Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Hebu nami nitupie machache ktk huu mjadala, kadri ambavyo nimerudia rudia tena na tena kusoma hii incident ya Noah najiwa na maswali mengi baadhi ni kama hivi!
1.Je ni muda gani ulipita tangu family hii itoke ktk safina mpaka tukio hili lilipofanyika.?
2.Canaan alikua mtoto Wa NNE Wa Shem , je huyu mtoto alikuaje kuaje mpaka Noah hakuingiwa na huruma yoyote kumpa laana nzito vile?
3. Je Ham alifuata nini ktk Tent la baba yake mpaka akamkuta ktk hali ile ilihali alikua ni MTU mzima mwenye mke na watoto na makazi yake?
6.Na kama ilikua bahati mbaya kwanini akaenda kuwasimulia nduguze tukio hilo kama vile it was funny ?
7.Yawezekana hakuwa na nia mbaya(ovu) alikwenda kwa baba yake may be kuzungumza but akamkuta amelewa akakereka na hilo hivyo kwa hasira akawambie nduguze "Ah baba mlevi kweli nilienda kuongea nae nmekuta yuko uchi kalala huko ndani" ndipo nduguze wakaenda kumfunika, lkn waliwezaje kumfunika pasipo na wao kumwona utupu ???.
Mwisho kabisa Noah alitambuaje yote haya wakati alikua hana ufahamu kwa pombe ?? Na kwanini hakutoa hata muda kutaka kujua jambo hilo kabla hajatoa hukumu ?
maneno haya!
 
Mkuu kunavitu naona wazi unajichanganya au hujavielewa. Mimi kama Mimi sihoji wala sipingi Mungu afanyapo jambo. Bali ili kuweka sawa elimu itokanayo na jambo au funzo la Mungu ndipo tunahitaji mijadala kueleweshana.
Naomba usome tena na uelewe:-
1. Mungu hamkulaani Canaan wala Ham Bali ni Nuhu na kwasababu Nuhu alikua na nguvu ya Agano na Mungu basi ile laana ikafanya kazi (kwa Canaan).
2.Canaan ni mtoto Wa NNE wa Ham na sio kizazi cha NNE cha Ham.
Mkuu Jo Venture kwanza kabisa unapaswa kuelewa kuwa Nuhu alikuwa kama Nabii wa MUNGU, hivyo basi Nabii wa MUNGU akitoa laana, laana hiyo imetoka kwa MUNGU, na Nabii wa MUNGU akitoa baraka, baraka hizo zimetoka kwa MUNGU, iko hivyo na hiyo haina ubishi.

Sasa ili niweze kujibu hoja yako vizuri, mimi nitaendelea kukujibu kwa kutumia Biblia sababu naamini kila jibu lipo ndani ya kitabu hichi hata kama majibu yamefichika. Labda naomba nikuulize wewe na wengine wote mnaouliza ni kwanini Caanan alilaaniwa na siyo Ham. Hivi ni kwanini Yakobo aliwabariki Efraimu na Manasse moja kwa moja kwa kuwawekea mikono kichwani na hakufanya hivyo kwa wajukuu wake wengine?? Kwanini alifanya hivyo kwa Efraimu na Manasse peke yao, tena kwa kumbariki mdogo ambaye ni Efraimu kwa baraka kubwa zaidi kuliko mkubwa ambaye ni Manasse?? Kwanini alimchagua mdogo??? (soma MWANZO 48:14-20)

Mimi naamini ipo sababu ya kufanya hivyo. Kumbukeni hata Yakobo alikuwa kama Nabii wa MUNGU, hivyo baraka zake au laana zake ni moja kwa moja zinatoka kwa MUNGU. Sasa turudi kwa Nuhu, kwanini alimlaani Caanani moja kwa moja na kuwaacha watoto wengine wa Hamu ambao hawakulaaniwa moja kwa moja kama ilivyokuwa kwa Caanan? Iko hivi; sisi wazazi huwa kuna mtoto tunampenda kuliko wote katika watoto wetu. Mara zote yule mtoto anayependwa zaidi na baba yake huwa kama amebeba roho ya baba yake. Inawezekana kabisa Caanani alikuwa kipenzi cha Hamu kuliko watoto wote aliokuwa nao ambao ni Kushi, Putu, Misri(Mizraim), na Caanan.

