Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

Kwanini Canaan alilaaniwa na sio Ham?!

1. Wana wa Israel wote walikuwa wameasi watatumikia miungu wengine

2. Hao waotumwa kwa Eliya inaonekana walikuwa na nia mbaya kwake ndo maana waliangamizwa

So, kiufupi ni kwamba woote walifanya kosa ndo maana wakaangamizwa na si mtu mmoja kafanya kosa wakaangamizwa wengine
Naomba upitie post #80 huenda tukaelewana
 
Mkuu hii ipo hivi mnyororo huu hapa chini

Baba-yako-na-kaka-yako-wewe-watoto-wa-kaka-yako-watoto-wa-kwako

Familia hii ina vinasaba vya baba yako kama baba yako ametenda maovu damu ya cheni hii yote inahusika hata vyombo vya ndani vina husika lakini kama ukiamua kujitoa katika hili utakuwa umejiweka huru karibu na Mungu wako
Lakini ukiendelea kuwepo katika hii cheni laana haikuachi
Kwa hiyo fahamu kabisa uovu wako utasababisha laana kwa kizazi chako chote
Mkuu soma kwanza kitabu cha Yoshua 7:1-26 ndo uje na majibu naona hujanielewa bado
 
1. Wana wa Israel wote walikuwa wameasi watatumikia miungu wengine

2. Hao waotumwa kwa Eliya inaonekana walikuwa na nia mbaya kwake ndo maana waliangamizwa

So, kiufupi ni kwamba woote walifanya kosa ndo maana wakaangamizwa na si mtu mmoja kafanya kosa wakaangamizwa wengine
Lakini huu ni mfano ingetokea kuna mmoja ameondoa mnyororo angepona lakini kwakuwa hawa walikuwa katika mnyororo mmoja ndio maana waliteketezwa.
 
Mkuu soma kwanza kitabu cha Yoshua 7:1-26 ndo uje na majibu naona hujanielewa bado
1 Lakini wana wa Israeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya Bwana ikawaka juu ya wana wa Israeli.
Yoshua 7 :1

2 Kisha Yoshua akatuma watu kutoka Yeriko mpaka mji wa Ai, ulio karibu na Bethaveni, upande wa mashariki wa Betheli, akawaambia, akisema, Pandeni juu mkaipeleleze nchi, basi wakapanda juu wakaupeleleza Ai.
Yoshua 7 :2

3 Wakarejea kwa Yoshua wakamwambia, Wasiende watu wote, ila waende watu kama elfu mbili, tatu, wakaupige Ai; usiwataabishe watu wote kwa kuwaendesha huko; maana watu hao ni wachache tu.
Yoshua 7 :3

4 Basi watu wakaenda huko wapata elfu tatu tu; nao wakakimbia mbele ya watu wa Ai.
Yoshua 7 :4

5 Watu wa Ai wakawapiga watu kama thelathini na sita; wakawafuatia kutoka mbele ya mlango mpaka Shebarimu, wakawapiga huko kwenye matelemko; mioyo ya watu ikayeyuka, ikawa kama maji.
Yoshua 7 :5

6 Yoshua akararua mavazi yake, akaanguka kifudifudi mbele ya sanduku la Bwana hata jioni, yeye na wazee wa Israeli; wakatia mavumbi vichwani mwao.
Yoshua 7 :6

7 Yoshua akasema, Ee Bwana MUNGU, kwa nini umewavusha watu hawa mto wa Yordani, ili kututia katika mikono ya Waamori, na kutuangamiza? Laiti tungelikuwa radhi kukaa ng'ambo ya Yordani
Yoshua 7 :7

8 Ee Bwana, niseme nini baada ya Israeli kuwapa visogo adui zao?
Yoshua 7 :8

9 Maana Wakanaani na wenyeji wote wa nchi hii watasikia habari hii, nao watatuzingira, na kulifuta jina letu katika nchi. Nawe utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?
Yoshua 7 :9

