baba-mwajuma
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 4,178
- 7,591
Boss Congo walicho ki experience ni tofauti kabisa na wa Africa wengine haya sio mambo ya kuangalia juu juuNdio nasema issue sio wazungu issue ni mtambuka. Hata leo DRC isiwe na vita unadhani Viongozi wake watatoa mikataba mizuri ya rasilimali?
1. Cobalt zilianza kuchimbwa toka enzi za ukoloni na Wacongo hawaja Experience ukoloni wa Muingereza na Ufaransa bali ukoloni wa kikatili, Wacongo waliwekwa hadi Museum, Ubelgiji hajaendeleza chochote pale bali walikua busy kuchota Madini, ndio maana hawana miundombinu, baina ya mkoa na mkoa hakuna barabara etc
2. Tukija kwenye hio miundombinu kuna vikundi ambavyo vina hakikisha miundombinu haijengwi Congo, Ndege ziwe ndio njia ya Transport, Reli zikijengwa zinavunjwa, Treni zinatekwa etc. Mobutu Single handed ameharibu miundombinu karibia yote.
3. Uwepo wa waasi ambao wana misaada kama yote, kuna waasi wana kila silaha huko, sasa hivi hadi Isis wameingia Congo kama kawaida yao kila kwenye Interest za Usa wapo.
4. Congo ni kubwa mno, zaidi ya mara 2 ya Tanzania na ina misitu ni ngumu sana kutengeneza Authority kila sehemu hasa vile hakuna Miundombinu na Uwepo wa waasi.
Anachofanya China sasa hivi Congo ndio exactly wanachohitaji Wacongo, ujenzi wa miundombinu kuconect nchi nzima, itasaidia logistic na kufikia Nchi nzima na hata kupambana na waasi.