Dalton elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 373
- 829
Mhe. Sophia Mwakagenda ameuliza swali la nyongeza Bungeni kutaka kujua ni lini Serikali italifanyia kazi suala la kugawa Jimbo la Mbeya Mjini kwa sababu ya ukubwa wa Jimbo hilo na wingi wa watu. Ombi la kugawanywa Jimbo la Mbeya Mjini lilitolewa na Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Spika wa Bunge, Dkt. Tulia.
Hoja hiyo inaibua maswali kadhaa yanayohitaji tafakuri. Je, hoja ni matakwa ya wananchi wa Mbeya Mjini au ni utashi wa Mbunge? Kama ni matakwa ya wananchi ilitolewa lini, katika kikao gani kilichohusisha wananchi? Je, wananchi walimtuma Mbunge apeleke hoja Bungeni? Je, hoja hiyo ni matakwa ya CCM ambacho ndicho Chama tawala katika Jimbo hilo? Kama ni hoja ya CCM, ilijadiliwa katika ngazi za Chama?
Je, Mheshimiwa Sophia Mwakagenda ni mkazi wa Jimbo la Mbeya Mjini au Jimbo mojawapo katika Wilaya ya Rungwe? Kama anatoka Jimbo la Rungwe, kuna maslahi gani kwake na Jimbo la Mbeya Mjini? Kama ametoa hoja kwa kuwa ni Mbunge anayetokea Mkoa wa Mbeya; je ni Jimbo gani kimsingi linalotakiwa kugawanywa kati ya Mbeya Mjini na Mbeya Vijijini? Je, kati ya Jimbo la Kyela na Jimbo la Mbeya Mjini ni lipi linahitaji kugawanywa kwa sababu tajwa? Je, uhitaji wa Jimbo la Mbeya Mjini nini hasa? Je, unafikiri changamoto zake zitakwisha kwa kuligawa Jimbo hilo ili kupata majimbo mawili?
Pamoja na ukweli kuwa mjadala huu unahusu watu wote, lakini itakuwa ni vizuri sana endapo wakazi wa majimbo yote ya Mkoa wa Mbeya watatoa maoni yao wakitoa ushahidi wakiunga mkono hoja. Tutapenda kusikia maoni kutoka Mbeya Mjini, Mbeya Vijijini na Kyela kuhusu uhitaji wa kugawanywa kwa majimbo yao.
Wapo wanaofikiri kuwa hoja ya kugawanywa kwa majimbo inatokana na ukweli kuwa ni mahesabu ya wanasiasa kwa siku za usoni. Je, upo ukweli wo wote katika hoja hii? Je, hoja hii ni ya kisiasa ili kupunguza ushindani wakati wa uchaguzi ujao na hivyo kugawa nafasi kwa wanasiasa? Je, hii ni hoja ya wanasiasa katika Jimbo la Mbeya Mjini? Wananchi wanasemaje? Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 3 Mei 2023.