Kwanini DPP Feleshi anatakiwa kuleta mashtaka dhidi ya RA na YM na wengin juu ya Kagoda

Huu mziki umepigwa muda mrefu lakini wenyewe wameamua kukaa kimya labda kutusahaulisha? Tuendelee kuimba au labda kuna Plan C?

Labda hiyo plan C ikipatikana inaweza kusaidia kuwafikisha hawa watuhumiwa mahakamani. Yani unashindwa kushangaa kwamba pamoja na documents zote zilizopo na vyombo vyote vya dola vilivyopo, serikali imeshindwa kabisa hata kuwafungulia mashtaka hawa mapapa na manyangumi.

Nadhani kama atapatikana independent prosecutor, basi angalau kesi inaweza kufunguliwa, vinginevyo tutaendelea kukumbusha hizi hujuma hadi siku tutakapoiondoa ccm madarakani ndipo tutafanikiwa kuwashitaki wezi wetu.
 
kwenye red mkuu, nina tatizo. Idadi ya wasomi tulionao ni kubwa mno (ukilinganisha na tulipopata uhuru) au basi tufute baadhi ya degrees kama zilitolewa kimakosa kama Kenya walivyokuwa wamependekeza kwa Mr. Kivuitu!
Na kama unasema mfumo ni mbaya na wanaofaidika nao ndio tuliowapa madaraka sio rahisi kuachia wenyewe kutokana na 'maumivu' ambayo wameshasababisha mpaka sasa na wanajua wakiachia yatajulikana zaidi ya hayo.
thus, a step forward ni kama Mr. Msemakweli alivyoamu kufanya kama mtu binafsi anayeguswa na matatizo ya Tanzania na Watanzania. Wengine wanadhani maisha yake yatakuwa hatarini lakini ndiyo asili ya maisha huwezi kuachieve bila kurisk!
Mwisho nakukumbusha kuwa Tanzania itamkumbuka zaidi Marehemu Stanslaus Katabalo (Mungu ailaze roho yake mahala pema) zaidi ya wale waliochukizwa na msimamo wake ambapo tunaona miaka 20 baadae Loliondo kuna 'nchi ndani ya nchi'!
Tukimpa support ya HALI NA MALI itakuwa na maana zaidi ya kukaa na kuamini kuwa "hatuwawezi hawa mafisadi"!
 
Ndio maana tumeweka hizo sheria umechukua muda kuzisoma? Feleshi akitaka anaweza kuchagua Independent Prosecutor or Investigator kama Ken Starr
Tatizo letu sie Watanzania hatusomi documents, ila ni wazuri sana wa kubabaisha na kujifanya tunajua vitu wakati hatusomi. Nenda kwa wafanyakazi wa Serikali wakienda kwenye vikao, mara zote huenda hata document hawana, eti anataka kusikiliza ndio achangie! wezetu wanasoma na kuchambua hizo documents ili waweze kujenga hoja. Na ndio maana siku zote watu wetu wamekuwa wakiuziwa Mbuzi kwenye ngunia badala ya Tenga ili amuone huyo mbuzi kama anafaa au laa.

Thanks MMJ for your contribution.
 
Katiba mpya, katiba mpya yenye kuondoa migongano ya kimaslahi. Baaasi.......
 
Mwanakijiji you are not serious this time!

State organs ni watch dogs kwani wewe hujui hilo!

Yes ni mbwa tena wenye meno makali na yenye sumu kali sana akiuuma hakika huwezi kupona huo ndio ukweli. lakini toka lini mbwa akauma bila kuamrishwa? Mbwa wa namna hiyo hana adabu maana anaweza kumg'ata hata mwenye mbwa! Sana sana wamiliki wa mbwa wakali ikiwa wanahisi mbwa wanaweza kung'ata hadi watoto pale nyumbani na kubughdhi wageni wake wapendwa uishia kumfungia mbwa wake kibandani.

For sure kama tupo mean, tumuulize mwenye mbwa siyo kumhoji mbwa mwenyewe, ukweli ubaki kuwa ukweli, mbwa anaye mtii owner ndio mbwa bora na aliye pata mafunzo vyema.
 
