JET SALLI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 2,392
- 1,578
Ndugu za wanaJamiiForums, nimepata taarifa leo hii kwamba kumbe CWT ambacho kimekuwa chama cha walimu kwa muda mrefu sasa kimepata chama mwenza ambacho ni chama cha CHAKUHAWATA. Taarifa hii nimeambiwa na mwalimu mmoja leo hii.
Mwalimu huyo amesikitika kuona kwamba pamoja na yeye kujiungana na chama kipya cha CHAKUHAWATA eti amekatwa mara mbili kwa maana ya kwamba CWT wamemkata na CHAKUHAWATA wamemkata, mwalimu amedai kwamba sheria mpya ya Ajira na mahusiano kazini inampa mtumishi nafasi ya kuchagua chama cha wafanyakazi anachotaka yeye ili kujiunga nacho na si kuchaguliwa chama au kulazimishwa kujiunga na chama fulani.
Ameendelea kusema kwamba hakuna sheria inayomruhusu Afisa Utumishi kupitisha makato ya aina mbili kwa chama cha wafanyakazi bila ridhaa ya mwajiriwa
Sasa nasikia leo mishahara ya walimu na watumishi wengine imetoka lkn cha kushangaza wale walimu waliojiunga na chama kipya cha CHAKUHAWATA wamekatwa na CWT kinyume na Sheria za Utumishi.
Hebu Basi tunaojua kudadavua hizi Sheria za utumishi mtusaidie tupate Elimu kidogo au kwa upana zaidi maana JamiiForums ni kisima cha great thinkers.