Kwanini CHADEMA tu inakomaliwa kuandaa uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa?

Ok sawa tusubiri tuone wataamuaje wenyewe kwenye uchaguzi yasije kuwa ya ccm, watu walimchoka kikwete akaja Magufuli wanalia na hawamtaki sasa wanamtaka kikwete.

Tatizo hatufahamu nani ni nani moaja apewe nafasi ya kuongoza.

Kuna msemo wakiswahili " ukitaka kujua tabia ya masikini subiri apate pesa" hili naliona kwetu waafrika, huwawazuri kabla ya kupata vyeo. Tukivipata ndio tunaeleweka kwa wenzetu.

Binafsi naona Mbowe kaiongoza taasisi hiyo vizuri. Wakimchagua mwingine pia ni sawa ndiyo inapaswa iwe hivyo yaani tuaminiane na tuachiane uongozi kila baada ya muda fulani.

Sipingi kwamba asichaguliwe mwingine, ila pia sintokuwa na tatizo kama wanamchagua yeye kuendelea kuiongoza CHADEMA.

Niwatakie uchaguzi mwana CHADEMA.
 

Hapa nimeona una hoja za msingi kwamba ngoja tuone wataamua kumchagua nani. Mimi binafsi sina tatizo na uwezo wa Mbowe na hasa hapa alipoifikisha cdm, bali kwangu suala la wakati ukuta limegoma kuondoka kichwani. Ila kwakuwa mimi sio sehemu ya wanaochagua mwenyekiti, ngoja ninywe tu mtori nyama nitazikuta chini.
 
Kumbe ulikua hujui, CHADEMA ni chama kikuu cha upinzani.

Kumbe hujui kwamba mwl l. Anapokua anakusimamisha sana darasani kujibu maswali ni ishara kwamba anaona kitu flani ndani yako na anataka kukihuisha.

Huu ni msimu wenu kipindi tunapigizana kelele na TLP na Mzee wa Kiraracha ulikua bado mtoto eeh. Wakati tukimsulubu Prof. Lipumba na Mwalimu Seif ulikua bado unasoma shule ya msingi eeh.

Tupiamo hata ka-like kama umenisoma mzee baba.
 


Ohh nimekusoma mkuu..bas kazi Africa ipo
 
Jembe ulaya lile....rejea maongezi yetu siku ile!!
CCM hata ukiwaambia ni Magufuli pekee anaweza kukubaliwa kupewa uenyekiti Chadema, wanaweza kumshawishi aache Urais ajiunge Chadema awe mwenyekiti ili aiue Chadema!
 
Chadema ndo chama pekee kinachojitabainisha kama chama cha Demokrasia...lazima wawe mfano wa demokrasia safi
 
Sio kukomaliwa, ni vema hii dhana ya Demokrasia ikaimalishwa zaidi huko kwenye vyama vyote vya siasa hii itasaidia kuifikisha maeneo mengi kirahisi hatimae kusambaa kwa wananchi wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…