Kwanini CHADEMA mmetunga na mnasambaza uzushi wa ukabila wa Hayati Magufuli?

Naona umemaliza na siasa ambazo huzipendi!.

Nilidhani tatizo ni CHADEMA kushindwa kuleta data ambalo hata mimi nakubaliana nalo.

NB
Hili ni tatizo la taasisi nyingi sana za umma na binafsi hawafanyi research kabisa wanakuja na vitu vya kubumba.

HITIMISHO LAKO
Nawe ukadondokea pale pale walipodondokea CHADEMA ukaja na kauli za jumla jumla.
 
Aaaah mkuu leo mmesahau Lowassa alisema nini kule Tabora? Tena Kaingiza Udini mbaya sana dhidi ya Katoliki! akavuta na Masheikh na kuzunguka nao mikoani. Kilichowasaidia Chadema ni EL kuja na Wagombea wazuri wanaoweza kushinda majimboni lakini walishindwa kuelewa kwamba Kiti Cha Urais hakitokani na Wabunge!

CCM wao toka mwanzo wakaweka nguvu zaidi ya kushinda Urais wakijua Ubunge wana wawakilishi.kila jimbo nchini lazima watapata hata nusu na ndio maana wakampeleleka EL Chadema kuwavuruga akili wasione Tunu ya Dr. Slaa ambaye 2010, JK mwenyewe Chupuchupu ..

Kampeni za Magufuli alisema wazi yeye sii Mwanasiasa, Maendeleo hayana Chama, hayana Kabila wala dini.
 

..Ni kweli Lowassa alikwenda Kanisani / Lutheran na kutoa kauli za kidini kuvutia upande wake.

..Lakini hutakuwa mkweli kama utabisha kwamba wapiga debe wa CCM walikuwa wakipanda majukwaani na kuwaambia wananchi waziwazi kwamba wasichague mgombea toka " kaskazini. "

..Ni bahati mbaya kwamba kampeni za namna hiyo hazikukemewa na Magufuli, kama mgombea, au kiongozi yeyote mkubwa ndani ya CCM.

..Kwasababu kampeni zilikuwa chafu na za kikabila ilitakiwa kufanyike juhudi za dhati kuponya MAKOVU baada ya uchaguzi.

..Ni bahati mbaya kwamba hali imeachwa kama ilivyo tangu kampeni za 2015 na matokeo yake umoja na mshikamano wa Watanzania uko mashakani.
 
Alikuwa analionesha wazi wazi hilo na kila mtu alikuwa anajionea mwenyewe so acha upumbavu wa kutetea ujinga.
 
Uchaguzi upi unazungumzia? Labda rusha clip moja nikumbushe maana sijawahi kusikia hili neno - Mgombea kutoka Kaskazini..

Yaani kweli uwaaambie wananchi wasimchague Sugu, Msigwa, Prof Jay, Mnyika, Lissu, Zitto, Maalim Seif? Na kwa Uaskazini upi mkuu mbona mnapotosha hivi?
2015 Vyama vya Upinzani viliunda Umoja wao wa UKAWA sii Bara tu mpaka CUF na Znz waliingizwa! Huyo mgombea wa Kaskazini nani? Mbowe? Ukisema EL aliitwa fisadi papa na kina Nape, hilo kweli na ndio ushindi wa CCM ulipotokea..
 
Akili zako naona umezisahu kwenye msiba chatou
 
Kwa takwimu Watu wa Kanda ya ziwa ndio wanatoa mstakabali wa urais nchi hii kwa sababu ya wingi.

Acha hawa mataahira waruke ruke mwaka 2025 wakaangwe wakimbilie kusema wameibiwa kura, maana ndio sababu zao.
Ila wanaoneza hili swala ni CCM wakiongozwa na January Makamba
 

..Nazungumzia Uchaguzi wa 2015 kwamba Chadema kilipigwa vita kama chama cha Wachaga au chama cha watu wa " kaskazini "?

..Je, wewe hujawahi kusikia tuhuma kwamba Chadema ni chama cha Wachaga, au cha watu wa " kaskazini. "

..Hukuwahi kusikia matamko kwako watu wa " kaskazini " hawafai kupewa uongozi wa nchi hii?

..Hili CCM walikuwa wanalisema waziwazi kwa mfano Ridhiwani Kikwete amewahi kunukuliwa akitoa matamshi hayo.

..Pia Mohamed Seif Khatib aliyepata kushika nyadhifa kubwa serikalini na ktk CCM aliwahi kuandika makala akiwananga wagombea Uraisi wenye asili ya mikoa ya " kaskazini. "
 
Daaah hizo tuhuma za Chadema ni Chama cha Wachagga toka 2000 mkuu hata kabla kabisa sisi wengine hatujajiunga 2003. Hata mimi nilikiona cha Wachagga kqani ilikuwa Uongo? maanake Enzi zile makao makuu, kambi rasmi ya Chama na Strong hold ilikuwa Kaskazini. Na Chadema ilipigania zaidi Sera ya Serikali ya MAJIMBO! Ukiona mtu anataka utengano, ujue kajitazama yeye nafasi yake kwanza!

