Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
China imejizolea umaarufu Kama Taifa lenye mahusiano makubwa na mazuri na Tanzania. Limeonekana kuwa moja ya Taifa lenye nia nzuri na Tanzania kiasi kwamba Rais wake alipewa fursa ya mazungumzo ya lisaa limoja na Rais Wetu.
Ila Taifa la China lilipewa kujenga bandari ya Bagamoyo baadaye ikabainika tuliingizwa chaka. Tukavunja mkataba.
China ilipewa miradi nyeti Zambia ikafadhili ila ikafikia kiwango Cha kudai na kushindikana kulipwa hivyo inaendesha baadhi ya maeneo nyeti ya Zambia kwa lengo la kufidia mikopo
Kenya waliwapa tenda ya reli na Sasa gharama za mradi hazikidhi matakwa ya rejesho Jambo linalopelekea deni kutokulipwa kwa kiwango kilichokubaliwa.
China wanapokuja kwenye miradi hii yamkakati naangalia nchi ya Misri kwenye Umeme na naangalia nafasi ya Yapi Markez kwenye reli, je haya makampuni yaliingia mkataba wa aina gani hapo awali ili mkataba huo usiathiriwe na mbia mpya ambaye ni china.
Lakini pia naangali namna gesi ilipouzwa kwenye awamu ya pili ya Jk nalinganisha na ubia huu wa mchina awamu ya pili, je hatuoni kama tunaweza ingia ubia wenye tija ila ukakosa tija pale kiongozi anayefuata awamu ya Tano atakapokuja kukinzana na utawala uliopo Sasa? Tukumbuke gesi iliuzwa bungeni kwa vikao vilivyokaa Hadi usiku lakini baada ya Mzalendo Magufuli kuingia aliamua kutoendelea na Sheria na mikataba iliyosainiwa awali kwa kufrastrate mikakati ya awali ya gesi ya Mtwara
Hofu yangu kubwa na ambayo ningeomba wataalam watusaidie kuingamua ni hii ya awamu iliyipo madarakani kuingia mikataba mikubwa ya rasilimali zetu kipindi Cha mwisho then awamu mpya inapoingia inakataa kutekeleza makubaliano ya mtangulizi wake na mwisho kuifanya Tanzania ionekane Kama haisimamii Sheria na mikataba inayoingia. Tunaposhtakiwa tunaishia kutumia mabilioni ya fedha za wananchi kulipa madeni na madai ambayo yangeweza kuepukika.
Tuilinde nchini kutoka kwenye mikataba mikubwa isiyo na ulinzi na uwazi kwa wananchi.