Mfano mzuri ni jinsi ambavyo Yakobo alivyokuwa anampenda sana Yusufu kuliko ndugu zake wote na Yusufu alikuwa ni mdogo, ingawa Benyamini alikuwa ndiyo mdogo zaidi. Ninachotaka kusema hapa ni kuwa roho ya baba huwa inakuwa juu ya mtoto yule anayempenda zaidi kuliko wote. Sasa inapotokea baraka zinamdondokea baba, hizi baraka zitaenda kwa mtoto yule anayependwa zaidi. Na pia kama itatokea laana ikamdondokea baba, laana hii itakwenda kwa yule mtoto anayependwa zaidi. Ndiyo kisa nikawauliza lile swali kwanini watoto wa Yusufu walipokea baraka moja kwa moja kutoka kwa babu yao Yakobo na wajukuu wengine hawakubarikiwa moja kwa moja??

Hivyo hivyo pia, kwa Nuhu kumlaani Caanani moja kwa moja ni lazima alijua kuwa Caanani ndiye kipenzi cha baba yake ambaye ni Ham. Sasa ili kumkomoa Ham ili aumie zaidi ni kumlaani yule anayempenda zaidi ambaye ndiye hasa anabeba roho yake. Siku zote laana ipo kwa ajili ya kukomoa na kuumiza, huwezi kumkomoa mtu na kumuumiza pale pasipo uma zaidi, huwezi kumkomoa mtu kama hutaharibu kile kitu anachokipenda zaidi, ukiharibu kile asichokipenda utakuwa hujamkomoa wala hatadhurika. Lakini ukiharibu kile anachokipenda kuliko vyote, hapo unakua umemkomoa na kumshikisha adabu ipasavyo. Ifahamike kuwa hawa watu wa kale, kitu laana au baraka walikuwa wanazichukulia very seriously. Ni wazi kabisa hizi laana zilimuumiza sana Ham kuliko hata Caanan aliyelaaniwa moja kwa moja.

Mfano mzuri katika hili ni lile lililowakuta Wamisri siku zile za Musa. Wote mnafahamu namna MUNGU alivyoamuru watoto wote wa kiume ambao walikuwa ni wazaliwa wa kwanza wa kila nyumba katika Misri wafe. Usiku ule akapita Malaika na kuwauwa watoto wote ambao ni wazaliwa wa kwanza wa Wamisri. Sasa hapa mtauliza; hivi wale watoto walikuwa na makosa gani mpaka wafe wao wakati siyo wao waliowatesa na kuwanyanyasa wana wa Israeli??? Kwanini waliuwawa watoto wao wasiokuwa na hatia??..... Jibu mnalijua tayari.

Iko hivi; maamuzi ya MUNGU wakati mwingine huwa hayaeleweki kwetu sisi wanadamu, lakini hiyo haina maana kuwa maamuzi yake siyo sahihi. Kwa watu ambao wanamwamini MUNGU na kuzishika Amri zake wanajua kabisa MUNGU huwa hakosei katika maamuzi yake na matendo yake. Kuna watu ambao hawamwamini MUNGU, wala hawazishiki Amri zake, watu hawa wakisoma Biblia, wanakimbilia kusema MUNGU ana makosa, wengine wanasema MUNGU ni muonevu, wanapoteza imani na kuona kama Biblia ni kitabu tu kama vitabu vingine.

Naamini ndugu yangu zitto junior na wengine wote mtakuwa mmenielewa. Swala la roho ya baba kwenda kwa mtoto wengine litakuwa limewachanganya sana, lakini fahamuni kuwa kila baba kuna mtoto wake anabeba roho yake. This is a mystery, it is paradoxical, but it is real. Mfano hata katika jamii zetu mmewahi kusikia watu wakisema; "huyu mtoto yuko kama baba yake kabisa, kuanzia kuongea mpaka kutembea". Mfano ni Adamu jinsi alivyofanana na Sethi;

"Adamu akaishi miaka mia na thelathini, akazaa mwana kwa sura yake, kwa mfano wake, akamwita jina lake Sethi". MWANZO 5:3.

