Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Mkuu hili ni tatizo , matokeo yake yameanza kuonekana sasa. Huu umoja wa ''CCM'' uta ambukiza nchi nzima..ili ubaguzi uwe systemic inabidi kwanza ulelewe kidogo kidogo kama inavyotokea sasa hivi.
..udini na ukabila tunavyoulea sasa hivi huko mbele ya safari utakuja kuwa tatizo kubwa kwa nchi yetu
Wakati wa Nyerere na waliotangulia ilikuwa ni vigumu kuona ukabila kama mfumo
Mkuu Mkandara aelewe kuwa ili ukabila uwe 'systemic' lazima ujengewe mazingira, upaliliwe na ukue.
Hapa ndipo Mwendazake alipolitia Taifa katika tatizo. Amejenga mazingira ya ukabila na sasa yanashamiri
Kiongozi wa nchi anaposimama na kusema '' watu wa eneo fulani watusubiri' tayari anajenga ukabila mioyoni mwa wasioelewa. Halafu anaporudi ofisini na kuteua kwa mfano ule ule anashadidia ukabila.