Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

View attachment 775662
Habari za jioni wanajukwaa....kama kichwa cha uzi kinavyosema ningependa tujadili mada hii Kutokana na hili swali swali kuulizwa mara nyingi kwenye thread zangu nimeona nifungue uzi wake ili tujaribu kulitatua hili swali

Je ni kwanini aliyetenda dhambi ya kumuangulia uchi wa babake ni HAM ila laana ikaenda kwa mwanaye ham aliyeitwa CANAAN....

STORI YENYEWE
Mwanzo 9
20 Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda mizabibu;
21 akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
22 Hamu, baba wa Kanaani, akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
23 Shemu na Yafethi wakatwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; na nyuso zao zilielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao.
24 Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua mwana wake mdogo alivyomtendea.
25 Akasema,Na alaaniwe Kanaani;Atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake.
26 Akasema,Na atukuzwe BWANA Mungu wa Shemu;Na Kanaani awe mtumwa wake


Mpaka hapa tunaona anayetajwa kuchungulia uchi ni Ham ila laana inaenda kwa Canaan why?? Embu tusome nadharia hii

NADHARIA #1
Kutoka vyanzo tofauti vya kihistoria na kidini vinaelezea kisa hiki kwamba Nuhu alipolewa Ham hakuona uchi kama uchi ila inaelezwa Ham alilala na Mke wa Nuhu yaani Ham alilala na mama yake mzazi na mwisho wa siku akabeba mimba na akazaliwa Canaan na hii ilipelekea Nuhu amlaani Canaan na sio Ham sababu alikuwa kizazi cha dhambi haramu kabisa..... Na vitabu hivi vinaenda mbali na kusema Ham alimuhasi baba yake alipokuwa amelewa hiyo nayo ikapelekea Nuhu kushindwa kuzaa mtoto mara baada ya gharika!!!

VITABU VYA DINI
Nadharia hii sio tu nje ya vitabu vya dini ila hta vitabu vya dini hasa biblia inaweza kutumika kuijengea hoja embu tuangalie tafsiri yake

Mambo ya walawi 20
11 Na mtu mume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao

Walawi 18:8
8 Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako

NB:Kitabu cha mwanzo na mambo ya walawi vyote viliandikwa mwanzoni na Nabii Musa hivyo kama tutachukua tafsiri yake ya ''KUANGALIA UCHI WA BABA YAKO'' inamaanisha kuna ukweli juu ya nadharia hii kuwa Ham alimlala mama yake mzazi/mke wa Nuhu

Na sio kwa baba tuu Musa alielezea zaidi

Walawi 20
20 Tena mtu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana.
21 Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana


Biblia haikuishia hapo ila ukisoma kitabu cha habakuki kinakataza mtu kulewesha jirani yake ili KUMCHUNGULIA UCHI.... Ikimaanisha kama ambayo Ham alimfanyia baba yake alipokuwa amelewa basi ndio hiko anachokataza habakuk ila sio kuchungulia kwa macho kama wengi tulivyoaminishwa

Habakkuk 2:15
15 Ole wake yeye ampaye jirani yake kileo, wewe utiaye sumu yako, na kumlevya pia, ili kuutazama uchi wao!

Mistari iko mingi zaidi ya 10 inayoeleza kwamba kumchungulia kaka baba au mjomba wako ni kulala na mke wake hivyo wa waliouliza swali hili naona tunaweza conclude kwa nadharia hii kuwa HAM alimlala mke wa NUHU ndio baada ya kuja kujua alichofanya na mimba aliobeba akamlaani Canaan sababu ndio zao la dhambi hiyo iliotendeka

NADHARIA #2
Ukisoma vitabu vya dini ya kiyahudi kma midrash vinasema Canaan aliona Nuhu akiwa uchi hivyo akaenda kumuhasi kwa kutumia kamba na alipotoka ndio baadae Ham alikuta Nuhu akiwa amevuliwa nguo yeye akaishia kucheka tu badala ya kumfunika na mwisho wa siku ndipo laana akapewa Canaan kwa kufanya hicho kitendo

NADHARIA #3
Hapa inadaiwa na wanatheolojia kuwa mwandishi wa kitabu hiki alikuwa anatafuta sababu ya kuhalalisha uvamizi wa israel kwenye nchi ya Canaan so akapachika jina Canaan badala ya HAM ili ahalalishe uvamizi wa israel kwa kigezo cha kwamba NENO LA MUNGU LILIANDIKA!!!

