

Kuhusu malango ya baraka ni vzuri ungeeleza ulichoelewa kuishia katikati hautusaidii kma unalink au pdf ama unakumbuka tuwekee hapa tujifunze zaidi mkuu

Ubarikiwe
 
Hizo nyingine unazo sema zinaitwa taifa la Mungu? BWANA YESU/MUNGU alipokuja dunuani alizaliwa wapi? BETHLEHEM na YERUSALEMU ziko Misri AU MAKKA. Iko ISRAEL? Hekalu la Nabii Selemani? Liko SAUDIA? Mtume Muhamad SAW kwa nini hakushushiwa Quran Makka AU Madina? Akasema alishushiwa hapo JERUSALEM?

 
Labda nikukisoe hapo mkuu canaan ya sasa sio canaan ya kale kumbuka kibiblia nchi ya ahadi kwa waisraeli ilikuwa inafika hadi River tigris na Euphrates kwahiyo una maana syria na iraq pia ni taifa la Mungu kwa definition hiyo unayotaka kutuaminisha???

Alafu nachotaka tufahamu ni kwamba Canaan walienda wayahudi sababu ya kutimiza laana hii ila kama Nuhu asingemlaani Canaan Mungu angewapeleka kwingine sio CANAAN na ndio maana bado kuna mjadala mkubwa sana hadi leo kuwa huenda Canaan aliwekwa kwenye laana ili kuhalalisha uvamizi huu wa wayahudi canaan!! Hivyo huenda Ethiopia ingekuwa taifa teule kma sio laana ya Ham so bado haijibu hoja kwanni Canaan ana utofauti

Alafu mkuu haya mambo yaliisha Yesu alipokuja wote tupo sawa mbele za Mungu hakuna kitu kama taifa la Mungu or what wayahudi walimkataa Yesu na hivo Mungu alitugeukia sisi wengine sasa hayo ya taifa teule yametoka wapi tena?? Wanaenda kuzimu kama kawaida so tuachage kuaminishana kuwa kuna taifa teule na israel ya sasa sio israel ya kale

Ni mawazo tu
 
Yesu alikuja kwao "wale walio kuwa wake hawakumpokea" (Wayahudi Taifa teule la Mungu), bali waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu wa aminio Jina lake. (Ndio watu wote wa dunia walio mpokea Bwana Yesu wakiwemo wakina Petro-Wayahudi).

Unajua maana ya Taifa Teule la Mungu?

Sio huenda Caanan aliwekwa katika laana ndivyo hivyo ilivyo. Ndio maana kuna taifa teule la Mungu ili kupitia hilo Mungu afanye ukuhani wake hapa duniani. Matendo ya Mungu hayo, ni makuu na ya ajabu.

 
Sijakuelewa hata kidogo hebu soma hii:

Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake. Ezekiel 18:20

Sasa iweje Canaan abebe uovu wa baba yake Ham?

Iweje Watoto wa Akani waangamizwe kisa uovu wa baba yao?

Iweje ardhi ilaaniwe kwa uovu wa Adam?
 
Hapana hapa nitofautiane na wwe tena....Canaan haikuwa taifa teule mkuu ila mpaka pale ilipotumika kutimiza laana ya Nuhu hivyo bila laana ya Nuhu wasingepelekwa Canaan sababu jiulize kwanini Abraham alipotolewa nchi yake aelekezwe Kwenda huko na sio Nigeria au china??? Kipi kinaashiria canaan ni taifa teule kiasi kwamba ilikuwa meant ikaliwe na wayahudi?? Embu tusaidie hapo maana ndipo tunapopishana

Na taifa teule haikuwa Israel mkuu ni kwamba Zilianza kwa shem na zikaenda throughout bloodline yake huyo Yakobo aliiba tu lakini Baraka ya Abraham ilikuwa kwa mataifa yote yaliyotokana kwake ila sio kwa Israel tu hivyo hata semites wengine wengi tu na edomites walipokea baraka hizi sio jews pekee kama mnavyotaka kutuaminisha

Mtazamo tu
 
Aiseee hoja nzito sana hii ngoja wataalam waje tikakami wa lopelope mitale na midimu
 
Swali/Hoja.
Inawezekana mtu atokae na kizazi cha Ibrahim/Abraham aje kulaaniwa na Mwanadamu au Mungu huko mbele?..
Sababu Mungu alishabariki hiki kizazi na kusema kwamba "Alaaniwe atakae Kulaani"..

Hakuna mwanadamu anayeweza kuwalaani wana wa Israeli na laana hiyo ikatokea au ikafanyakazi, hakuna... Lakini, MUNGU peke yake anaweza kuwalaani Waisraeli wale ambao hawatafuata amri zake na maagizo yake na sheria zake. Ukisoma KUMBUKUMBU LA TORATI 28:15-19, utaona jinsi ilivyo.

Pia nikufahamishe kuwa watu hawana shaka na laana katika mkasa wa huu wa Nuhu..
Tatizo linakuja kwanini isianze kwa Ham na kuendelea mbele kwa uzao wake wote?..
Kwanini Canaan tu?..
Hili swali lako nimeshalijibu kwa kirefu sana, tafuta comment [HASHTAG]#103[/HASHTAG] katika uzi huu na ujisomee.

Unajua nini mkuu Babu Kivu kuna kitu watu wengi wanakosea sana bila kujua, kitu hicho ni pale watu wanapotaka "kumwelewa" BWANA MUNGU. Hakuna Mwanadamu wala Malaika mwenye uwezo wa kumwelewa MUNGU. Sisi Wanadamu na Malaika, tunao uwezo wa "kumwamini" na "kumtii" MUNGU, lakini hatuna uwezo, wala akili za "kumwelewa". Hata Biblia haikupi nafasi ya "kumwelewa" MUNGU, isipokuwa inakupa uwezo wa kumwamini na kumtii basi. Tena kuamini na kutii ni hiari, wala BWANA MUNGU hamlazimishi yeyote.

Watu wengi wanaisoma Biblia ili "wamwelewe" MUNGU, wanapogundua Biblia haiwaeleweshi kuhusu MUNGU, wanakata tamaa, wanasema MUNGU ni muonevu, mara ooh, anaupendeleo, mara ooh, Biblia inaji-contradict, n.k. Wanakosa imani, mwishowe wanasema MUNGU hayupo.

Lakini ukweli ni kwamba MUNGU yupo sana, sema tu hajatupa nafasi ya sisi kumwelewa, yaani hajavipa nafasi viumbe vyake vyote kumwelewa. Isipokuwa ametoa nafasi kubwa sana ya viumbe vyake vyote kumwamini na kumtii. Na hilo ndilo jambo muhimu kuliko yote, kuamini na kutii.
 
Ndugu unataka uholela gan tena zaidi ya huu wakutoa laana adi kizazi cha nne
 
Ni
niajabu mkuu haki yake mwenye haki na uovu wake mwenye uovu kila mtu ahukumiwe kwa matendo yake laana mpaka kizazi ni hadaa tupu
 
Ni
niajabu mkuu haki yake mwenye haki na uovu wake mwenye uovu kila mtu ahukumiwe kwa matendo yake laana mpaka kizazi cha nne ni hadaa tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…