SSD (Solid State Drive) ni teknolojia mpya ya uhifadhi wa data iliyokuja baada ya HDD (Hard Disk Drive). Inaleta faida kadhaa kama vile kasi kubwa, ukisearch kitu unakipata haraka, na kutokuwepo kwa sehemu zinazotembea ama kuzunguka kama ilivyo kwenye HHD, hivyo inapunguza uwezekano wa kuharibika.
Hata hivyo, sababu moja inayoweza kusababisha kompyuta zinazotumia SSD kuwa na ukubwa mdogo (storage space) ni gharama. Katika soko, gharama za SSD bado ni ghali zaidi kwa kila GB ukilinganisha na HDD. Hivyo, ili kupunguza gharama ya kompyuta na kuifanya kuwa na bei nafuu, wazalishaji wanaweza kuweka SSD yenye ukubwa mdogo wa nafasi ya uhifadhi.
Ingawa SSD ina faida nyingi, ukubwa wa uhifadhi bado ni changamoto hasa kwa watumiaji wanaohitaji kuhifadhi vitu vingi, kama vile video, picha, na program kubwa. Katika hali hii, watumiaji wanaweza kuchagua kompyuta inayotumia SSD kama sehemu ya kasi na utendaji, na kutumia external hard drive kwa kuhifadhi vitu vingine.