NADHARIA #4
Inasema Canaan hakuwa mtoto wa Nuhu ila ndio alirudisha damu ya wanefili baada ya gharika baada ya Malaika aliyeitwa SHAMAEL siku chache kabla ya gharika alimlala mke wa HAM aliyeitwa Neitamuk na kumpa mimba ya mnefili CANAAN na ndio alisababisha maasi na roho ya shetani kupata nguvu upya immediately baada ya gharika na ndiye alipelekea kuzaa wanefili kama wale wa kabla ya gharika hivyo kwa kuona uovu wa HAM aliofanya, hasira za Nuhu zikaishia kwa CANAAN sababu ndio alikuwa uzao wa roho ya kishetani (SHAMAEL) iliosababisha hadi dhambi kurudi baada ya gharika

BAADA YA LAANA
Tunaona canaan akizaa watoto walioishi miji kama sodoma Gomorrah na Gaza zote israel ya sasa na walikuwa na falme zenye nguvu sana ila kwa kuwa laana hii ya Nuhu iliwafuata ilikuja kutimizwa na watoto wa yakobo (uzao wa SHEM) waliokuja kuwapora nchi yao ya CANAAN na wakawachinja takribani kizazi chote rejea kitabu cha joshua na kumbukumbu la torati na hata wachache waliobaki waliendelea kuteswa sana na waisrael na BIFU hili lilienda hadi kwa Yesu alipokataa kumponya mwanamke wa kanaani

Mathayo 15:22
22 Na tazama, mwanamke Mkanaani wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo.
23 Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.
24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa


CANAAN NA WANEFILI
Hoja ya kwamba canaan huenda alikuwa uzao wa malaika shamael ama uzao wa ajabu wa Ham na mama yake watoto wake wote walikuwa wanefili yaani majitu ya futi mpaka 28..... Kati ya watoto wote wa ukoo wa Nuhu hakuna mtu aliyezaa wanefili kuliko Canaan na makabila yote ya warefai kipindi hicho walitoka familia ya canaan wawe wayebusi wagilgal waamori wahiti wahivi n.k je huu unaweza kuwa ushahidi kuwa hakuwa mtoto wa uzao wa kawaida ndio maana akazaa wanefili watupu huku na yeye akiwa mnefili???

HAM KWENYE UISLAM
Sijapata popote kwenye Quran inapoandikwa kuhusu laana hii ya Canaan ila kwenye ukristo ma uyahudi ndipo imetajwa. Ila ukisoma hadeeth mbalimbali na machapisho ya wasomi nguli wa kiislam wa mwanzo kabisa kina Muhammad ibn-jarir al tabari pamoja na ibn khaldun wanaeleza kwamba HAM alilaaniwa sababu akiwa kwenye Safina ya Nuhu alimlala mke wake kitu kilichokatazwa hivyo alilaaniwa kwa kupewa ngozi nyeusi na ndio maana watoto wake wote wakawa weusi!!! So hawa angalau wamesema HAM alilaaniwa ila kwa kosa tofauti.... Hivyo bado hawajatupa jibu la kisa cha Nuhu na Canaan

HITIMISHO
Mada hii imetumiwa sana na wazungu wakoloni hasa karne ya 19 kuhalalisha ukoloni wa watu weusi kwa kigezo kuwa mwafrika alilaaniwa ila hoja hii naipinga sababu canaan alilaaniwa peke yake na kizazi chake kwa ukubwa kilishafutwa ila waafrika 80% walitokana na kizazi cha wale watoto 3 wa HAM ambao laana hii haikuwahusu hivyo natumia fursa kupinga propaganda hiyo rasmi na ni vizuri waafrika tupende kusoma historia yetu ili wahuni wachache wasipotoshe ukweli

Naomba kuwasilisha

Karibuni wanajukwaa wote tusaidiane kujadili kuhusu nadharia hizi,
Hapo kwa Yesu kukataa kumponya mwanamke mkanaani, si kweli alimponya tena kwa msifu ya kuwa hajaona imani km ya yule mwanamke kisha akamponya
 
Hapo kwa Yesu kukataa kumponya mwanamke mkanaani, si kweli alimponya tena kwa msifu ya kuwa hajaona imani km ya yule mwanamke kisha akamponya
Mwanzo Yesu alipogundua yule mama ni uzao wa CANAAN alikataa kumponya mkuu ila mwanamke alilazimisha na Yesu akasema IMANI YAKO IMEKUPONYA ina maana kama angekata tamaa asingeponywa....