Mkuu,
Natofautiana na wewe kidogo kwenye red. Huwezi kumfananisha Ghadafi na viongozi wetu wa Tanzania. Kwa mtazamo wangu Ghadafi ni mtu mwenye kupenda maendeleo ya nchi yake na Afrika kwa ujumla tofauti na hawa viongozi wetu wa Tanzania ambao kazi yao ni kujineemesha wao na familia zao bila kujali wananchi na nchi kwa ujumla. Jaribu kusoma hii article hapo chini ujihabarishe zaidi.
Citifmonline - Why the West wants the fall of Gaddafi
Kwa taarifa ni Ghadafi ndie aliyesaidia kwa kiwango kikubwa sana Afrika kuwa na urahisi wa technologia. Isingekuwa yeye africa kwenye maswala ya Technologia mambo yangekuwa magumu sana.
 
kila jambo linawakati hata wapindishe sheria wakati ukifika yote yatafanyiaka tu wala msiwe nawasiwasi nani alijua Gadafi angevuliwa madaraka?
 


Thanks Bro MMJ,

Umenipa mwanga mwingine zaidi,

Sasa ndio naona umuhimu wa watu kuitaji katba mpya ili utendaji kazi uonekane upya sio sasa twaenda hoe hae
 
Mkuu Arafat sawasawa umenena vyema...... hivi Feleshi akulupuke afanye tu kazi bila maelekezo ya mwajili wake ataendelea kweli kuwa kazini..? Nafkili ameamua kufanya tu yale mwajili wake anapenda afanye ili nayeye watoto wake wapate ugali...! Nina uhakika kabisa yote aliyoyaandika MwkJJ Feleshi anayafahamu sana tu tena kwa mapana zaidi kwa maana si rocket science..!
 
Ooooh,haya
wimbo wa ufisad unakuja na remix kila kukicha
 

Siyo rahisi hasijue kazi yake, ukitaka kujuwa hapa Tanzania tatizo ni jinsi ya kutumia rasilimali watu vizuri, wewe niambie baada ya Mzee Mkapa kuondoka pale Ikulu, unadhani aliondoka na watumishi wote wa Umma?

Unaweza kushangaa ukampa Mwanakijiji urais na bado DPP akawa Feleshi ukashangaa anavyochapa kazi na kushinda keshi dhidi ya Mafisadi! Hapa ni mchezo wa kufungia mbwa bandani, we angalia swala la Jairo haiwekani Rais hadi Bunge wanashindwa kutoa maamuzi yao juu ya kitu kinachoeleweka wanapoteza fedha za walipa kodi kuchunguza kitu ambacho wanakifahamu!? Kupoteza muda na kuacha kushughulikia mambo ya muhimu wanakalia muda mwingi kwa jambo ambalo halipo hata kwenye list yoyote ya kazi za maendeleo, tutakesha hapa miaka mitano tunaimba Jairo..Jairo hadi 2015 bila hadi decimal point moja ya GDP kupanda.


Mara nyingine mi namlilia Lyatonga na Sokoine maana Jambo la Jairo lisinge tupotezea hata siku moja tunge kuwa tumesha sahau siku nyingi sana.


Hiyo tume ya EPA yenyewe sijui kama mnajuwa kuwa wataalam waliofanya nao kazi ambao hawakuwa UWT wanakufa mmoja mmoja kwa njia za ajabu! Leo wanajifanya kuwa karibu na Msema kweli kana kwamba kuna jambo kaliongea jipya? Mambo yote aliyoongea msema kweli lililo jipya hapo ni hilo la kufafanua kuwa fedha alizochukuwa RA na Manji hazikuingia katika kampeni za Kikwete hivyo watu wasidanganywe lakini mengine yote na wanayajuwa na wanawajuwa wahusika fika.
 
Ndio maana tumeweka hizo sheria umechukua muda kuzisoma? Feleshi akitaka anaweza kuchagua Independent Prosecutor or Investigator kama Ken Starr

Kwa nini ni lazima Feleshi? Hakuna uwezekano mwingine wa kuwafungulia mashtaka hawa watu? Ina maana kama Feleshi akikataa ndio kusema mtu hawezi kabisa kushtakiwa. Mimi sio mwanasheria naomba ufafanuzi.
 
