Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

.
Mwanzo 9

22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.

Inapingana na hiyo Dhana ya kumzuia asimzini
Hahahaha mkuu Najaribu kuwaza tu huenda alikuwa anawaambia kwa kelele kuwa "shem na japhet huu mzigo wa mama ni mtamu sana" huku akiwa bado yupo naye kitandani ila kina shem wakiwa nje ya hema waliweza kusikia na wakakasirika wakaingia wakamtoa HAM asiendelee kumlala mama yao hivyo kwa kuwa hawakutaka na wenyewe kumlala mama yao bali wakamzuia Ham ina maana WALIFUNIKA UCHI WA BABA YAO

Najaribu kuwaza tu possibility za nadharia hii kuwezekana kwenye context hiyo ya biblia
 
  • Thanks
Reactions: Ok9
Mkuu Jo Venture kwanza kabisa unapaswa kuelewa kuwa Nuhu alikuwa kama Nabii wa MUNGU, hivyo basi Nabii wa MUNGU akitoa laana, laana hiyo imetoka kwa MUNGU, na Nabii wa MUNGU akitoa baraka, baraka hizo zimetoka kwa MUNGU, iko hivyo na hiyo haina ubishi.

Sasa ili niweze kujibu hoja yako vizuri, mimi nitaendelea kukujibu kwa kutumia Biblia sababu naamini kila jibu lipo ndani ya kitabu hichi hata kama majibu yamefichika. Labda naomba nikuulize wewe na wengine wote mnaouliza ni kwanini Caanan alilaaniwa na siyo Ham. Hivi ni kwanini Yakobo aliwabariki Efraimu na Manasse moja kwa moja kwa kuwawekea mikono kichwani na hakufanya hivyo kwa wajukuu wake wengine?? Kwanini alifanya hivyo kwa Efraimu na Manasse peke yao, tena kwa kumbariki mdogo ambaye ni Efraimu kwa baraka kubwa zaidi kuliko mkubwa ambaye ni Manasse?? Kwanini alimchagua mdogo??? (soma MWANZO 48:14-20)

Mimi naamini ipo sababu ya kufanya hivyo. Kumbukeni hata Yakobo alikuwa kama Nabii wa MUNGU, hivyo baraka zake au laana zake ni moja kwa moja zinatoka kwa MUNGU. Sasa turudi kwa Nuhu, kwanini alimlaani Caanani moja kwa moja na kuwaacha watoto wengine wa Hamu ambao hawakulaaniwa moja kwa moja kama ilivyokuwa kwa Caanan? Iko hivi; sisi wazazi huwa kuna mtoto tunampenda kuliko wote katika watoto wetu. Mara zote yule mtoto anayependwa zaidi na baba yake huwa kama amebeba roho ya baba yake. Inawezekana kabisa Caanani alikuwa kipenzi cha Hamu kuliko watoto wote aliokuwa nao ambao ni Kushi, Putu, Misri(Mizraim), na Caanan.

Mfano mzuri ni jinsi ambavyo Yakobo alivyokuwa anampenda sana Yusufu kuliko ndugu zake wote na Yusufu alikuwa ni mdogo, ingawa Benyamini alikuwa ndiyo mdogo zaidi. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa roho ya baba huwa inakuwa juu ya mtoto yule anayempenda zaidi kuliko wote. Sasa inapotokea baraka zinamdondokea baba, hizi baraka zitaenda kwa mtoto yule anayependwa zaidi. Na pia kama itatokea laana ikamdondokea baba, laana hii itakwenda kwa yule mtoto anayependwa zaidi. Ndiyo kisa nikawauliza lile swali kwanini watoto wa Yusufu walipokea baraka moja kwa moja kutoka kwa babu yao Yakobo na wajukuu wengine hawakubarikiwa moja kwa moja??

