Kwanini darasani hatujafundishwa kuhusu wanawake hawa walioshiriki kupigania Uhuru wa Tanganyika?

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Nimekutana na picha hii na nimepata maswali sana.

Hawa ni wajumbe wa tawi la wanawake la TANU wakiagana na Mwalimu Nyerere usiku wa kuamkia safari yake ya Umoja wa Mataifa mwaka 1955

Kutoka kulia: Bi. Chiku bint Said Kisusa, maarufu Mama Sakina, Bi. Titi Mohamed, kushoto wa kwanza ni Bi. Tatu bint Mzee na Julius Nyerere yuko katikati.

Hawa akina mama wana historia kubwa katika kuwakusanya wanawake wa Dar es Salaam kuja katika mikutano ya kwanza ya TANU Mnazi Mmoja kuichangamsha kwa vigelegele, nyimbo na mashairi.

Cha ajabu katika wanawake anayejulikana zaidi ni Bibi Titi Mohamed, wengine wote ni wanaume the likes of Oscar Kambona na wengineo.

Naomba kuuliza kwanini darasani hatujafundishwa kuhusu wanawake waliopambani uhuru. Kwanini tumefundishwa tu kuhusu wanaume?


​
 
Huu uzi hautakamilika bila Mohamed Said kufika kudai haki ya "wazee wake"
 
Umezaliwa mwaka gani kwanza tuanzie hapo? Kwenye masomo ya uraia miaka ya kuanzia 1990 kurudi nyuma mbona darasani wameongelewa sana.

Ni yupi na yupi aliongelewa?

Ilikuwa kwenye somo gani?
 
Ni yupi na yupi aliongelewa?

Ilikuwa kwenye somo gani?
Haujajibu swali langu,hao kuna vitabu vimewaongelea na wametajwa michango yao,labda kama ulitaka wapewe exclusive yao pekee jambo ambalo ni ngumu.

Hata huyo bibi titi walimzungumzia tu kama kiongozi wa kundi but haikuwa personal biography sababu hakusimama yeye kama yeye.
 
Zemanda,
Hakuna kitabu cha historia kilichoandika historia ya wanawake waliopigania uhuru wa Tanganyika mfano wa Bi Aza wa Kilwa, Shariffa bint Mzee wa Lindi, Zarula bint Abdulrahman, Nyange bint Chande, Hidaya bint Mabruki wa Tabora, Halima Selengia, Amina Kinabo, Mama bint Maalim wa Moshi kwa kuwataja wachache.

Kipo kitabu cha Suzanne Geiger "TANU Women," Mmarekani huyo angalau kajitahidi kuandika historia hii.
 
Walikuwa viburudisho
Mwichiluwi,
Kiongozi wa akina mama hawa alikuwa Bi. Chiku bint Said Kisusa mke wa Shariff Abdallah Attas.

Alikuwa mama mtu mzima na wanae wawili Mwalimu Sakina na Mwalimu Fatma walikuwa walimu wa shule Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika Muslim School.

Ukoo wa Attas ndiyo waliokuwa viongozi wa Msikiti wa Kisutu nenda nyumza zaidi ya miaka 100.

Kulikuwa na Bi. Halima bint Khamis msichana mdogo miaka hiyo na alikuwa Mwalimu ana chuo chake anasomesha Qur'an.

Hawa akina mama baadhi ni mama zangu na wengine ni shangazi zangu.
 
Mind...
Historia ya TANU imeandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni lakini hakuna majina ya walioasisi African Association Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Cecil Matola kwa kuwataja wachache na waasisi wa TANU Abdulwahid Sykes na Hamza Mwapachu hawamo.

Angalia video hii:
"Sababu ya Sheikh Suleiman Takadir Kufutwa Katika Historia ya Tanzania"


View: https://youtu.be/AMv5l5gvKAY?si=h6CeT-UjmW8BotFb
 
Ila wanawaume hawaangali ilo la utu zima kikubwa waonje
 

Me niliwasomq kiongozi, qkina bi titi Mohammed, akina Siti bin said nawengine.

Mfano Bi titi Mohammed aliacha ndoa ili aendelee ba mapambano.

(Maybe sijui umesoma history had form ngapi ila kuna roles of women in fighting for independence in tz in form 6)
 
Kitafsiriwe ili kurithisha maarifa na historia hii kwa kizazi cha watanzania ambao kiswahili ndio lugha yao
 
Bibi titi kushoto kabisa wengine ni akina nan
 
Ok
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…