Maana yake ni kwamba roho ya Adamu ilihamia kwa Sethi, licha ya kwamba Adamu alikuwa na watoto wengine wengi tu mbali na Sethi.
Cc Doto Dotto
 
pale neno la Mungu mwenye uwezo wote juu ya kila kitu duniani na mbinguni linapo jichanganya lenyewe kwa lenyewe ni hatari sana.Mkuu zitto junior mwisho wa siku hakuna mtu yyte atakaye kuwa na uthibitisho juu ya neno lolote lililo ktk vitabu vya dini kwa hiyo njia rahisi ni kuamini kitakachokupendeza moyoni mwako, sababu hivyo vitabu vinasema uatahukumiwa kutokana na unavyo amini.
nimependa ulivyo malizia hapo kwa wazungu na waaabu,wanavyo tumia maneno ya vitabu vya dini kulaghai na kutenda maovu
 
Hivyo hivyo pia, kwa Nuhu kumlaani Caanani moja kwa moja ni lazima alijua kuwa Caanani ndiye kipenzi cha baba yake ambaye ni Ham. Sasa ili kumkomoa Ham ili aumie zaidi ni kumlaani yule anayempenda zaidi ambaye ndiye hasa anabeba roho yake. Siku zote laana ipo kwa ajili ya kukomoa na kuumiza, huwezi kumkomoa mtu na kumuumiza pale pasipo uma zaidi, huwezi kumkomoa mtu kama hutaharibu kile kitu anachokipenda zaidi, ukiharibu kile asichokipenda utakuwa hujamkomoa wala hatadhurika. Lakini ukiharibu kile anachokipenda kuliko vyote, hapo unakua umemkomoa na kumshikisha adabu ipasavyo. Ifahamike kuwa hawa watu wa kale, kitu laana au baraka walikuwa wanazichukulia very seriously. Ni wazi kabisa hizi laana zilimuumiza sana Ham kuliko hata Caanan aliyelaaniwa moja kwa moja.
Mkuu sipingani na wewe.ila umejibu swali kwa mtazamo wako wewe.ungeleta aya ya ushahidi ingekuwa vizuri zaidi...Mjadala huu umetokea kwakuwa aya hazija weka wazi ni kwa nini au kwa sababubu gani? Ndio maana wewe unamtazamo wako na wengine wanamtazamo wao.
 
View attachment 775662
Habari za jioni wanajukwaa....kama kichwa cha uzi kinavyosema ningependa tujadili mada hii Kutokana na hili swali swali kuulizwa mara nyingi kwenye thread zangu nimeona nifungue uzi wake ili tujaribu kulitatua hili swali

Je ni kwanini aliyetenda dhambi ya kumuangulia uchi wa babake ni HAM ila laana ikaenda kwa mwanaye ham aliyeitwa CANAAN....

STORI YENYEWE
Mwanzo 9
20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
25 Akasema,Na alaaniwe Kanaani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
26 Akasema,Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake


Mpaka hapa tunaona anayetajwa kuchungulia uchi ni Ham ila laana inaenda kwa Canaan why?? Embu tusome nadharia hii

NADHARIA #1
Kutoka vyanzo tofauti vya kihistoria na kidini vinaelezea kisa hiki kwamba Nuhu alipolewa Ham hakuona uchi kama uchi ila inaelezwa Ham alilala na Mke wa Nuhu yaani Ham alilala na mama yake mzazi na mwisho wa siku akabeba mimba na akazaliwa Canaan na hii ilipelekea Nuhu amlaani Canaan na sio Ham sababu alikuwa kizazi cha dhambi haramu kabisa..... Na vitabu hivi vinaenda mbali na kusema Ham alimuhasi baba yake alipokuwa amelewa hiyo nayo ikapelekea Nuhu kushindwa kuzaa mtoto mara baada ya gharika!!!