Hivyo hivyo pia, kwa Nuhu kumlaani Caanani moja kwa moja ni lazima alijua kuwa Caanani ndiye kipenzi cha baba yake ambaye ni Ham. Sasa ili kumkomoa Ham ili aumie zaidi ni kumlaani yule anayempenda zaidi ambaye ndiye hasa anabeba roho yake. Siku zote laana ipo kwa ajili ya kukomoa na kuumiza, huwezi kumkomoa mtu na kumuumiza pale pasipo uma zaidi, huwezi kumkomoa mtu kama hutaharibu kile kitu anachokipenda zaidi, ukiharibu kile asichokipenda utakuwa hujamkomoa wala hatadhurika. Lakini ukiharibu kile anachokipenda kuliko vyote, hapo unakua umemkomoa na kumshikisha adabu ipasavyo. Ifahamike kuwa hawa watu wa kale, kitu laana au baraka walikuwa wanazichukulia very seriously. Ni wazi kabisa hizi laana zilimuumiza sana Ham kuliko hata Caanan aliyelaaniwa moja kwa moja.

Mfano mzuri katika hili ni lile lililowakuta Wamisri siku zile za Musa. Wote mnafahamu namna MUNGU alivyoamuru watoto wote wa kiume ambao walikuwa ni wazaliwa wa kwanza wa kila nyumba katika Misri wafe. Usiku ule akapita Malaika na kuwauwa watoto wote ambao ni wazaliwa wa kwanza wa Wamisri. Sasa hapa mtauliza; hivi wale watoto walikuwa na makosa gani mpaka wafe wao wakati siyo wao waliowatesa na kuwanyanyasa wana wa Israeli??? Kwanini waliuwawa watoto wao wasiokuwa na hatia??..... Jibu mnalijua tayari.

Iko hivi; maamuzi ya MUNGU wakati mwingine huwa hayaeleweki kwetu sisi wanadamu, lakini hiyo haina maana kuwa maamuzi yake siyo sahihi. Kwa watu ambao wanamwamini MUNGU na kuzishika Amri zake wanajua kabisa MUNGU huwa hakosei katika maamuzi yake na matendo yake. Kuna watu ambao hawamwamini MUNGU, wala hawazishiki Amri zake, watu hawa wakisoma Biblia, wanakimbilia kusema MUNGU ana makosa, wengine wanasema MUNGU ni muonevu, wanapoteza imani na kuona kama Biblia ni kitabu tu kama vitabu vingine.

Naamini ndugu yangu zitto junior na wengine wote mtakuwa mmenielewa. Swala la roho ya baba kwenda kwa mtoto wengine litakuwa limewachanganya sana, lakini fahamuni kuwa kila baba kuna mtoto wake anabeba roho yake. This is a mystery, it is paradoxical, but it is real. Mfano hata katika jamii zetu mmewahi kusikia watu wakisema; "huyu mtoto yuko kama baba yake kabisa, kuanzia kuongea mpaka kutembea". Mfano ni Adamu jinsi alivyofanana na Sethi;

"Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi". MWANZO 5:3.

Maana yake ni kwamba roho ya Adamu ilihamia kwa Sethi, licha ya kwamba Adamu alikuwa na watoto wengine wengi tu mbali na Sethi.
Cc Doto Dotto
Umenipa jambo kubwa sana kudos mkuu
 
Mkuu zitto junior kwenye Quran ulishasema hakuna hio mada sasa jiulize hawa wasomi uliowataja na unaopenda sana kuwataja wamepata wapi hayo? Hijawahi kutokea Mtume wa Mungu eti mke wake kutembea na mtoto wake. Please mkuu.
 
Quran haielezi kuhusu tukio hili la laana maana quran haiwezi kuandika kila kitu isingeweza kubebeka yaani wataje kila kitu kwenye Surat Hud??? Ndio maana hili la laana wasomi wanatumia sources zilizo reliable na Huyo Al Tabari ni accredited na jumuiya zote za kiislam huwa wanatambua maandiko yake na yanatumiwa na wanazuoni wa kiislam kujenga hoja kwenye masuala mbalimbali ya kiimani kama ilivyo flavius josephus kwa upande wa wakristo huyo ni mwanazuoni accredited kabisa kwenye kujengea hoja za biblia

Embu msome hapa na uliza masheikh wako kama hawamtambui na usikute wamesoma hiyo Tafsir al tabari na machapisho yake mengine ili kuichambua vzuri Quran tukufu..... Hivyo ni source inayokubalika mkuu kwa waislam usiwe na shaka

