Mkuu lawama na laani ni vitu tofauti sana. Waziri hawezi kuua mtu huko Iringa then Magufuli ndo akamatwe Mmmh!! hapana.
Haya maandiko ya Bible me yananivuruga sana Ukisoma Mwanzo 3:17 Mungu anailaani ardhi sababu ya Adamu sasa ardhi ilifanya kosa gani pale Eden?
Yoshua 7:24+ Akani alifanya dhambi ya kuiba aliteketezwa yeye na uko wake mzima hadi ng'ombe, punda, na vitu vyake vyote. sasa wao viumbe wengine walikosa nini wahusike kwenye adhabu ya Akani?
Sikumbuki ni kitabu gani but utanisaidia kama unakijua. kuna mtumishi mmoja wa Elisha Nabii alifanya kosa kumuomba zawani Naamani alieponywa ukoma na Elisha nabii. Huyo mtumishi alipatwa na ukoma yeye na ukoo mzima. sasa wao ndugu zake wengine walifanya kosa gani mpk wahusishwe kwenye adhabu ya huyo mtumishi?
Najiuliza Mungu yukoje? na anatumia kanuni, sheria, utaratibu gani kuadhibu watu vitu ambavyo hata havijahusika kuadhibiwa pasipo kosa?
Mkuu katika maisha yetu tupo katika mnyororo tunavutana yaani ni hivi watu walio na damu ya baba yako wote na mama yako nyote mu uzao wa damu moja kama baba yenu ambaye ni shina atatenda mabaya nanyi yakawafurahisha nanyi na vizazi vyenu mtahesabiwa katika dhambi ila kama mtajitenga na laana ya kizazi cha damu yenu mtakuwa mtakuwa mmekata cheni inayowazunguka mtahesabiwa haki
Soma hapa ili kujua cheni ya kuambatana inavyowavuta wote wasiotaka kugeuza nia zao na kuangamizwa
10 Eliya akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka, ukamteketeza, yeye na hamsini wake.
2 Wafalme 1 :10
11 Akatuma tena akida wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka upesi.
2 Wafalme 1 :11
12 Eliya akajibu, akamwambia, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza, yeye na hamsini wake.
2 Wafalme 1 :12
13 Tena akatuma akida wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule akida wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako.
2 Wafalme 1 :13
14 Tazama, moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawateketeza wale akida wa hamsini wawili wa kwanza pamoja na hamsini wao; laiti sasa roho yangu na iwe na thamani machoni pako.
2 Wafalme 1 :14
Jiulize kwanini hawa wote waliteketezwa kwa moto ni kwasababu walijifunga katika cheni ya maasi