Kwanini dunia inamchukulia Adolf Hitler kama kiongozi katili katika historia ya Dunia?

Kwanini dunia inamchukulia Adolf Hitler kama kiongozi katili katika historia ya Dunia?

hermanthegreat

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
1,274
Reaction score
3,282
Dunia imekuwa ikitawaliwa na viongozi wengi walio makatili na wanyama sana mfano.ukiachana na Hitler(1889-1945) kuna
1. Joseph Stalin(1878-1953)
2. Pol Pot (1925-1998)
3. Saddam Hussein (1937-2006)
4. Iddi Amin (1952-2003)

Nachohitaji kufahamu zaidi kutoka kwenu ni kwanini Hitler anatajwa zaidi kama kiongozi katili mno mbali na kutenda mambo mazuri yafuatayo:-

[emoji117]Alizuia Uvutaji wa sigara katika nchi ya ujerumani. Hitler alikuwa muathirika wa Uvutaji sigara hadi pale alipopona 1919 na kuzuia kabisa hata watu wengine.
[emoji117]Alianzisha mashindano ya Olympic kama tamaduni iliyosahauliwa nchini ujerumani.
[emoji117]Alikuwa kiongozi wa kwanza kujali watoto. Alipenda watoto wote wasome, wafundishwe ukakamavu wawe na afya njema hadi leo nchini Ujerumani kuna malipo ya 200 Euro kwa kila mtoto.
[emoji117]Alitoa ajira. Baada ya Hitler kuingia madarakani alikomesha tatizo la ajira kupitia uzalishaji, Ulinzi, kilimo. Nk.
[emoji117]Alidumisha umoja baina ya nchi za ulaya eg. Marekani na Urusi.
[emoji117]Alilinda wanyama. kufuatia kifo cha mpwa waake kwa kujinyonga, Hitler aliacha kula nyama na kuzuia nchi nzima ulaji wa nyama na kuwalinda wanyama.

Sasa kwanini dunia inamchukulia Hitler kama gaidi mno zaidi hata ya Napoleon?
karibu kwa mchango.
View attachment 1829408
IMG_20210625_132027_413.JPG
View attachment 1829407
 
Dunia imekuwa ikitawaliwa na viongozi wengi walio makatili na wanyama sana mfano.ukiachana na Hitler(1889-1945) kuna
1.Joseph Stalin(1878-1953)
2.Pol Pot (1925-1998)
3.Saddam Hussein (1937-2006)
4.Id Amin (1952-2003)
Nachohitaji kufahamu zaidi kutoka kwenu ni kwanini Hitler anatajwa zaidi kama kiongozi katili mno mbali na kutenda mambo mazuri yafuatayo:-
[emoji117]Alizuia Uvutaji wa sigara katika nchi ya ujerumani. Hitler alikuwa muathirika wa Uvutaji sigara hadi pale alipopona 1919 na kuzuia kabisa hata watu wengine.
[emoji117]Alianzisha mashindano ya Olympic kama tamaduni iliyosahauliwa nchini ujerumani.
[emoji117]Alikuwa kiongozi wa kwanza kujali watoto. Alipenda watoto wote wasome, wafundishwe ukakamavu wawe na afya njema hadi leo nchini Ujerumani kuna malipo ya 200 Euro kwa kila mtoto.
[emoji117]Alitoa ajira. Baada ya Hitler kuingia madarakani alikomesha tatizo la ajira kupitia uzalishaji, Ulinzi, kilimo. Nk.
[emoji117]Alidumisha umoja baina ya nchi za ulaya eg. Marekani na Urusi.
[emoji117]Alilinda wanyama. kufuatia kifo cha mpwa waake kwa kujinyonga, Hitler aliacha kula nyama na kuzuia nchi nzima ulaji wa nyama na kuwalinda wanyama.

Sasa kwanini dunia inamchukulia Hitler kama gaidi mno zaidi hata ya Napoleon?
karibu kwa mchango.
View attachment 1829408View attachment 1829409View attachment 1829407
Hitler aliua wayahudi wengi sana directly na indirectly, pia alifanya uvamizi kwa miaka ya karibuni wakati Napoleon alifanya invasion huku Europe miaka ya 1800 wakati ambapo hapakuwepo na maendeleo ya upashanaji wa habari mfano hakukuwepo Tv's
 
Huyu jamaa kwa wajerumani sio dikteta ni shujaa

Kwanza alipokuwa prime ministers alivunja mkataba waliowekewa ujerumani na France, na British na hawa ndio chanzo cha yote hayo yanayoitwa udikteta.

Kwa muda mrefu wajerumani walisubiri mtu wa kuvunja mkataba huo wa kinyonyaji uliowataka kulipa faini pesa ndefu, kutokuzalisha silaha, kuacha kutumia meli za kivita baharini!

Kwa muda Hitler aliivunja serikali ya kijerumani iliyoitwa weimar government. Ambayo kiuhalisia wajerumani waliichukia kwani, ilibariki mkataba huo.

Kwanza waingereza ndio watu kwa asilimia kubwa walichochea Vita kuu ya pili, kutokana na chokochoko zake kwa German's, hasa guns competition. Nae Hitler kwa maslahi ya nchi yake hakutakiwa kukubali upuuzi.

Pia Vita kuu ya pili ilihamasisha kwa kiasi kikubwa African revolution. Kutokana na baadhi ya ex soldiers wa kiafrika kupelekwa vitani na wachache waliorudi wakawa influencer kwa wenzao.

