Kwanini Congo DRC?

viongozi,wananchi wenye akili ndio walisababisha hii vita,hawawezi kukubali kuona maliasili zao znasombwa
Vita zimeanza 1960, hao wananchi walikua na uelewa gani? Enzi hizo Zaire illiteracy ilikua zaidi ya 70%
 
LFP hata Tesla wanatumia sio China pekee ndio mwenye nayo

Acha kuishi ukale Cobalt sio The gold of the 21st century ukijiuliza kwa nini Rare earths zimepewa hilo jina na mataifa makubwa yanapambana kuhodhi na vita kubwa mbili katika ya marekani na China katika awamu hizi mbili hata hii ya tatu zitahusisha maeneo haya utaacha kuona na kusema kila mara Cobalt Cobalt kama vile ndio kila kitu na Congo pekee ndio waliyonayo dunia nzima.
 
Computer ipi hiyo inaweza kufanya kazi bila rare earths ? Una andika kitu unacho kielewa kweli ? Unajua REES zina cover maeneo mangapi katika Computer mpaka ifanye kazi
Boss Electronic za zamani haitumii Rare earth material, mfano engine ya kizamani kama Induction haina rare earth material ila ya kisasa utahitaji,

Computer za zamani semiconducor hazikutumia laser ama sophisticated technology nyengine, kama hujui Computer material kubwa kabisa inayotumika ni mchanga, mchanga ndio unatengeneza silicon, kutoka silicon ndio unapata transistor na hapo zinatoka Cpu, Ram, storage na mambo mengineyo.

Kutengeneza hizo transistor ndio watu wanatumia semiconductor companies kama Tsmc, sababu technology inakua ndio uhitaji nao ukakua wa rare earth ila ni 100% possible kutengeneza electronics bila rare earth materials.
 
Tesla ananunua BYD fanya homework yako vizuri.

Kitu kinaitwa rare sababu kipo kichache lugha inakusumbua? Kitu kuwa uchache hakimaanishi ni muhimu. Udongo wa kiko sisi Tanzania si tupo juu? Ni rare huo Udongo ila unatusaidia nini?

Kitu kinaweza kisiwe rare na Kikawa na Umuhimu mfano mzuri unao mafuta, mafuta ni mengi mno dunia nzima hata sio rare ila thamani yake na mziki wake unaujua wala sina haja ya kuelezea.
 
baba-mwajuma inabidi raisi wa China Xi Jinping akutafute akupe maua yako.
Aloo unampamba vilivyo, hana baya tajiri , kapoaaa.
Kwahiyo mchina ana huruma na wakongo??
Mbona una uhasama gani na west aisee??, unawapiga spana balaa.
 
..kilichokua kinatokea Angola kilikuwa kinafikirisha sana.

..visima vya mafuta vya makampuni ya Marekani vilikuwa upande wa Mpla ambao walikuwa wanasaidiwa kijeshi na Cuba.
Afrika tungeachwa tutengeneze nchi wenyewe, tuchapane vilivyo sisi kwa sisi bila msaada wa huko nje, akili ingekaa sawa.

West walichapana sana wao kwa wao miaka hiyo, chapana kweli mpaka akili zikawakaa sawa kua hatuhitaji kuchapana bali kuchapa wa nje huko.
 
Wewe unaandika vitu unavyo vielewa kweli unataja processor, mara storage sijui transistor kwa hiyo hapa umeona rare earths haina matumizi katika haya maeneo uliyotaja ? Unakielewa kweli unacho kiandika ?

Nimekuambia ni Computer ipi hiyo inaweza kufanya kazi bila rare earths ulichofanya wewe nikuonesha kabisa namna rare earths ni muhimu katika maeneo yote uliyotaja katika computer
 
Lfp ni ya 2022 na ni battery nzito mno possibility ni utumie kwenye hivyo vifaa vya matani.
Kwa hiyo wanaotumia hawatambui haya mpaka ? Na kuzidi kujikita huko

Na hiyo cobalt haina disadvantages ?
 
baba-mwajuma inabidi raisi wa China Xi Jinping akutafute akupe maua yako.
Aloo unampamba vilivyo, hana baya tajiri , kapoaaa.
Kwahiyo mchina ana huruma na wakongo??
Mbona una uhasama gani na west aisee??, unawapiga spana balaa.
Its just interest za China na Africa zinaendana Atleast for now, simpambi mchina ana mabaya yake na yeye ya kutosha ila kutoa zaidi ya $10B kujenga hizo barabara hakuna mtu yoyote wa west atakaefanya hivyo, watakuletea ARV, vyandarua etc ila sio barabara na ukitaka barabara tegemea mikopo yenye Riba.
 
Kwa hiyo wanaotumia hawatambui haya mpaka ? Na kuzidi kujikita huko

Na hiyo cobalt haina disadvantages ?
Cobalt nyepesi,

Chukulia mfano simu kama S24 ultra ina 5000mah

Kila 1000mah kwa lfp ni gram 90 ina. Maana 5000mah ni gram 450 nusu kilo hio just battery pekee, at same time battery ya S24 uzito wake ni gram 90 tu. Umeona hapo utofauti?
 
Kwani China hatoi mikopo ya riba ?
 
Nimekupata mkuu, una hoja usikilizwe.
 
Kwani China hatoi mikopo ya riba ?
Anatoa mingi tu, mingine ina Riba kubwa kushinda west, ila point hapa ni kwamba anaejenga Miundombinu Congo, kwa zaidi ya 10B usd sababu ana migodi ya Cobalt, na Analipa Cobalt kwa Serikali ya Congo (Sio waasi wala Rwanda), wao west wameamua kununua Haya Madini Rwanda hali ya kuwa wa nafahamu fika hayatoki Rwanda. Na wao West Kupitia Mobutu walivunja reli na kuharibu barabara ili Congo isitawalike, na kumpa matuzo kibao.
 
Cobalt nyepesi,

Chukulia mfano simu kama S24 ultra ina 5000mah

Kila 1000mah kwa lfp ni gram 90 ina. Maana 5000mah ni gram 450 nusu kilo hio just battery pekee, at same time battery ya S24 uzito wake ni gram 90 tu. Umeona hapo utofauti?
Acha porojo nyingi, simu na laptop za juzi tu hapo ambazo tulikuwa tunatumia ambazo betri zake hazikuwa built in ambazo watu walikuwa wanaweza kuzibadilisha na wanaenda kuchajisha betri vibandani zilikuwa zinatumia betri za NiCd-Nickel-cadmium na NIMH na wala sio Cobalt.

Simu na Laptop za kisasa ambazo huwezi kuchoma betri(built in batteries) na vifaa vingine vingi pia ndizo zinatumia Cobalt kwa wingi na ni ujanja wa kibiashara uliogunduliwa na makampuni ya electronics ili watu watumie simu na laptop kwa muda mfupi, wasiweze kubadilisha betri au vifaa vingine kwa urahisi wawe wananua simu mpya kila mara. Sio necessity
 
Tatizo ni utajiri wa n chi ya congo
 
Babu huelewi hizo vita zote wanaozipanga ndo haohao watu wa nchi za mgharibi!...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…