Al-Tabari - Wikipedia
 
Wacha kupotosha hakuna kitu kama hicho kaka. Naona unamsafiria sana Mu Iran Al Tabari. Yeye ni jamii ya Shia ambao wanamitazamo yao kutokana na jinsi wanavyoamini. Tuwekee chapter moja ambayo Al tabari ameongea kuhusu hio issue mkuu
 
hakuna kitu kama hicho
Mkuu ni vizuri tukijenga hoja kwa facts kama wewe unasema ni mpotoshaji basi tuwekee hapa pingamizi lako sio KUPINGA bila sababu.... Hutusaidii kabisa huyo tabari nimekuta masheikh wengi tu hata vyuoni wanatumia reference kutoka hadith alizoandika yeye sasa unapomkataa wewe basi acha wanaomtambua wamsome hatuwezi acha comments za wasomi kisa tu muislam mmoja au mkristo mmoja hamtambui

Mfano hapa nimetoa reference kwenye vitabu hata visivyo vya kikristo!! hivyo usiweke mahaba ya kidini humu maadam nimeshasema kwenye Quran hakuna wwe hayo ya Ibn Tabari yanakuumiza nini?

Mkuu tusiingize udini humu tutaharibu uzi kama humtaki basi acha wengine wajifunze
 
Dharra
Naona unataka kubishana tu kitabu kizima kiko hapa soma kuanzia page ya 10 na anaweka na facts kabisa kuhusu simulizi zake

Ni vizuri tupende kusikia hoja kinzani ila kuingia na misimamo ya kidini kwenye mada kama hizi tutakuwa hatujifunzi chochote
 
Mkuu ni vizuri tukijenga hoja kwa facts kama wewe unasema ni mpotoshaji basi tuwekee hapa pingamizi lako sio KUPINGA bila sababu.... Hutusaidii kabisa huyo tabari nimekuta masheikh wengi tu hata vyuoni wanatumia reference kutoka hadith alizoandika yeye sasa unapomkataa wewe basi acha wanaomtambua wamsome hatuwezi acha comments za wasomi kisa tu muislam mmoja au mkristo mmoja hamtambui

Mfano hapa nimetoa reference kwenye vitabu hata visivyo vya kikristo!! hivyo usiweke mahaba ya kidini humu maadam nimeshasema kwenye Quran hakuna wwe hayo ya Ibn Tabari yanakuumiza nini?

Mkuu tusiingize udini humu tutaharibu uzi kama humtaki basi acha wengine wajifunze

Mkuu tupo kwenye mjadala hapa nawe vile vile uwe na ubavu wa kukoselewa. Kwa mfano ulio wazi angalia jinsi ulivyonukuu maandiko hapo juu, unaponukuu usijaribu tu kuweka nukuu za upande mmoja kisha una justify eti hata uislam unaamini hivyo kitu ambacho sio kweli kabisa. Waislam tunamjua huyo tabari na ndio maana katika wasomi wakubwa wa dini hayupo kabisa katika list. Unapoleta mabandiko kama haya uwe muangalifu na ni bora usitaje kabisa dini na hasa Uislam. Sababu Uislam hauendani na idea za mtu na wala matamanio ya mtu. Ukishaweka maandiko kutoka katika vitabu vitakatifu ni wazi kuwa umefungua mjadala wa kidini na uwe tayari kwa consequences zake. Nakunukuu "Ila ukisoma hadeeth mbalimbali na machapisho ya wasomi nguli wa kiislam wa mwanzo kabisa kina Muhammad ibn-jarir al tabari pamoja na ibn khaldun wanaeleza kwamba HAM alilaaniwa sababu akiwa kwenye Safina ya Nuhu alimlala mke wake kitu kilichokatazwa hivyo alilaaniwa kwa kupewa ngozi nyeusi na ndio maana watoto wake wote wakawa weusi!!! So hawa angalau wamesema HAM alilaaniwa ila kwa kosa tofauti.... Hivyo bado hawajatupa jibu la kisa cha Nuhu na Canaan
 
Wapi nimegeneralise si nimesema ni mawazo ya WASOMI WA KIISLAM na sio UISLAM kama DINI ama QURAN!! au Al tabari ni mkristo?? Anyway ulitaka nisemeje mkuu embu nishauri ili nisirudie makosa