10 Bwana akamwambia Yoshua, Haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi?
Yoshua 7 :10

11 Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe.
Yoshua 7 :11

12 Ndiposa wana wa Israeli hawawezi kusimama mbele ya adui zao; wakawapa visogo adui zao, kwa sababu wamelaaniwa; mimi sitakuwa pamoja nanyi tena, msipokiharibu kitu kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.
Yoshua 7 :12

13 Haya! Inuka, uwatakase watu, ukaseme, Jitakaseni, mwe tayari kesho; maana Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi; Kitu kilichowekwa wakfu kiko katikati yako, Ee Israeli; huwezi kusimama mbele ya adui zako, hata mtakapokiondoa kile mlicho nacho kilichowekwa wakfu.
Yoshua 7 :13

14 Basi asubuhi mtaletwa karibu nami kabila kwa kabila; kisha itakuwa ya kwamba kabila ile atakayoitwaa Bwana itakaribia jamaa kwa jamaa; na jamaa ile atakayoitwaa Bwana itakaribia nyumba kwa nyumba; na nyumba ile atakayoitwaa Bwana itakaribia mtu kwa mtu.
Yoshua 7 :14

15 Tena itakuwa ya kwamba yeye atakayetwaliwa, naye anacho kitu kile kilichowekwa wakfu, atateketezwa kwa moto, yeye na vitu vyote alivyo navyo; kwa sababu amelivunja agano la Bwana, na kwa sababu ametenda upumbavu katika Israeli.
Yoshua 7 :15

16 Basi Yoshua akaondoka asubuhi na mapema, akawasogeza Israeli kabila kwa kabila; kabila ya Yuda ikatwaliwa.
Yoshua 7 :16

17 Akazisogeza jamaa za Yuda, akaitwaa jamaa ya Wazera; akaisogeza jamaa ya Wazera mtu kwa mtu; Zabdi akatwaliwa.
Yoshua 7 :17

18 Akawasogeza watu wa nyumba yake mmoja mmoja; na Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila ya Yuda akatwaliwa.
Yoshua 7 :18

19 Yoshua akamwambia Akani, Mwanangu, nakusihi, umtukuze Bwana, Mungu wa Israeli, ukaungame kwake; uniambie sasa ulilolitenda; usinifiche.
Yoshua 7 :19

20 Akani akamjibu Yoshua, akasema, Kweli nimefanya dhambi juu ya Bwana, Mungu wa Israeli, nami nimefanya mambo haya na haya.
Yoshua 7 :20

21 Nilipoona katika nyara joho nzuri ya Babeli, na shekeli mia mbili za fedha, na kabari ya dhahabu, uzani wake shekeli hamsini, basi nalivitamani nikavitwaa; tazama, vimefichwa mchangani katikati ya hema yangu, na ile fedha chini yake.
Yoshua 7 :21

22 Basi Yoshua akatuma wajumbe wakapiga mbio mpaka hemani; na tazama, vile vitu vilikuwa vimefichwa hemani mwake, na ile fedha chini yake.
Yoshua 7 :22

23 Wakavitoa kutoka hapo katikati ya hema, wakavileta kwa Yoshua, na kwa wana wa Israeli wote, nao wakaviweka chini mbele za Bwana.
Yoshua 7 :23

24 Kisha Yoshua, na Israeli wote pamoja naye, wakamtwaa Akani, mwana wa Zera, na ile fedha, na Lile joho, na ile kabari ya dhahabu, na wanawe, na binti zake, na ng'ombe zake, na punda zake, na kondoo zake, na hema yake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, wakavileta juu hata bonde la Akori.
Yoshua 7 :24

25 Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? Bwana atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe.
Yoshua 7 :25

26 Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa ya mawe hata leo; naye Bwana akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata hivi leo.
Yoshua 7 :26
 