Hivi mtu anaomba aponywe alafu anajibiwa hivi wewe ungetafsiri vp

24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa
 
Mtoto analaanika kwa dhambi ya wazazi ila akitubu hujiondoa katika laana
mtoto kosa lake nilipi !? sasa "" wewe unaweza kwenda kumchukia mtoto wa mtu aliyekutapeli""? na ukawa na kinyongo na huyo mtoto mpka pale ambapo atakuja kukuomba msamaha"" kwa kosa alilofanya baba yake ndio umsamehe ""?nakutoa hicho kinyongo""
 
Kuna vitu haujajifunza unahitaji upate neema ndio ujifunze ipo siku utaelewa
sihitaji kujifunza hayo manadharia..."" kama Mungu wenu anampatia laana mtoto mchanga asiyejua..kitu kisa tu baba yake ni fisadi "" sasa kuna haja gani ya kukaa na kujifunza magundisho Yke "" huoni kuwa na mimi nitaanza kuwa hukumu watu wasiohusika kunitendea ubaya kisa tu "" dada/kaka ..baba/mama yao alinifanyiaga ubaya""
 
Wapi nimegeneralise si nimesema ni mawazo ya WASOMI WA KIISLAM na sio UISLAM kama DINI ama QURAN!! au Al tabari ni mkristo?? Anyway ulitaka nisemeje mkuu embu nishauri ili nisirudie makosa

Nlishasema toka mwanzo kama wwe humtambui Al tabari wengine wanamtambua hasa washia... kama wwe unaona washia wako wrong kuna maeneo ushia unatambulika kama Iran na miskiti yao wanaquote sana mafundisho yake na wanaitwa waislam sasa ulitaka nisiweke mafundisho yake kisa wasunni hamutambui washia??? Tutafika kweli

Ni hivi Al tabari ni muislam na wanazuoni wakiislam hasa washia wanatambua mafundisho yake sasa whether wwe humtambui huo ni mjadala mwingine ila kwa kuwa machapisho yake yanatambuliwa na jumuiya za waislam basi sio mbaya kuweka mawazo yake hapa kma halikufai liache wengine wajifunze hapa tunaweka source zote hata za wapagani na wachawi as long as tunaunganisha dots kupata jibu moja

So samahani kama nimekukwaza ila huo ndio msimamo wangu
Mkuu huyo wala asikuapasue kichwa "" kitu ambacho tunapaswa kukifahamu"" kwanza hizi dini zote mbili zina madhehebu tofauti na yote yameletwa either na wazungu au waarabu "" sisi watu weusi ni watu wa mapokeo tu Bender's fuata upepo...na hayo madhehebu yamekuwa yanajipinga kimaandiko wao kwa wao "" so huwenda ikawa huyo mwanazuoni uliye mquote hadithi yake ikawa na mantiki " lakini kwakuwa anatoka katila dhehebu tofauti na mtoa comment akaona kuwa huyo mwanazuoni nimuongo na hayupo sahihi"" na wakati huo huo Jamii ya dhehebu la huyo mwanazuoni linamuhesabu mwanazuoni wao kuwa ni Moja ya wasomi nguli kwao "" nahayo ndio matatizo yaliyopo katika hzi dini kwanza wao kwa wao wanapingana"" mfano mdogo RAMADHANI hiyo yaja...katika mfungo kuna madhehebu ndani ya huo huo uislam yanakinzana dhidi ya mwezi muandamo..kuna ambao wataanza kufunga kwa madai mwezi umeonekana na kuna ambao watapinga kuonekana kwa mwezi watafunga siku inayofuatia....so hapa uhalali wa mafundisho utategemea na aina ya dhehebu ambalo waumini wanatokea.....
kwahiyo Hawa Jamaa wasikuchanganye maana wao wenyewe tu ni zege tosha.,..full kuchanganyana
 
Luth alipo lala wanawe wa kike bible haikuficha, so. Sioni sababu wafiche kwa hamu, ni speculation potofu.
 
Mwanzo Yesu alipogundua yule mama ni uzao wa CANAAN alikataa kumponya mkuu ila mwanamke alilazimisha na Yesu akasema IMANI YAKO IMEKUPONYA ina maana kama angekata tamaa asingeponywa....