VITABU VYA DINI
Nadharia hii sio tu nje ya vitabu vya dini ila hta vitabu vya dini hasa biblia inaweza kutumika kuijengea hoja embu tuangalie tafsiri yake

Mambo ya walawi 20
11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao

Walawi 18:8
8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako

NB:Kitabu cha mwanzo na mambo ya walawi vyote viliandikwa mwanzoni na Nabii Musa hivyo kama tutachukua tafsiri yake ya ''KUANGALIA UCHI WA BABA YAKO'' inamaanisha kuna ukweli juu ya nadharia hii kuwa Ham alimlala mama yake mzazi/mke wa Nuhu

Na sio kwa baba tuu Musa alielezea zaidi

Walawi 20
20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana.
21 Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana


Biblia haikuishia hapo ila ukisoma kitabu cha habakuki kinakataza mtu kulewesha jirani yake ili KUMCHUNGULIA UCHI.... Ikimaanisha kama ambayo Ham alimfanyia baba yake alipokuwa amelewa basi ndio hiko anachokataza habakuk ila sio kuchungulia kwa macho kama wengi tulivyoaminishwa

Habakkuk 2:15
15 Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!

Mistari iko mingi zaidi ya 10 inayoeleza kwamba kumchungulia kaka baba au mjomba wako ni kulala na mke wake hivyo wa waliouliza swali hili naona tunaweza conclude kwa nadharia hii kuwa HAM alimlala mke wa NUHU ndio baada ya kuja kujua alichofanya na mimba aliobeba akamlaani Canaan sababu ndio zao la dhambi hiyo iliotendeka

NADHARIA #2
Ukisoma vitabu vya dini ya kiyahudi kma midrash vinasema Canaan aliona Nuhu akiwa uchi hivyo akaenda kumuhasi kwa kutumia kamba na alipotoka ndio baadae Ham alikuta Nuhu akiwa amevuliwa nguo yeye akaishia kucheka tu badala ya kumfunika na mwisho wa siku ndipo laana akapewa Canaan kwa kufanya hicho kitendo

NADHARIA #3
Hapa inadaiwa na wanatheolojia kuwa mwandishi wa kitabu hiki alikuwa anatafuta sababu ya kuhalalisha uvamizi wa israel kwenye nchi ya Canaan so akapachika jina Canaan badala ya HAM ili ahalalishe uvamizi wa israel kwa kigezo cha kwamba NENO LA MUNGU LILIANDIKA!!!

NADHARIA #4
Inasema Canaan hakuwa mtoto wa Nuhu ila ndio alirudisha damu ya wanefili baada ya gharika baada ya Malaika aliyeitwa SHAMAEL siku chache kabla ya gharika alimlala mke wa HAM aliyeitwa Neitamuk na kumpa mimba ya mnefili CANAAN na ndio alisababisha maasi na roho ya shetani kupata nguvu upya immediately baada ya gharika na ndiye alipelekea kuzaa wanefili kama wale wa kabla ya gharika hivyo kwa kuona uovu wa HAM aliofanya, hasira za Nuhu zikaishia kwa CANAAN sababu ndio alikuwa uzao wa roho ya kishetani (SHAMAEL) iliosababisha hadi dhambi kurudi baada ya gharika

BAADA YA LAANA
Tunaona canaan akizaa watoto walioishi miji kama sodoma Gomorrah na Gaza zote israel ya sasa na walikuwa na falme zenye nguvu sana ila kwa kuwa laana hii ya Nuhu iliwafuata ilikuja kutimizwa na watoto wa yakobo (uzao wa SHEM) waliokuja kuwapora nchi yao ya CANAAN na wakawachinja takribani kizazi chote rejea kitabu cha joshua na kumbukumbu la torati na hata wachache waliobaki waliendelea kuteswa sana na waisrael na BIFU hili lilienda hadi kwa Yesu alipokataa kumponya mwanamke wa kanaani

Mathayo 15:22
22 Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa


CANAAN NA WANEFILI
Hoja ya kwamba canaan huenda alikuwa uzao wa malaika shamael ama uzao wa ajabu wa Ham na mama yake watoto wake wote walikuwa wanefili yaani majitu ya futi mpaka 28..... Kati ya watoto wote wa ukoo wa Nuhu hakuna mtu aliyezaa wanefili kuliko Canaan na makabila yote ya warefai kipindi hicho walitoka familia ya canaan wawe wayebusi wagilgal waamori wahiti wahivi n.k je huu unaweza kuwa ushahidi kuwa hakuwa mtoto wa uzao wa kawaida ndio maana akazaa wanefili watupu huku na yeye akiwa mnefili???

