Kwanini Congo DRC?

Kwanini Congo DRC?

Ndio nasema issue sio wazungu issue ni mtambuka. Hata leo DRC isiwe na vita unadhani Viongozi wake watatoa mikataba mizuri ya rasilimali?
Boss Congo walicho ki experience ni tofauti kabisa na wa Africa wengine haya sio mambo ya kuangalia juu juu

1. Cobalt zilianza kuchimbwa toka enzi za ukoloni na Wacongo hawaja Experience ukoloni wa Muingereza na Ufaransa bali ukoloni wa kikatili, Wacongo waliwekwa hadi Museum, Ubelgiji hajaendeleza chochote pale bali walikua busy kuchota Madini, ndio maana hawana miundombinu, baina ya mkoa na mkoa hakuna barabara etc

2. Tukija kwenye hio miundombinu kuna vikundi ambavyo vina hakikisha miundombinu haijengwi Congo, Ndege ziwe ndio njia ya Transport, Reli zikijengwa zinavunjwa, Treni zinatekwa etc. Mobutu Single handed ameharibu miundombinu karibia yote.

3. Uwepo wa waasi ambao wana misaada kama yote, kuna waasi wana kila silaha huko, sasa hivi hadi Isis wameingia Congo kama kawaida yao kila kwenye Interest za Usa wapo.

4. Congo ni kubwa mno, zaidi ya mara 2 ya Tanzania na ina misitu ni ngumu sana kutengeneza Authority kila sehemu hasa vile hakuna Miundombinu na Uwepo wa waasi.

Anachofanya China sasa hivi Congo ndio exactly wanachohitaji Wacongo, ujenzi wa miundombinu kuconect nchi nzima, itasaidia logistic na kufikia Nchi nzima na hata kupambana na waasi.
 
Ni kweli mkuu, ina rasilimali nyingi sana. Lakini, kwani ni Congo DRC pekee ndiyo yenye utajiri wa rasilimali? Mbona nchi zingine tajiri kama Congo DRC hazina machafuko?
rudia kusoma kisha edit swali lako mkuu,ndo nitakujibu vizuri mkuu.
 
Sababu wana Mali, leo hii Congo ikifungwa hakuingii hakutoki Kitu nchi nyingi za west zitakua katika hali ngumu sana.

Congo ndio wana run Dunia kwenye mambo mengi sana na Madini yao ni crucial kwenye Technology za sasa. Mabwana wakubwa hawataki wajitawale na kujielewa ili mambo yao yaende.
..DRC ni shamba la bibi, ni mkakati wa mabeberu
 
Sasa angalia na value per square meter, hiyo DRC ni mara 5 ya Tanzania ila kwa size yetu bado we are good than most nations huku Africa.
Wanaoiba hawaangalii hicho, huu sio ushindani wa Tanzania na Congo ila ni maelezo ya kwa nini Congo haina Amani na ina misuko suko wakati wote.

Pia kama nilivyoelezea comments nyengine Madini ya Congo wao ni Monopoly, kuwa na 70% share ya Madini ambayo ni sababu ya Leo Tuna Apple, Microsoft, Nvidia, GOOGLE na wengine si jambo la kitoto. Gesi wanaweza wasichukue ya Tanzania wakaenda Qatar, Urusi, Algeria etc hakuna Nchi yenye Monopoly ya Gesi,
 
Nchi nyingi zina mali lakini zina utulivu, why DRC? Shida ni uongozi na hulka ya Wacongo wenyewe.
kusema nchi nyingi ni tajiri na zina utulivu pasipo kuzitaja hizo nchi unamaanisha nini mkuu?
 
Hiyo Cobalt ipo Congo,Russia,Indonesia,Australia,Cuba
At what percent? Hii ni production ya Cobalt 2023

Screenshot_20250111-144300_Pixel Launcher.png

We Unaona ni sawa kuzitaja hizo nchi compare na Congo?
 
Wanaoiba hawaangalii hicho, huu sio ushindani wa Tanzania na Congo ila ni maelezo ya kwa nini Congo haina Amani na ina misuko suko wakati wote.

Pia kama nilivyoelezea comments nyengine Madini ya Congo wao ni Monopoly, kuwa na 70% share ya Madini ambayo ni sababu ya Leo Tuna Apple, Microsoft, Nvidia, GOOGLE na wengine si jambo la kitoto. Gesi wanaweza wasichukue ya Tanzania wakaenda Qatar, Urusi, Algeria etc hakuna Nchi yenye Monopoly ya Gesi,
Hauna Apple, Microsoft, Dell na Google n.k kwa sababu ya madini ya Congo, unavyo hivi kwa sababu ya vichwa vya kina Steve Jobs, Bill Gates, Michael Dell, Sergey Brin, Larry Page n.k Hata bila ya madini ya Congo hivi vitu vingekuwepo.
 
Kuna nchi zilishawahi kuingia katika misukosuko ya kisiasa lakini hatimaye zilikuja kutukia. Rwanda ni mojawapo.

