Kwanini darasani hatujafundishwa kuhusu wanawake hawa walioshiriki kupigania Uhuru wa Tanganyika?

Kwanini darasani hatujafundishwa kuhusu wanawake hawa walioshiriki kupigania Uhuru wa Tanganyika?

Zemanda,
Hakuna kitabu cha historia kilichoandika historia ya wanawake waliopigania uhuru wa Tanganyika mfano wa Bi Aza wa Kilwa, Shariffa bint Mzee wa Lindi, Zarula bint Abdulrahman, Nyange bint Chande, Hidaya bint Mabruki wa Tabora, Halima Selengia, Amina Kinabo, Mama bint Maalim wa Moshi kwa kuwataja wachache.

Kipo kitabu cha Suzanne Geiger "TANU Women," Mmarekani huyo angalau kajitahidi kuandika historia hii.
Asante sana mkuu kwa kuwaumbua wajuaji. Na Asante sana kuwataja akina mama hao japo kwa uchache ...unaonaje ukaja na makala.maalum.kwa ajili yao naamini andiko LAKO hapa kwenye hii forum.litaishi na kusomwa na vizazi vingi.vijavyo.kama forum hii itaendelea kuwepo
 
Pale Masaki Kuna barabara Ina jina la Ally Bint Said
Ni jambo jema ila vijana wanaokua watakua wanakatiza tu.mitaa hio bila kujua huyo alieandikwa hapo ana mchango.gani kwa yeye kua hapo anatembea free akidunda
.. tunaitaji kitabu maalum pengine wanaweza kuviona na kuvisoma.
 
Inakusaidia nini kwenye maisha kwa mfano kuwajua wapigania uhuru hewa
The Redeemer,
Kitabu cha Abdul Sykes kilipotoka mara ya kwanza na watu kuona kuwa historia iliyokuwa inasomeshwa ina upungufu mkubwa vyuo vikuu vyote vinavyosomesha historia ya Afrika vilitaka kumfahamu mwandishi wa kitabu hicho.

Mwandishi akawa anaalikwa kuzungumza kwenye vyuo vingi duniani kuanzia Kusini ya Afrika, Chuo Kikuu Cha Johannesburg hadi kaskazini ya United States, Northwestern University Chicago, Marekani.

Mialiko ya aina hii ni ndoto ya kila msomi na kila mwandishi ulimwenguni.
 
Wakuu,

Nimekutana na picha hii na nimepata maswali sana.

Hawa ni wajumbe wa tawi la wanawake la TANU wakiagana na Mwalimu Nyerere usiku wa kuamkia safari yake ya Umoja wa Mataifa mwaka 1955

Kutoka kulia: Bi. Chiku bint Said Kisusa, maarufu Mama Sakina, Bi. Titi Mohamed, kushoto wa kwanza ni Bi. Tatu bint Mzee na Julius Nyerere yuko katikati.

Hawa akina mama wana historia kubwa katika kuwakusanya wanawake wa Dar es Salaam kuja katika mikutano ya kwanza ya TANU Mnazi Mmoja kuichangamsha kwa vigelegele, nyimbo na mashairi.

Cha ajabu katika wanawake anayejulikana zaidi ni Bibi Titi Mohamed, wengine wote ni wanaume the likes of Oscar Kambona na wengineo.

Naomba kuuliza kwanini darasani hatujafundishwa kuhusu wanawake waliopambani uhuru. Kwanini tumefundishwa tu kuhusu wanaume?

Tatizo ni mfumo dume mkuu
 
Namna ya kutafuta hela mlifundishwa?
 
Back
Top Bottom