HAM KWENYE UISLAM
Sijapata popote kwenye Quran inapoandikwa kuhusu laana hii ya Canaan ila kwenye ukristo ma uyahudi ndipo imetajwa. Ila ukisoma hadeeth mbalimbali na machapisho ya wasomi nguli wa kiislam wa mwanzo kabisa kina Muhammad ibn-jarir al tabari pamoja na ibn khaldun wanaeleza kwamba HAM alilaaniwa sababu akiwa kwenye Safina ya Nuhu alimlala mke wake kitu kilichokatazwa hivyo alilaaniwa kwa kupewa ngozi nyeusi na ndio maana watoto wake wote wakawa weusi!!! So hawa angalau wamesema HAM alilaaniwa ila kwa kosa tofauti.... Hivyo bado hawajatupa jibu la kisa cha Nuhu na Canaan

HITIMISHO
Mada hii imetumiwa sana na wazungu wakoloni hasa karne ya 19 kuhalalisha ukoloni wa watu weusi kwa kigezo kuwa mwafrika alilaaniwa ila hoja hii naipinga sababu canaan alilaaniwa peke yake na kizazi chake kwa ukubwa kilishafutwa ila waafrika 80% walitokana na kizazi cha wale watoto 3 wa HAM ambao laana hii haikuwahusu hivyo natumia fursa kupinga propaganda hiyo rasmi na ni vizuri waafrika tupende kusoma historia yetu ili wahuni wachache wasipotoshe ukweli

Naomba kuwasilisha

Karibuni wanajukwaa wote tusaidiane kujadili kuhusu nadharia hizi,
Kipindi waingereza wakiitawala marekani walihangaika sana kutafuta vibarua katika mashamba yao huko marekani ili kupata malighafi kwajili ya viwanda vyao huko UK!

Baada ya wahindi weusi kushindwa kufanya kazi wakaamua kuwatumia Wazungu wenzao ambao waliokua wemehukumiwa vifungo jela kwa makosa mbali mbali.
Nao pia waliwashindwa kwakua ni wazumgu wenzao na walijua sheri na haki zao za msingi hivyo ilikua ngumu kuwaburuza kwa maslah yao.

Ndipo alipotokea Bishop mmoja akawawapa kisa cha NUHU na watoto wake Hamu, Shame na Yafeth. Kuhusu NUHU alipomlaani huyo mtoto wake Hamu akawa mweusi na kwa laana ile aliapizwa kuwa atakuwa mtumwa wa ndugu zake (Shamu na Yafeth) ambao wao ni weupe.

Hivyo bwana Bishop akawaambia waingereza "Kwanini muhangaike kutafuta vibarua wakati kuna huyu Hamu ambaye ana laana na kwa laana ile atakua mtumishe wetu!? hivyo lazima mumtafute ili aje amitumikie"
Baada ya hapo Wazungu wakaanza kumtafuta Hamu na kizazi chake kwa utambulisho wa rangi yao ambayo ni nyeusi.

Ndipo wapokutana na mtu mmoja (nahisi ni Vasco Dagama ila sina uhakika) akawambia mbona watu weusi wapo wengi sana Africa? Ndio wakaingia Africa kwa mbinu mbali mbali ila lengo lilikua ni kukifuata kizazi cha ndugu yao Hamu ambacho kiasili kimelaaniwa ila wakakitumiishe kama ilivyoagizwa.
Kweli walifanikiwa na wakawachukua Waafrika wengi kwenda USA kwenye mashamba yao na kuwatumikisha, na walikua walikua na nguvu sana, baada ya USA kupata uhuru wakahamia kabisa kwao (kwakina hicho kizazi cha Hamu ambapo ni Africa) kuendelea kuwatumia kwa mbinu mbali mbali kwa maslah yao!
Mwisho.
 