Hapa kwetu Tanzania sheria inatafsiriwa kulingana na mtuhumiwa anayehusika. Chamsingi ni kuungana na kuwa suport wanaharakati wanao jitolea kupigania haki za watz kama huyu Bw. Kainerugaba Msemakweli
 
Hata mimi ningekuwa Feleshi ningekaa kimya. Kwani hizi issue kwa mtazamo wake na wengine walio serikalini zina tija gani??? Nadhani wana mambo mengine muhimu sana ya kushughulikia na kwa hiyo hawana muda mchafu wa kupoteza na mambo (ambayo kwa mtazamo wake Feleshi na wenzake) ya hovyo kama Kagoda na EPA kwa ujumla au Meremeta na mengineyo!!


Kwa kuyashughulikia ni sawa na kufanya biashara kichaa!!
 
Thanks Bro!! Ngoja nizame, nitarudi huku!!
 
tatizo nchii hii kila kitu kinaingizwa siasa ata jambo la taaluma bado siasa inawekwa mpaka masuala ya imani za dini wanasiasa waingiza siasa zao
 


Kuanzia leo tunakuchaguwa wewe uje kuifanya hiyo kazi.
 

Mkuu propaganda za Gaddafi ziache kule kule. Gaddafi na familia yake nao hawakujineemesha? Kuwa alikuwa anajali maisha ya Walibya kwa ujumla? Labda ndio maama alipiga marufuku ufundishaji wa Kiingereza Libya wakati anapeleka watoto wake Uingereza kusoma Kingereza hicho hicho tena kwenye very expensive schools na ku hire private teachers Uingereza kufundisha watoto wake kingereza. Eti Ghadafi ndie aliyesaidia kwa kiwango kikubwa sana Afrika kuwa na urahisi wa technologia? Usinchekeshe. Heri ameondoka maana angetulazimisha kila Mwafrika afuge kuku kama alivyowalzimisha Walibya. Anyway, nisije nikaharibu hii thread.
 

Mzee Mwanakijiji, hili la DPP kufungua mashitaka dhidi ya Kagoda haliwezi kufanyika kamwe, unless otherwise!

Natumaini umesoma mamlaka ya DPP,

Naomba nikuwekee na kifungu chenyewe ili tuelewane.

Part II Sec 9,-(1) (a) decide to prosecute or not to prosecute in relation to an offence;

Ni kwa kutumia kifungu hicho, DPP anaweza kufungua mashitaka, ama anaweza asifungue na hakuna wa kumuuliza sababu, hata rais hawezi. Siku zote nimekuwa naimba haka kawimbo cha madaraka ya ajabu ya DPP. Kwa lugha nyepesi, hata kama jinai imetendeka na ushahidi upo kwa asilimia 100%, DPP ana mamlaka kuendesha kesi au kutokuendesha na hakuna mamlaka ya kuuliza ni kwa nini.

Kuna kipindi cha nyuma, Ijumaa moja, mtoto ambaye ni mwana pekee wa kiume wa kigogo mmoja, ilichukua bastola ya baba yake akamiminia risasi 6 adui yake mmoja na kufa papo hapo. Mtoto huyo alichukuliwa na kulazwa polisi, Jumatatu asubuhi mtoto alifikishwa mahamani kusomewa shitaka la mauaji. Jioni ya siku hiyo DPP alipeleka Nolle Prosequi, Jumanne kesi ikafutwa, mtoto akaachiwa na kupelekwa nje ya nchi, baba kigogo wakayamaliuza na familia ya marehemu, kesi ikaishia hapo.

Powers hizo za DPP kupeleka Nolle, pia hazihojiwa na mamlaka yoyote, wala DPP hapaswi kutoa sababu zozote za nolle kwa yoyote.

Sababu za DPP kutoanzisha mashitaka dhidi ya Kagoda, nimezieleza kwenye thread yangu ya 'Kagoda Kamwe Haitafikishwa Mahakamani!'

Pasco.
 
Kwa nini ni lazima Feleshi? Hakuna uwezekano mwingine wa kuwafungulia mashtaka hawa watu? Ina maana kama Feleshi akikataa ndio kusema mtu hawezi kabisa kushtakiwa. Mimi sio mwanasheria naomba ufafanuzi.
Crucifix, DPP ni mungu mtu, akikataa ndio amekataa, hapaswi kutoa sababu kwanini hataki wala hakuna mamlaka ya kumuuliza sababu. Mamlaka hayo amepewa na katiba yetu!

Kisheria akiona yeye hawezi, ana mamlaka ya kumteu mtu kuendesha hayo mashitaka, tatizo hawezi kata tawi la mti alioukalia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…