Nlishasema toka mwanzo kama wwe humtambui Al tabari wengine wanamtambua hasa washia... kama wwe unaona washia wako wrong kuna maeneo ushia unatambulika kama Iran na miskiti yao wanaquote sana mafundisho yake na wanaitwa waislam sasa ulitaka nisiweke mafundisho yake kisa wasunni hamutambui washia??? Tutafika kweli

Ni hivi Al tabari ni muislam na wanazuoni wakiislam hasa washia wanatambua mafundisho yake sasa whether wwe humtambui huo ni mjadala mwingine ila kwa kuwa machapisho yake yanatambuliwa na jumuiya za waislam basi sio mbaya kuweka mawazo yake hapa kma halikufai liache wengine wajifunze hapa tunaweka source zote hata za wapagani na wachawi as long as tunaunganisha dots kupata jibu moja

So samahani kama nimekukwaza ila huo ndio msimamo wangu
 
Mkuu ganster siyo kila kitu kilichoandikwa kwenye Biblia kimewekwa wazi wazi, lakini ukiisoma vizuri Biblia na kuielewa basi hata vile vilivyofichika utaelewa maana yake. Mfano mzuri ni hili Swali; kwanini Efraimu na Manasse walibarikiwa moja kwa moja na babu yao Yakobo kwa kuwekewa mikono kichwani na wajukuu wengine hawakubarikiwa moja kwa moja???

Nini cha ziada walichokifanya Efraimu na Manasse kuzidi wenzao, maana wakati wanabarikiwa walikuwa ni watoto wadogo tu??

Ukiweza kujua ni kwanini hawa walibarikiwa wakiwa wadogo, pia utafahamu ni kwanini Caanani alilaaniwa akiwa mdogo.
Biblia inahitaji utulivu wa kiroho kuielewa
 
watakwambia mungu ..hapangiwi...yaani trilion 1.5 aibe jiwe halafu hukumu apew jesca like serious "" Mungu huyu Mungu gani aliyejaa visasi kama mzee wa chatle ..na bado watu wana mnyenyekea tu ..lakini mzee wa chatle alipoleta visasi vyake watu wamepga makelele mpaka basi
Nawapatiliza wana maovu ya baba zao kizazi cha kwanza hadi cha tatu
Nawarehemu maelfu elfu wanipendao na kuzishika amri zangu
 
Mkuu Hawa watu na Mungu wao wanayetufundisha tumuamini ni hatari ..mimi sikuhizi sitaki kabisa kuamini hivyo vitabu ...vina mambo mengi ya kushangaza ....waweza kusoma ukasikia Suleiman alikuwa na rundo la wanawake lakini hakuwahi kuitwa mzinzi "" lakini ukifanya hivyo wewe unaonekana mzinzi balaaa....""
Soma kwa utulivu wa roho utaelewa lakini ukisoma kwa ajiri ya kushindanisha mwili hautokaa ujue kitu
 
hapo hapo sasa "" yaani mafundisho mengine wanayotupa kupitia hizi dini na Matendo ya Mungu wanaye tuhubiria ...kama huyu Mungu angelikuwa anaishi duniani ..wallahi angestahiki kuwa jela ..muda huu"" inashangaza kusikia kwamba tunda walikula Eva na adamu...halafu na sisi wengine ambao hatukuwepo tukapewa laana ambayo inatokana na utendaji wa dhambi ambayo hatujawahi kushiriki...huyu Mungu amejaa visasi mnooo aisse...halafu hapo hapo ..anatuasa sisi tuwe tuna samehe 7× 70 wakati yeye mwenyew amediriki kutulaani hata sisi tusio husika na wala hatuwajui hao wahusika...huu siuonevu uliwazi kabisa huu""!!?
Kuna vitu haujajifunza unahitaji upate neema ndio ujifunze ipo siku utaelewa
 
kwahiyo unaona sawa mtoto kulaanika kwa kosa ambalo hajalifanya...yaani na hiyo degree yko uliyonayo unaona kabisa kuwa hilo Lina leta tija "" sindio "" ?? baba fisadi "" basiii na Watoto wake wrote ni mafisadi sindio ??
Mtoto analaanika kwa dhambi ya wazazi ila akitubu hujiondoa katika laana
 
Back
Top Bottom