Hivi mtu anaomba aponywe alafu anajibiwa hivi wewe ungetafsiri vp

24 Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
25 Naye akaja akamsujudia, akisema Bwana, unisaidie.
26 Akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa
duuuhh""
 
Mtoto analaanika kwa dhambi ya wazazi ila akitubu hujiondoa katika laana
wakati huku duniani " mtoto mchanga anapozaliwa huwa tuna muona kuwa ni innocent mpaka kufikia hatua ya kumuita malaika "" kumbe Mungu anakuwa ameshamlaani "" kisa " mama yake alizini na Mjomba wake. ndio akazaliwa huyo mtoto" "" hahaaaa Mungu huyu noma "" ...kama ndio hivyo hiyo nadharia ya Kuwaita Watoto ni malaika kuanzia leo ife ""maana Kuna baadhi yanayo laana ya Mungu kutokana na ushirika wa dhambi ambao ulitendwa na wazazi wao "" Mungu hana huruma hata na Watoto "" kashindwa hata nasie binaadamu ambao tunatambua kuwa Watoto ni innocent mpaka tumefikia hatua ya kuwaita malaika "" sasa mnaposemaga kuwa Mungu baba ni Mwenye huruma "" hiyo huruma anaitoa wapi "" wakati hapa tunaona kuwa hata binaadamu aliowaumba wamemshinda huruma '''
 
Pia.

Kama Nuhu alimpenda sana Ham mpaka kufikia kushindwa kumlaani kwa mahaba yake kwake..Akaamua kumlaani mjukuu..

Iweje.
Mungu aikubali kuipitisha hiyo laana iliyobebwa na Mahaba/Chuki ya kibinadamu?
hahaaa..haya maswali hawataki kuyajibu "" utasikia wanakwambia kuwa unasoma bibilia kama gazeti"" kwanza mtume wa Mungu anakunywaje pombe "" yaaani hata madhara ya pombe hayajui kweli ""? kumbe ndio maana watu wake hawakuwa wanamuelewa "" kwa sababu walikuwa wanajua kuwa na bi wao ni mlevi ""
 
mtoto kosa lake nilipi !? sasa "" wewe unaweza kwenda kumchukia mtoto wa mtu aliyekutapeli""? na ukawa na kinyongo na huyo mtoto mpka pale ambapo atakuja kukuomba msamaha"" kwa kosa alilofanya baba yake ndio umsamehe ""?nakutoa hicho kinyongo""
Mbona baraka au utajiri mtoto anarith, basi hivyo hivyo na laana pia.
 
Aliye ona uchi ni Ham baba wa canaani

5 mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Kutoka 20 :5

Swali fikirishi, hii laana ya kizazi cha tatu mpaka cha nne hutolewa na Mungu ama yoyote?,
 
Mbona baraka au utajiri mtoto anarith, basi hivyo hivyo na laana pia.
kwahiyo huyo "" Mungu mmeanza kumfananisha utendaji wake na wakibinaadamu MAKUBWA !!!"" sasa""? kwahiyo nikikwambia mbona binaadamu nae huwa anazini " kwa hiyo Mungu nae anazini nitakuwa nimekingiuka au ""!?."" sipingi kuhusu mtoto kurithi laana Bali hoja yangu ""nikwamba..huyo anayeitoa hiyo laana nimuonevu "" maana anampa laana kiumbe ambaye hajahusika katika utendaji ulisababisha hiyo laana """
 
Luth alipo lala wanawe wa kike bible haikuficha, so. Sioni sababu wafiche kwa hamu, ni speculation potofu.
Okay upo sahihi kwa mtazamo wako ila inakuwa haijibu swali letu kwamba kwanini laana iende kwa canaan kma kwenye hilo kosa hausiki popote.... Tukijua sababu basi nadharia hizi zinakuwa hazina maana
 
Okay upo sahihi kwa mtazamo wako ila inakuwa haijibu swali letu kwamba kwanini laana iende kwa canaan kma kwenye hilo kosa hausiki popote.... Tukijua sababu basi nadharia hizi zinakuwa hazina maana
Ndio sijajibu why canaan, ila nimeondoa ule mtazamo kwamba Ham alilala na mke wa baba yake.
Kuhusu why canaan nimeona tayari limejibiwa na wadau humu vizuri tu. Mfano mwingine ni mfalme suleiman ndiye aliye rithi kiti cha daudi baba yake japo yeye alikuwa mdogo, wakati kaka zake walikuwepo. mambo ya malango mkuu.
 
Back
Top Bottom