Kwa hiyo Lawama na kelele za watu ndio zilikifanya Chama kibadirike by 2003 nakumbuka tena kupitia hapa Hapa JF Kitila alituvuta sisi wengine Kuingia Chadema. Na ajabu basi watu wote walopigania Chadema kiwe Chama cha Kitaifa wamepigwa vita woote na kuondolewa..Slowly now vita ipo kwa kina Halima Mdee yaani Chadema nadhani kuna mzimu mbaya sana, maanake wanashindwa hata kuona vita baridi ya CCM kweli?.
 

..Kauli za kibaguzi dhidi ya Wachaga zilianza kidogo kidogo kama ulivyoeleza mpaka zikaota mizizi na kufika ktk majukwaa ya kampeni za uchaguzi mkuu wa 2015.

..Sasa hivi kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya hawa ndugu zetu imekuwa ni jambo la kawaida na lisilokemewa.

..Chadema iliwahi kuwa na Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, na Mwenyekiti Umoja wa vijana, wote walikuwa Wasukuma. Je, uliwahi kusikia wameitwa chama cha Wasukuma?

..Unadhani waandamizi wote hao wangekuwa wanatoka Kaskazini au ni Wachaga kelele na shutuma dhidi yao zingekuwa kiasi gani?

NB.

..Hata jina Chadema nimewahi kusikia lilitokana na pendekezo la mmoja wa waasisi ambaye ana asili ya kanda ya ziwa / shinyanga.
 
Mkuu zamani watu walikuwa hawana Mwamko wa kimfumo kuhusiana na Uongozi wa Vyama vya Siasa. Hili lazima tulikubali kwa maana ya kwamba Kabla ya Uhuru Vyama vya Siasa viliwakilisha Makabila au maeneo fulani. Na hata tuliporudi na Vyama vingi 1993 tulikuja na mfumo huo huo kutazama Maslahi ya JIMBO ama Maeneo. Hivyo, Mbowe alipochukua Uongozi watu wengi walichukulia kama Mapinduzi ka hijack Chama! Wagombea wengi walianza nao kutoka Kaskazini kuliko mikoa na majimbo mengineyo!

Vile vile CUF kina Maalim Seif kupigania Znz.. CCM pekee ndio kilionekana Chama chenye ofisi zake Tz nzima. Zitto alipoanza na ACT bila kujijua akaweka nguvu kubwa Kigoma...Leo ACT nguvu kubwa ipo Zanzibar Why? Usiniulize mimi..
 
UPUMBAVU MTUPU!
Kuna wakati enzi za Nyerere,kulikuwa na tetesi kwamba NBC chini ya Nsekela ilikuwa imeajiri Wanyakyusa wengi, habari zikamfikia Nyerere , kama ilivyokawaida Nyerere akamwita Nsekela ajieleze juu ya hizi habari za Wanyakyusa kupendelewa na kuwa wengi kwenye hiyo benki, uzuri wa Wanyakyusa narudia tena uzuri wa Wanyukyusa hasa wale wa miaka ile walikuwa hawaogopi,tofauti na wengi marehemu Mzee Nsekela alikuwa hamuogopi Nyerere, alipoulizwa nae akajibu hivi mwalimu kule JWTZ wamejaa watu kutoka Mara je nawe unawapendelea? mwalimu hakuwa na jibu akamwambia aendelee kuchapa kazi,hivyo ndivyo walivyo wapinzani wa mwendazake walikuwa wako mbele kusema anapendelea Wasukuma, na tujiulize Mbowe anapendelea Wachaga? jibu unalo mwenyewe.
 
Sio kanda ya ziwa ndio ilimaliza,tazama mikoa ya kusini na kaskazini kwa kura za urais,watu walichoka na brabra za siasa,walikuwa wanataka kiongozi wa VITENDO,
 
Wako 20, katika kabila lenye 15% ya Watanzania. Ukitaka majina nitakupa, lakini wewe eleza jinsi hili lilivyo na ukabila.
Sio asilimia 15 tu,wasukuma mpk sasa wako milioni 21 kwa watu milioni 60,utawakwepaje hao kina ngosha?
 


Msome mwenyewe mbaguzi kwa maneno yake mwenyewe
 
Hivi hii kesi huyu mtu anaendelea nayo? Nashauri akomae nayo ili Samia atawale milele

 
Uchafu wa mhutu yule si wakutafuta.... Hata mtoto mdogo anajua bahana jamaa lilitugawa sn watz kwa ukabila na ukanda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…