Mkurugenzi wa Mashtaka amepewa dokezo kuwa kuna uhalifu umefanyika na ni uhalifu ambao unagusa taasisi mbalimbali nyeti na hata watu ambao tunaweza kusema ni watu maarufu. Tuhuma ambazo zimetolewa jana si ngeni lakini kilichodokezwa zaidi ni madai kwamba kilichofanyika hakikuwa wizi wa ulaghai tu bali ulikuwa ni uhalifu dhidi ya uchumi na taasisi zetu. Hivyo ameombwa kuchunguza na kuleta mashtaka.
Nimeambatanisha hapa sheria mbili (kwenye sheria ya NPS angalia ibara hasa ya 16) na nyingine mtu anaweza kujisomea kuwa hakuna mtu mwenye uwezo na madaraka ya kuleta uchunguzi wa kihalifu (criminal investigation) kama Feleshi. Aangalie ushahidi uliopo na aliambie Taifa kuwa hakukuwa na uhalifu wowote uliofanyika na kama hakuna uhalifu wale wote wanaohusishwa na Kagoda warudishiwe 'fedha zao'. ..
Kwa ufupi.. Feleshi alitakiwa kufanya haya yote yeye mwenyewe na binafsi naamini anatakiwa kumteua Public Prosecutor chini ya article 22 ya NPSA. Sheria ya Anti-Money Laundering nayo imeambatanishwa kuwasaidia watu kupima madai yaliyotolewa..
Ndugu zangu, kama Feleshi angekuwa anatumia madaraka yake ipasavyo kusingekuwa na haja za kina Hosea na Kamati Teule. Binafsi ninaamini mmoja watu ambao kutokana na madaraka yake amekuwa ni sehemu iliyohalalisha kukua na kukomaa kwa ufisadi nchini. Nimewahi kuandika hili kwa kirefu huko nyuma na katika Kagoda tunalirudia tu kwani angekuwa ni mtu anayetumia madaraka yake vizuri na ipasavyo hata tume ya EPA isingeundwa wala Luhanjo asingemchunguza Jairo!
Wakati umefika wa kuanza kutaka huyu jamaa aliyeapa kufanya kazi hii aaifanye kama hawezi ni bora ajiuzulu ili mtu mwingine mwenye nia na uwezo wa kusimamia sheria zetu kufanya kazi hiyo.
Kama yeye mwenyewe anaona hawezi kuchunguza jambo hili au anaona kwamba hawezi kuwa impartial ana uwezo wa kumchagua independent prosecutor kufanya uchunguzi - kuanzia na hizi nyaraka zilizowekwa jana - na hatimaye kuleta mashtaka yapasayo.
Mzee Mwanakijiji, hili la DPP kufungua mashitaka dhidi ya Kagoda haliwezi kufanyika kamwe, unless otherwise!
Natumaini umesoma mamlaka ya DPP,
Naomba nikuwekee na kifungu chenyewe ili tuelewane.
Part II Sec 9,-(1) (a) decide to prosecute or not to prosecute in relation to an offence;
Ni kwa kutumia kifungu hicho, DPP anaweza kufungua mashitaka, ama anaweza asifungue na hakuna wa kumuuliza sababu, hata rais hawezi. Siku zote nimekuwa naimba haka kawimbo cha madaraka ya ajabu ya DPP. Kwa lugha nyepesi, hata kama jinai imetendeka na ushahidi upo kwa asilimia 100%, DPP ana mamlaka kuendesha kesi au kutokuendesha na hakuna mamlaka ya kuuliza ni kwa nini.
Kuna kipindi cha nyuma, Ijumaa moja, mtoto ambaye ni mwana pekee wa kiume wa kigogo mmoja, ilichukua bastola ya baba yake akamiminia risasi 6 adui yake mmoja na kufa papo hapo. Mtoto huyo alichukuliwa na kulazwa polisi, Jumatatu asubuhi mtoto alifikishwa mahamani kusomewa shitaka la mauaji. Jioni ya siku hiyo DPP alipeleka Nolle Prosequi, Jumanne kesi ikafutwa, mtoto akaachiwa na kupelekwa nje ya nchi, baba kigogo wakayamaliuza na familia ya marehemu, kesi ikaishia hapo.
Powers hizo za DPP kupeleka Nolle, pia hazihojiwa na mamlaka yoyote, wala DPP hapaswi kutoa sababu zozote za nolle kwa yoyote.
Sababu za DPP kutoanzisha mashitaka dhidi ya Kagoda, nimezieleza kwenye thread yangu ya 'Kagoda Kamwe Haitafikishwa Mahakamani!'
Pasco.