Kwanini imekuwa tofauti nchini Congo DRC?

1. Tatizo ni uongozi? Angepatikana huko kiongozi kama NYERERE, au KAGAME au MAGUFULI angeweza kuituliza?

2. Wasababisha machafuko ya Congo DRC wana nguvu kuliko wazuiaji?

3. Hulka ya raia wa Congo DRC inachangia?
Kikubwa zaidi ni vikwazo vya kununua silaha za kisasa vilivyowekewa serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa ili kuilazimisha serikali kufanya mazungumzo na waasi.

Endapo vikwazo vitaondolewa na serikali ikaruhusiwa kununua zana za kisasa za kijeshi ni wazi waasi wangekuwa wamefurushwa!
 
Hauna Apple, Microsoft, Dell na Google n.k kwa sababu ya madini ya Congo, unavyo hivyo kwa sababu ya vichwa vya kina Steve Jobs, Bill Gates, Michael Dell, Sergey Brin, Larry Page n.k
Idea zao haziwezi kuwa implemented bila Cobalt?

Leo hii mimi nigundue kiti cha mbao, naweza kutengeneza bila mbao?

Hakuna Google na Microsoft bila servers, hakuna servers bila cobalt, hakuna Iphone bila motherboard na battery hakuna battery na motherboard bila cobalt it's easy ila zunguka zunguka wewee, jifanye kama huoni.
 
Maelezo mengi lakini hauja jibu nilicho uliza ,zaidi umekwenda mbali kwa kuonesha wanufaika wa Mali ya DRC.

South Africa Kuna mali mbona kumetulia,shida ya Congo iko kwa Wacongomani wenyewe.
south africa asilimia kubwa ya migodi inamilikiwa na wamagharibi. Na kuna matukio mengi ya mauaji migodini,
 
Nani kasema cobalt ni rare earths.

Rare earths ndio muhimu kwa duniani ya sasa na inayokuja mpaka kupachikwa jina la gold of the 21st century na huyo Congo unayemtaja hayupo kwenye charts kubwa
Wewe ndo umeenda OP mwenyewe na kuleta kitu ambacho hakipo kwenye mada, ulivyowekwa graph ya rare earth kwenye comment ya Cobalt ulitegemea nini?

Mwaka 2023 rare Earth market value ni $7B wakati Cobalt ilikua ni $30B so kadanganye watoto wenzio rare earth mineral zina thamani kuliko Cobalt.
 
Jeshi ni dhaifu kwasababu uongozi ni dhaifu

Naona Tanzania tunaelekea huko km viongozi hawatastuka
 
Hili swali iulizwe company ya GSM wao wanayo majibu
 
..Na mimi nimeuliza mbona mpaka wa Congo na South Sudan, Afrika ya Kati, Tanzania, Zambia, Angola, hakuna shida?

..kwanini eneo lisilo na amani ni lile linalopakana na Rwanda, na Uganda, wakati mipaka mingine iko shwari?
South africa asilimia kubwa migodi inamilikiwa na wazungu,south sudan kuna nini cha kuvutia wazungu,afrika ya kati kuna vita vya serikali dhidi ya waasi, tanzania,angola na zambia wananchi ni waoga, serikali zao znakubali mikataba ya kinyonyaji huku wananchi hawahoji. manake wananchi wangekuwa na akili wakawa wana maandamano,kupinga na kukataa mikataba hii,hao hao wamagharibi wangewatumia hao wananchi kuwa waasi,vita vya msituni vingetamalaki na mali ingeenda tu kivyovyote vile. wale jamaa wanapiga popote,ukiamka wanapga,ukiwa umelala wanapga,hakuna pa kukimbilia
 
Ni kweli mkuu, ina rasilimali nyingi sana. Lakini, kwani ni Congo DRC pekee ndiyo yenye utajiri wa rasilimali? Mbona nchi zingine tajiri kama Congo DRC hazina machafuko?
Congo inamiliki 70% ya Colbat duniani

Mpaka hapo jiulize
 
Sio kweli, Tanzania mbona tuna rasilimali na hakuna waasi. In fact wazungu wanajichotea almasi tu dhahabu kwa mikataba mibovu ndio sembuse watake vita.

Unataka kuniambia DRC bila vita hao viongozi hawahongeki?

Tuache kusingizia wazungu, hata Mugabe aliachiwa kila kitu ila bado nchi ikamshinda kwa kunuka ufisadi.
shida sio viongozi,wananchi wenye akili ndio walisababisha hii vita,hawawezi kukubali kuona maliasili zao znasombwa. So badala ya njia ya kutumia mikataba feki kujulikana na wananchi wakaamua watumie waasi na mataifa jirani. Like wise tanzania wananchi mkishtuka,watawatumia hawa wapinzani,watatengeneza uikundi vya waasi ili mradi tu wafikie adhima yao.
 
Back
Top Bottom