Mkuu soma kwanza kitabu cha Yoshua 7:1-26 ndo uje na majibu naona hujanielewa bado
19 Yoshua akamwambia Akani, Mwanangu, nakusihi, umtukuze Bwana, Mungu wa Israeli, ukaungame kwake; uniambie sasa ulilolitenda; usinifiche.
Yoshua 7 :19

20 Akani akamjibu Yoshua, akasema, Kweli nimefanya dhambi juu ya Bwana, Mungu wa Israeli, nami nimefanya mambo haya na haya.
Yoshua 7 :20

Hapa kama akan angejitakasa (kutubu) mapema haya yasingemkuta
 
Swali moja nikuulize. Kwa mfano ingetokea mtoto mmoja wa Akani akaungama saa ile je wangemuacha wasimuangamize?
 
Mkuu hii ipo hivi mnyororo huu hapa chini

Baba-yako-na-kaka-yako-wewe-watoto-wa-kaka-yako-watoto-wa-kwako

Familia hii ina vinasaba vya baba yako kama baba yako ametenda maovu damu ya cheni hii yote inahusika hata vyombo vya ndani vina husika lakini kama ukiamua kujitoa katika hili utakuwa umejiweka huru karibu na Mungu wako
Lakini ukiendelea kuwepo katika hii cheni laana haikuachi
Kwa hiyo fahamu kabisa uovu wako utasababisha laana kwa kizazi chako chote
Kwann mzigo wa baba abebeshwe mtoto? wacha mtoto ajibebee mzigo wake
 
Yani mtu alifanya kosa adhabu yake ni kunyongwa sasa eti unakusanywa ukoo wake wote, mifugo yake yote, vyombo vya ndani vyote, vinachomwa moto hadi nyumba? hii si haki, na si sawa
 
Swali moja nikuulize. Kwa mfano ingetokea mtoto mmoja wa Akani akaungama saa ile je wangemuacha wasimuangamize?
Asingeachwa na wanadamu lakini kwa Mungu angehesabika haki

39 Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi.
Luka 23 :39

40 Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo?
Luka 23 :40

41 Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa.
Luka 23 :41

42 Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.
Luka 23 :42

43 Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi.
Luka 23 :43

Hapa nadhani umeelewa
 
Ufafanuzi kidogo awa walihukumiwa kiserikali sasa uhusiano wao upo wap?
 
Hapa ndio kwenye utata sasa mbuzi anakuaje na unasaba na mtu?
Unasaba wa mbuzi na mwanadamu unakuja katika kumiliki hivi masoud sufuria ikipika nyama ya nguruwe si unaitupa?
Si najisi tayali hapo kwanini baada ya kutoa nyama tuone kuwa unajisi umetoka?

Sufuria na nyama zina husiana vipi?

Ukijiuliza vema ukapata majibu utakuwa umemaliza mjadala
 
Mtoto ambaye ni damu Masoud mdhahara:. akitaka kujiepusha ktk laana ya baba yake masoud haina budi afuate yaliyo mapenzi mema ya Mungu ili apone katika hili
Sawa kwann fursa hii ya kutenda mema wengine awapewi mfano uzao wa kwanza wa misri kipindi cha mussa waliteketezwa kwa ukaidi wa pharao
 
Unasaba wa mbuzi na mwanadamu unakuja katika kumiliki hivi masoud sufuria ikipika nyama ya nguruwe si unaitupa?
Si najisi tayali hapo kwanini baada ya kutoa nyama tuone kuwa unajisi umetoka?

Sufuria na nyama zina husiana vipi?

Ukijiuliza vema ukapata majibu utakuwa umemaliza mjadala
Unatupa sufuria kisa nyama ya nguruwe huyo atakuwa punguani hakuna unasaba wa binadamu na mnyama wala vitu binadamu kila mmoja ahukumiwe kwa matendo yake
 
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Mkamate Sana Elimu Usimwache Aende Zake Maana Ni Uzima Wako.
 
Back
Top Bottom