Mkuu sipingani na wewe.ila umejibu swali kwa mtazamo wako wewe.ungeleta aya ya ushahidi ingekuwa vizuri zaidi...Mjadala huu umetokea kwakuwa aya hazija weka wazi ni kwa nini au kwa sababubu gani? Ndio maana wewe unamtazamo wako na wengine wanamtazamo wao.
Mkuu ganster siyo kila kitu kilichoandikwa kwenye Biblia kimewekwa wazi wazi, lakini ukiisoma vizuri Biblia na kuielewa basi hata vile vilivyofichika utaelewa maana yake. Mfano mzuri ni hili Swali; kwanini Efraimu na Manasse walibarikiwa moja kwa moja na babu yao Yakobo kwa kuwekewa mikono kichwani na wajukuu wengine hawakubarikiwa moja kwa moja???

Nini cha ziada walichokifanya Efraimu na Manasse kuzidi wenzao, maana wakati wanabarikiwa walikuwa ni watoto wadogo tu??

Ukiweza kujua ni kwanini hawa walibarikiwa wakiwa wadogo, pia utafahamu ni kwanini Caanani alilaaniwa akiwa mdogo.
 
Msingi wa mada nimeuelewa sana ila kuna kitu hapo kuhusu laana ya vizazi kwa vizazi mlijaribu kuzungumzia kama sehemu ya utetezi sasa ndio nataka maoni yako kuhusu hili jambo kutoa laana kwa vizazi ambavyo avijashiriki kwenye uovu uoni sio jambo jema maana mnawanyima fursa ya kutubu ni ilo mkuu
watakwambia mungu ..hapangiwi...yaani trilion 1.5 aibe jiwe halafu hukumu apew jesca like serious "" Mungu huyu Mungu gani aliyejaa visasi kama mzee wa chatle ..na bado watu wana mnyenyekea tu ..lakini mzee wa chatle alipoleta visasi vyake watu wamepga makelele mpaka basi
 
Mkuu lawama na laani ni vitu tofauti sana. Waziri hawezi kuua mtu huko Iringa then Magufuli ndo akamatwe Mmmh!! hapana.

Haya maandiko ya Bible me yananivuruga sana Ukisoma Mwanzo 3:17 Mungu anailaani ardhi sababu ya Adamu sasa ardhi ilifanya kosa gani pale Eden?

Yoshua 7:24+ Akani alifanya dhambi ya kuiba aliteketezwa yeye na uko wake mzima hadi ng'ombe, punda, na vitu vyake vyote. sasa wao viumbe wengine walikosa nini wahusike kwenye adhabu ya Akani?

Sikumbuki ni kitabu gani but utanisaidia kama unakijua. kuna mtumishi mmoja wa Elisha Nabii alifanya kosa kumuomba zawani Naamani alieponywa ukoma na Elisha nabii. Huyo mtumishi alipatwa na ukoma yeye na ukoo mzima. sasa wao ndugu zake wengine walifanya kosa gani mpk wahusishwe kwenye adhabu ya huyo mtumishi?

Najiuliza Mungu yukoje? na anatumia kanuni, sheria, utaratibu gani kuadhibu watu vitu ambavyo hata havijahusika kuadhibiwa pasipo kosa?
Mkuu Hawa watu na Mungu wao wanayetufundisha tumuamini ni hatari ..mimi sikuhizi sitaki kabisa kuamini hivyo vitabu ...vina mambo mengi ya kushangaza ....waweza kusoma ukasikia Suleiman alikuwa na rundo la wanawake lakini hakuwahi kuitwa mzinzi "" lakini ukifanya hivyo wewe unaonekana mzinzi balaaa....""
 
