Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Mkuu..

Hebu nisaidie hapo uliposema Mtume Muhammad alisema alishushiwa Quran Jerusalem..

Sijaelewa..
 
Nini Maana ya Taifa Teule?..
 
Ni

niajabu mkuu haki yake mwenye haki na uovu wake mwenye uovu kila mtu ahukumiwe kwa matendo yake laana mpaka kizazi cha nne ni hadaa tupu
MUNGU hachunguziki kwani ukisoma kitabu cha mwanzo 15;8-16 kipindi ambacho MUNGU anamwambia Abraham amtolee sadaka katika kuitoa ile sadaka Abraham anasinzia ikawa kama sababu angalau biblia haitaji kama kosa ambalo linapelekea kizazi chake cha 4 kitaenda utumwani miaka mia 4 kwaio hoja ya msingi kwamba BWANA MUNGU hachunguziki na anaweza kutumia ukamilifu wake kwenye namba ndomana ukisoma maandiko namba 7 inaonyesha ukamilifu wa jambo 4 inaonyesha ukamilifu wa vizazi 40 inaonyesha ukamilifu wa toba
 
Hakuna mwanadamu anayeweza kuwalaani wana wa Israeli na laana hiyo ikatokea au ikafanyakazi, hakuna... Lakini, MUNGU peke yake anaweza kuwalaani Waisraeli
Mwanzo 49
5 Simeoni na Lawi ni ndugu;Panga zao ni silaha za jeuri.
6 Nafsi yangu, usiingie katika siri yao,Fahari yangu usiungane na kusanyiko lao,Maana katika ghadhabu yao walimuua mtu,Na kwa ukaidi wao walikata mshipa wa ng?ombe;
7 Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali,Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma.Nitawagawa katika Yakobo,Nitawatawanya katika Israeli


Mkuu hapa vp mbona kuna waisrael wamelaaniwa hapa ama kwa kuwa imetoka kwa Muisrael mwenzao?? Ikiwa na maana muisrael akimlaani muisrael mwenzake its ok ila mtu asiye musirael akimlaani muisrael ndio haifanyi kazi??

Simply una maana waisrael ndio wenye haki pekee ya kulaani mtu??
 
Mkuu ukisoma mwanzo 49 unaona kwamba yakobo ambae ndo israel mwenyewe anawakusanya wanae anawaambia yatakayowatokea siku za mwisho angalau baraka haziwezi kuwa sawa ndomana hata YUSUPH na alipewa makabila mawili EFRAIMUnaMANASE na pia kama umekosea utapewa kinachostairi, lakini katika kule kuwa wana wa yakobo ni baraka tosha ndomanai wote waligawiwa nchi na YOSHUA walivyorudi kanani
 
hapo naona hii ni historia tu na kwenye historia error haiwezi kosekana aliyeleta huu ujumbe kwa mara ya kwanza inform of written document huenda alikoseaga na waliofuata kukopi maandishi haya either waliyadadavua na kuyatafsiri hivyo wakayaharibu zaidi na ndio mpaka sasa kuna mkanganyiko kwenye swala hili pia hapa huwezi pata jibu labda utafute vitabu vya kidini vya kale kabisa vyenye lugha mama ya kipindi hicho ndipo ujarbu kufanya translation kwa yaliyoandikwa hapo utapata jibu halisi

pamoja kiongozi zitto jr maada hii nzuri
 
Mkuu maelezo yako nimeyaelewa ila Son of Gamba alisema HAKUN mtu anaweza mlaani muisraeli yeyote na hiyo laana ikafanya kazi ndio nkamuuliza mbona Musiraeli Huyo lawi na shimeon walilaaniwa?? Yeye amesema wenye nguvu ya kulaani Israel ni MUNGU pekee ndio nikauliza je hapa Muisrael (LAWI) alipolaaniwa na baba yake ina maana waisraeli wanaweza kufanya kazi ya Mungu??

Hapo ndio sijamuelewa mkuu
 
Nimekusoma..... Pamoja sana mkuu
 
Duuh hii security sio ya kawaida
 
I smell ignorance he ni mfumo fair kuumba gumfumo gwa kunisumbua kwa maovu ya baba wakati kila MTU atahukumiwa kivyake
 
Hebu ni saidie kwa nini nnangangania hapo temple mount? Kama sehemu muhimu ya kihistoria?
Japo umerudisha swali ntakusaidia kidogo..

Kushushwa kwa Quran na Kuhusu Habari ya Msikiti wa Al Aqsa ambao upo Jerusalem ni vitu viwili tofauti kabisa..

Quran imepokelewa Saudia si Jerusalem..
 
NA KWANINI AWE KAANI PEKE YAKE ILIHALI HAM ANAWATOTO WANNE. KWA NADHARIA YAKO HII LAANA ILIBIDI IENDE KWA WATOTO WOTE WA 4. SIO KWA KAANANI PEKE YAKE
 
Lakini caanan hakufa kwenye gharika!
According to Quran mkuu Kanaan alifia kwenye gharika baada ya kukataa kuingia kwenye safina ya Nuhu na akaishia kwenda milimani soma Surat Hud nzima utakuta habari za mkasa huu ila kibiblia Kanaan yupo baada ya gharika ila kikubwa Quran inasema kanaan alikuwa mtoto wa Nuhu yaani mtoto wa mke wa Nuhu hivo inaweza tupa mwanga zaidi ya canaan alitokea wapi?? So huenda ni kweli alikuwa baba yake ni Ham na mama yake ni mke wa Nuhu!!!! Kwa assumption ya sura hii ya Quran
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…