Kwanini Chips za Vibandani ni tamu kuliko zile tunazopika nyumbani?

Kwanini Chips za Vibandani ni tamu kuliko zile tunazopika nyumbani?

Nauliza tu maana nimetoka kula Chips za home lakini ukilinganisha na zile ambazo zinakuja kwenye foil na mitaani zinakuwaga tamu balaa na hata mpishi mwenyewe aliyepika anasema kabisa zile za mtaani zinakuwa bomba sana

Nimekula Chips za Nyumbani na nimekula Chips za vibandani lakini mara nyingi hizi za vibandani zinakuwa tamu zaidi kuliko zile ambazo zinapikwa nyumbani. Hii ni kwangu tu na wengine pia ni hivi hivi?

Viungo ni vile vile lakini na viazi vinakuwa vilevile nini zinafanya hizi za mtaani zinakuwa tamu zaidi?

Mnauziwa chips zilizopikwa na mafuta ya transformer ndio maana mnaona ni tamuuuuu
 
Nyumbani wengi hawaweki udambwi
Mimi chips nazopika naenjoy naweka pilipili sauce, mayonnaise, kachumbari namwagia na redgold tomato utamu wake mpaka kichogoni.
Hivyo vinanulika kabisa , hapa kitaa kuna kibanda mara nyingi ninaenda kuwachukulia madogo chips , huyo jamaa anauza sana chips. Chips zake akishaosha viazi mara mara mbili , ile tatu vile viazi anaweka kwenye ndoo ya maji ila kuna vitu anaweka kule , yaani kama unaona viazi vinakuwa na rangi ya njano fulani then anaweka kwenye karai moja moja .

Chips zake ni tamu kinoma , mida ya saa nane mchana anamsha mpaka sita usiku bado anapewa order.​
 
Anaweka manjano
 
🤣🤣🤣🤣🤣 lbda mpishi wa nyumbani huna ujuzi kama wa mpishi wa vibamdani
 
Back
Top Bottom