Yani hapo ndo unanivuruga kabisa. Mfano wewe unikosee halafu eti hata mtoto utakaemzaa nimchukie? ya nn sasa itakuwa sina utu ubinadamu

Sasa Mungu ana hekima kutuzidi sisi iweje aendelee kukomalia maovu waliotenda adamu na Hawa adhabu tupate sisi? Serious!! is not fair
hapo hapo sasa "" yaani mafundisho mengine wanayotupa kupitia hizi dini na Matendo ya Mungu wanaye tuhubiria ...kama huyu Mungu angelikuwa anaishi duniani ..wallahi angestahiki kuwa jela ..muda huu"" inashangaza kusikia kwamba tunda walikula Eva na adamu...halafu na sisi wengine ambao hatukuwepo tukapewa laana ambayo inatokana na utendaji wa dhambi ambayo hatujawahi kushiriki...huyu Mungu amejaa visasi mnooo aisse...halafu hapo hapo ..anatuasa sisi tuwe tuna samehe 7× 70 wakati yeye mwenyew amediriki kutulaani hata sisi tusio husika na wala hatuwajui hao wahusika...huu siuonevu uliwazi kabisa huu""!!?
 
Duh hii hoja nzito sana..... Nimewahi kusikia claims hizi kuwa kuna uwezekano mwandishi wa kitabu cha mwanzo alionyesha laana imekwenda kwa CANAAN na kwamba uzao wake watakuwa watumwa kwa SHEM yote haya kuwaandaa watu kisaikolojia ili hata wakija kuvamia waseme MAANDIKO YALISHATABIRI!!! Sasa wwe umeiongelea ndio umenipa mwanga zaidi kuwa huenda kuna propaganda zilichezwa hapa

Aseee hatari sana kama hii ni kweli
umeona sasa ..."" basiii kama ndio hivyo ..nashawishika kusema kuwa hivi vitabu ..havipaswi kuaminika aissee....vina ji contradict mnoo""
 
Mkuu hii ipo hivi mnyororo huu hapa chini

Baba-yako-na-kaka-yako-wewe-watoto-wa-kaka-yako-watoto-wa-kwako

Familia hii ina vinasaba vya baba yako kama baba yako ametenda maovu damu ya cheni hii yote inahusika hata vyombo vya ndani vina husika lakini kama ukiamua kujitoa katika hili utakuwa umejiweka huru karibu na Mungu wako
Lakini ukiendelea kuwepo katika hii cheni laana haikuachi
Kwa hiyo fahamu kabisa uovu wako utasababisha laana kwa kizazi chako chote
kwahiyo unaona sawa mtoto kulaanika kwa kosa ambalo hajalifanya...yaani na hiyo degree yko uliyonayo unaona kabisa kuwa hilo Lina leta tija "" sindio "" ?? baba fisadi "" basiii na Watoto wake wrote ni mafisadi sindio ??
 
Yani mtu alifanya kosa adhabu yake ni kunyongwa sasa eti unakusanywa ukoo wake wote, mifugo yake yote, vyombo vya ndani vyote, vinachomwa moto hadi nyumba? hii si haki, na si sawa
hahaaa...hatari sana "" tukiambiwa tuna angamia kwakukosa maarifa tunakuwa wakali "" Yaani mtoto asiyejua kitu ahukumiwe kwa ujinga wa mzazi wake ...na bado mnaona sawa ....halafu bado wanajiita wasomi huko shuleni walikwenda kusomea ujinga au ""
 
Yaani doto Mungu ana makusudi yake ndiye anaye fahamu kwanini iwe hivi
uwongo "" Mungu anazushiwa hawezi kuwa katili kiasi hiki....nikuulize swali ..?? kama maamuzi hayo anayoyafnya Mungu " angekuwa nayo kiongozi wa kibinaadamu "" angeonekana ni mtu wanamna gani "" mfano " raisi wa nchi aamue " kumkamata mtu yeyote ambaye ni muhaini " kisha amuhukumu " kifungo kuanzia yeye(muhaini ) mpaka familia yake yote " na mifugo yke " huyo raisi ataeleweka vipi na jamii ??..na kama huyo raisi ataonekana ni muonevu " iweje Mungu aonekane mtakatifu katika maamuzi yake onevu kama hayo "" ?
 
Kipindi waingereza wakiitawala marekani walihangaika sana kutafuta vibarua katika mashamba yao huko marekani ili kupata malighafi kwajili ya viwanda vyao huko UK!

