KERO Kwanini Dawasco hawatoi ratiba ya maji?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Joy B

New Member
Joined
Mar 19, 2024
Posts
3
Reaction score
0
Jamani, mimi sielewi kwanini huku Dar maji yanaweza katika kwa muda mrefu bila taarifa. Maji yanakatikaje wiki mpaka wiki mbili bila taarifa?

Ni changamoto tofauti kuwa na uhaba wa maji, lakini changamoto nyingine kabisa kuwepo kwa mgao bila taarifa yoyote.

Sijawahi kuona kipindi maji yanatoka mfululizo, ukiuliza unaambiwa kuna ratiba. Basi tupeni hiyo ratiba ili nasisi tujipange.

Tupeni hiyo ratiba na sisi tuone kwamba kwa mwezi, nina maji siku ngapi, ili namimi niweze kujipanga. Au kuna wanaojua wapi naweza pata ratiba ya maji jijini Dar?
 
hakuna kitu inaitwa DAWASCO... rekebisha heading hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…