Kwanini dini zinazataka wanawake kuvaa vitambaa kufunika vichwa vyao?

Kwanini dini zinazataka wanawake kuvaa vitambaa kufunika vichwa vyao?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Katika maandiko ya dini zote tatu za Uisalamu, Ukristo na Uyahudi suala la wanawake kujifunika vichwa vyao linazungumziwa japo kwa msisitizo tofauti.

Katika Ukristo mazingatio yake ni madogo sana mfano kwa masista wa Kikatoliki na kwa makanisa machache mfano kwa Kakobe, katika Uyahudi siku hizi msisitizo umebaki kwa wanawake kufunika kichwa katika ibada tu, kwa upande wa Uislamu hilo bado ni jambo muhimu sana na tena kwenye nchi nyingine ni shurti kabisa.

Kwa nini mungu katika hizi dini na maandiko yake aliweka hayo maelekezo na sababu za msingi hasa ni zipi?
 
Ngoja watumishi(wenye uchambuzi mpana unaoeleweka kwa maneno machache)waje watuhabarishe/ndiyo kutuhubiria kwa ushahidi.

NB;
Kumbukumbu zangu zinanionesha hata Musa alijifunika hadi kichwani alipoenda kupokea amri kumi za Mungu.

Vilevile makuhani na mfanano wao walikuwa wenye kujifunika hadi vichwani mwao.Ingawa sijasema kwamba Mashariki ya kati kuna hali ya majangwa na upepo mkali.Walijisitiri mbela za Bwana Mungu wao.
 
Kichwa cha mwanamke ni mume wake.

1 Wakorintho 11
3. Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.

Hakiongelewi kichwa hiki cha physically
 
Katika maandiko ya dini zote tatu za Uisalamu, Ukristo na Uyahudi suala la wanawake kujifunika vichwa vyao linazungumziwa japo kwa msisitizo tofauti. Katika Ukristo ...
Sio dini ni Mila na tamaduni za ki babarism za za kiyahudi na kiarabu ambazo kimsingi ni Mila za eneo Moja ambazo dini Tatu za kiyahudi, kiislamu na Kikristu zilichipukia.Mila hizo kwa kuwa ziliibuka katika kipindi Cha babarism ambapo mwanamke alionekana sio binaadamu sawa na mwanaume Bali ni Mnyama kazi anayeongea (Instrumentum vocale)

Basi mabwana walioleta Imani hizo walikuwa na hayo mamila Yao ambayo kimsingi yanagandamiza Sana haki za wanawake hata kwenye nyumba za ibada hawatakiwi wawe viongozi wasimame mbele ya wanaume.
 
Kichwa cha mwanamke ni mume wake.

1 Wakorintho 11
3. Lakini nataka mjue ya kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu.

Hakiongelewi kichwa hiki cha physically
Hii inahusianaje na kufunika kichwa kwa kitambaa??
 
Wakristo (hapa wakatoliki ( wake kwa waume), wa orthodox, Lutheran, Anglican ), Waislam na wayahudi viongozi wao hufunika vichwa vyao kwa namna yoyote iwe kwa hijab,nikab, bagarashia, kofia kubwa au yenye ufuniko mdogo.

Waislam na wayahudi wameenda mbali zaidi uhusisha mpaka waamini wake.

Ufunikaji wa vichwa unahusisha jinsia zote kwa wanawake unatiliwa zaidi mkazo kwa sababu ya matamanio na stara.
 
Sio dini ni Mila na tamaduni za ki babarism za za kiyahudi na kiarabu ambazo kimsingi ni Mila za eneo Moja ambazo dini Tatu za kiyahudi, kiislamu na Kikristu zilichipukia.Mila hizo kwa kuwa ziliibuka katika kipindi Cha babarism ambapo mwanamke alionekana sio binaadamu sawa na mwanaume Bali ni Mnyama kazi anayeongea (Instrumentum vocale ).
Mkuu kwa barbarians kama Vikings wanawake hawakuwa wanafunika vichwa, dini ndio zilileta hili jambo.
 
Ufunikaji wa vichwa unahusisha jinsia zote kwa wanawake unatiliwa zaidi mkazo kwa sababu ya matamanio na stara.
Hii napinga, ni nadra sana mwanaume kumtamani mwanamke kwa kutazama kichwa chake.
 
Wayahudi
yom-kippur-489828672_4x3.jpg
Jewish-man-shofar-Rosh-Hashana.jpg
boy-bar-mitzvah-service-Torah-Western-Wall.jpg
 
Kabisa Kichwa chake urembo tosha ,ukija kifuani napo konzi ,ukicha wezere na neema za allah mtihano napo.

Inatakiwa wajisitiri.
Ni nadra kuona mwanaume ameposti au amegeuza shingo kwa mwanamke kwa sababu ya uzuri wa kichwa tu, ila mara nyingi sana na asilimia kubwa ya wanaume hupata kiwewe na sehemu nyingine za mwili wa mwanamke hata kama kichwa chake sio kizuri kabisa.
 
Hii napinga, ni nadra sana mwanaume kumtamani mwanamke kwa kutazama kichwa chake.
Kila kiungo cha mwanamke huleta matamanio kwa mwanaume.

Matamanio baina ya mwanaume kwa mwanaume hutofautiana.

Kuna wanaume ambao huvutiwa na uzuri wa nywele, miguu, mikono, makalio, ngozi, macho, lips, meno, sera, maziwa, shingo n.k kila kiungo ukionacho kwa mwanamke kinaweza leta matanio kwa mwanaume fulani hata kama kwako hakileti muamsho wa kihisia.
 
Kama ni hivyo kwa nini msisitizo ni kufunika kichwa tu na sio mwili wote kabisa asionekane kabisa?
 
Mkuu kwa barbarians kama Vikings wanawake hawakuwa wanafunika vichwa, dini ndio zilileta hili jambo.
Soma Moja wapo ya sifa za babarism kama zilivyoelezewa na philosopher Fredrick Engels . Moja wapo ya sifa ni kumgandamiza mwanamke, na kumuweka kwenye kundi la wanyama kazi. Kitendo Cha kufunika nywele ni kumkinga eti asionwe na kutamaniwa na meanamme mwingine
 
Back
Top Bottom