Baada ya wahindi weusi kushindwa kufanya kazi wakaamua kuwatumia Wazungu wenzao ambao waliokua wemehukumiwa vifungo jela kwa makosa mbali mbali.
Nao pia waliwashindwa kwakua ni wazumgu wenzao na walijua sheri na haki zao za msingi hivyo ilikua ngumu kuwaburuza kwa maslah yao.

Ndipo alipotokea Bishop mmoja akawawapa kisa cha NUHU na watoto wake Hamu, Shame na Yafeth. Kuhusu NUHU alipomlaani huyo mtoto wake Hamu akawa mweusi na kwa laana ile aliapizwa kuwa atakuwa mtumwa wa ndugu zake (Shamu na Yafeth) ambao wao ni weupe.

Hivyo bwana Bishop akawaambia waingereza "Kwanini muhangaike kutafuta vibarua wakati kuna huyu Hamu ambaye ana laana na kwa laana ile atakua mtumishe wetu!? hivyo lazima mumtafute ili aje amitumikie"
Baada ya hapo Wazungu wakaanza kumtafuta Hamu na kizazi chake kwa utambulisho wa rangi yao ambayo ni nyeusi.

Ndipo wapokutana na mtu mmoja (nahisi ni Vasco Dagama ila sina uhakika) akawambia mbona watu weusi wapo wengi sana Africa? Ndio wakaingia Africa kwa mbinu mbali mbali ila lengo lilikua ni kukifuata kizazi cha ndugu yao Hamu ambacho kiasili kimelaaniwa ila wakakitumiishe kama ilivyoagizwa.
Kweli walifanikiwa na wakawachukua Waafrika wengi kwenda USA kwenye mashamba yao na kuwatumikisha, na walikua walikua na nguvu sana, baada ya USA kupata uhuru wakahamia kabisa kwao (kwakina hicho kizazi cha Hamu ambapo ni Africa) kuendelea kuwatumia kwa mbinu mbali mbali kwa maslah yao!
Mwisho.
Asee hawa wazungu sio watu kabisa mkuu
 
mkuu nimefuatilia kwa ufupi, nimegundua kuna nadharia rundo kuhusu hilo tukio.
na wengine wameenda mbali nadhani umekwepa kuiandika kwa sababu ya kimaadili Huyo Ham alimsodoma (homosexuality) baba yake au hiyo hoja ya castration pia. hii ni kwa mujibu wa babylonian talmud na tafsiri za baadhi ya marabbi. wameenda mbali hadi kutafsiri neno la kigiriki (kutoka kwenye septugiant ) "akamuona" wametafsiri au weka maana ya kimapenzi zaidi.

MAONI YANGU ZAIDI:
Naendelea kujikita kwenye maandiko matakatifu (bibilia ) tu kujenga baadhi ya hoja.

1:Hakuna mambo ya kusodomana, wala kuziniana kwenye hilo tukio, nadhalia hizo naona zinamadhaifu hata jitihada za kuzihusianisha na aya za mbele zisizoumana kimaana.

2: Kwa nini Ham asilaaniwe alaaniwe mwanaye?
*Kumbuka laana hiyo imetolewa na Nuhu sio Mungu. hivyo inatufikirisha zaidi.
*Mungu alikuwa amekwishambariki HAMU.
" Naye Mungu akambariki Noa na wanawe(ham,shem na yapheti), akawaambia: “Zaeni, muwe wengi, mjaze dunia." Mwanzo 9:1
hapo ni wazi Mungu kambariki HAMU hivyo laana ya nuhu inaweza isifanye kazi, na wenda imeandikwa kuwa inaenda kwa kaanani kwa sababu ndio mzao wake ambae alikuwa hana hizo baraka zilizotolewa na Mungu.
Maoni haya ambayo nayaunga mkono yanaumana na Magombo ya kale yaliyochimbuliwa (dead sea scrolls 4Q252) wakizungumzia tukio hilo.
kwenye biblia unasema "atakae kulaani nitamlaani na atakae kubariki nitambariki" nazani baada ya nuh kujua mungu kashambariki huyo mwanae ilibidi asira amalizie Kwa mjukuu wake
 
Back
Top Bottom