second9
JF-Expert Member
- Jun 22, 2016
- 216
- 451
Hii mifano aliweza sana kuitumia Dr Slaa kipindi chake cha Kampeni, na ilileta matokeo flani chanya.Hizo takwimu watasikiliza na kuelewa wachache.
Ukitaka mtanzania asikuelewa tumia namba katika kueleza mambo.
Ningekuwa mwanasiasa nataka kuwaeleza jambo watanzania mfano upigaji labda wa bilioni 8.
Ningetumua mifano inayoendana na nlipo. Kama wana shida ya maji ningesema wamepiga bilioni nane fedha ambayo ingeweza kujenga visima vya maji 100 mkaondokana na tatizo la maji.
Kama shuda ni barabara ningesema fedha ambayo ingeweza kujenga barabra ya lami toka kijiji fulani hadi fulani.
Kwanza takwimu ni watanzania wachache ambao huwa wanaziverify ndiyo maana january makamba aliwahi soma report yenye kutofautina na takwimu halisi.