Kwanini CHADEMA hawataki tuwahoji kuhusu utendaji wa wabunge na madiwani wao?

Kwanini CHADEMA hawataki tuwahoji kuhusu utendaji wa wabunge na madiwani wao?

Wamechemka. Ingawaje si kazi ya msingi ya wabunge kusaidia miundombinu lakini wanaweza. Kama wanaweza kujaza watu kwenye mikutano na wanaweza wanaomba kuchangiwa kutoka jela au kufanya kampeni na kuchangiwa mamilioni wanaweza pia kuleta maendeleo kwenye jamii.

Tufike wakati tuache hizi siasa za kuwa na malaika mmoja anayeamua huku kufanyike nini kwingine kusifanyike. Tuko wengi sana kuweka hatma zetu kwa mtu mmoja ni upuuzi.
 
ni muda wa hukumu kwa wale wabunge wa chadema waliopewa fursa
 
Kazi ya msimsingi ya wabunge ni ipi?

Kwanini tusiwahoji wabunge wote?Kwanini useme upinzani pekee?Nakumbuka kilianzishwa kipindi fulani na Tiddo Mhando kiliitwa mchakato majimboni!Kilichofuata ni Mhando kufurumushwa TBC kwani kipindi hicho kilionekana mwiba kwa CCM kwani wananchi walifunguka kweli kweli!
Ungeshauri kipindi hicho kirejeshwe ili kufanya tathimini ya huo utendaji kwa wabunge wote!
 
Mkuu unahiji vipi wabunge na madiwani wa upinzani wakati wako chini ya mkurugenzi anayetekeleza ilani ya uchaguzi wa CCM?

Unamhoji vipi mbunge au diwani wa upinzani huku mwenyekiti wa CCM akitumia ushindi wa upinzani kama adhabu kwa kuwanyima maendeleo?? (Rejea hotuba ya JPM Bunda).

Unahoji vipi diwani au mbunge ambaye katika baraza la madiwani wako chini ya akidi ya ushindi?? Yaani wawe wanne katika ishirini katika mfumo wa kufanya maamuzi kwa kura??

Mleta mada ukiambiwa mpumbavu utasema umetukanwa lakini ni kisifa tu cha uwezo wako kiakili. Sio tusi!!
 
ni muda wa hukumu kwa wale wabunge wa chadema waliopewa fursa
Mkuu barabara nyingi za Kigoma mjini zimepigwa lami,Zao lamichikichi limefufuliwa, ushuru hakmashauri ilikuwa imepandisha, lkn wakashusha ,maendeleo mengi yamefanyika ndani ya hii miaka mitano chini ya ubunge wa Zitto , nani apongezwe kati ya Zitto na Serikali?.
 
Ukitaka kuoga matusi humu jamvini waulize wanachadema wakwambie ni nini wabunge na madiwani wao walikifanya baada ya kupewa dhamana mwaka 2015?

Kuna hoja ya kusema eti hawakuwa na dola lakini ukweli ni kuwa zipo halmashauri nyingi zilikuwa chini ya Chadema na hawakuja na lolote.
Halmashauri zote zilinyang'anywa vyanzo vya mapato, na mwenye mamkaka na fungi la halmashauri ni mkurugenzi, ambaye ni mteule wa mwwnyekiti wa CCM, tafakari!
 
Ukitaka kuoga matusi humu jamvini waulize wanachadema wakwambie ni nini wabunge na madiwani wao walikifanya baada ya kupewa dhamana mwaka 2015?

Kuna hoja ya kusema eti hawakuwa na dola lakini ukweli ni kuwa zipo halmashauri nyingi zilikuwa chini ya Chadema na hawakuja na lolote.
Hawana majibu.
 
Hapa utaambiwa tu kuwa sio kazi ya mbunge kuleta maendeleo,huo ndio utetezi ila hutoelezwa mafanikio ya hao wabunge katika hizo kazi za msingi za mbunge.
 
sisi hapa sombetini hakuna kilichofanywa juzi juzul tu ndio tumepata Lami katika hii awamu ya kazi tu
 
Back
Top Bottom