Hitler bila Vita ya pili pengine ujerumani angeifanya kuwa taifa lenye nguvu kuliko sasa.
 
Hua nasema kwamba kwa kila mtu ukiamua kutafuta utakayoona ni mazuri yake utayapata na ukiamua kutafuta utakayoona mabaya yake utayapata.

Salamu ya Nazi maarufu kama 'Salute' imepigwa marufuku nchi nyingi ukionwa umeifanya inakuhakikishia kwenda jela. Kama unajiuliza Hitler alikua na ubaya wa kiasi gani ona hapa;

Giorgos Katidis aliyekua midfielder wa timu ya Ugiriki na AEK Athens alishinda goli halafu akafanya saluti ya Nazi.

Kilichofuatia ni chama cha mpira cha Ugiriki kumu-exile Katidis katika level zote za timu ya taifa ya Ugiriki. AEK ikamfutia mkataba wake, timu zote za ligi kuu zikagomea kumsajili.

Career ya Katidis iliishia pale akiwa mdogo tu hazidi miaka 24. Utetezi wake akadai hajui kama ile ni salamu ya Nazi, lakini watu wakahoji kwa umri wake na nchi aliyokulia kuna uwezekano kweli akawa hajawahi kusikia kuhusu Nazism? Hitler au Holocaust?

Funny thing ni kwamba siku anapiga hii saluti ilikua ni siku ya kuikumbuka Holocaust duniani.
 
Huyu jamaa kwa wajerumani sio dikteta ni shujaa

Kwanza alipokuwa prime ministers alivunja mkataba waliowekewa ujerumani na France, na British na hawa ndio chanzo cha yote hayo yanayoitwa udikteta.

Kwa muda mrefu wajerumani walisubiri mtu wa kuvunja mkataba huo wa kinyonyaji uliowataka kulipa faini pesa ndefu, kutokuzalisha silaha, kuacha kutumia meli za kivita baharini!

Kwa muda Hitler aliivunja serikali ya kijerumani iliyoitwa weimar government. Ambayo kiuhalisia wajerumani waliichukia kwani, ilibariki mkataba huo.

Kwanza waingereza ndio watu kwa asilimia kubwa walichochea Vita kuu ya pili, kutokana na chokochoko zake kwa German's, hasa guns competition. Nae Hitler kwa maslahi ya nchi yake hakutakiwa kukubali upuuzi.

Pia Vita kuu ya pili ilihamasisha kwa kiasi kikubwa African revolution. Kutokana na baadhi ya ex soldiers wa kiafrika kupelekwa vitani na wachache waliorudi wakawa influencer kwa wenzao.

Hitler bila Vita ya pili pengine ujerumani angeifanya kuwa taifa lenye nguvu kuliko sasa.
Sasa kama kwa Ujerumani ni shujaa mbona Ujerumani wamepiga marufuku 'Salute'?
 
1. Hitler hakudumisha umoja wa mataifa ya Ulaya. Alitaka kuyatawala ndio ugomvi ulipoanzia

2. Hitler hakupenda watoto ndio maana naye hakuzaa, sijui kama uwezo huo hakuwa nao. Alikuwa na jeshi la watoto linaitwa Hitler's Youth na vitoto vya miaka 16 vilipelekwa kwenye mapigano. Hawezi muita mtu huyu kama mpenda watoto

3. Hitler aliua Wayahudi zaidi, na wana deko sana wale watu. Mpaka vitendo vile wakavitungia jina special kuwa ni Holocaust wakati ni ethnical cleansing kawaida kama za kule Bosnia na Hezgovina na kwingine

4. Joseph Stalin hawezi tajwa ovyo kwa vile alikuwa upande wa allies. Na baada ya vita aliishi mpaka 1953, hakuwa bad guy mbele ya scholars wengi wa Ulaya. Wao wanazingatia aliyewasumbua ndio maana Pol Pot hutomsikia sana. Stalin alikuwa gaidi maradufu kuliko Hitler, alianzisha purges kwake na kaua sana kule Poland na Finland
 
Mkuu umesema kweli kabisa, kasoro point namb 2 hapo nabisha hoja yako, Hitler alipenda sana watoto na hata ushahidi wa videos upo, wanasema alikaribisha sana watoto nyumbani kwake na alifurah kuwaona.

Sababu ambayo hakuwa na mtoto haijulikani haswa, ila amewahi kusikika akisema kitu kama "sihitaji kuleta wa kwangu kwenye hii dunia" aliona dunia kama vile pahala pasipofaa, lakini baadhi ya wanahistoria wanadai korodani zake zilipasuka wakati wa WW1
 
Sasa kama kwa Ujerumani ni shujaa mbona Ujerumani wamepiga marufuku 'Salute'?
Kupiga marufuku salute haimaniishi wanamchukia.

Ila ili kuepusha kuharibu mahusiano na nchi zingine alizokuwa na mzozo nazo ikiwemo Britain na France.
Kwani hawataki waonekane kwamba walikuwa wanamkubali wazi.

Ndio maana hata kwenye soka ligi ya epl na ufaransa ni marufuku kupiga salute ya nazi.
 
Kupiga marufuku salute haimaniishi wanamchukia
Ila ili kuepusha kuharibu mahusiano na nchi zingine alizokuwa na mzozo nazo ikiwemo Britain na France..
Kwani hawataki waonekane kwamba walikuwa wanamkubali wazi..

Ndio maana hata kwenye soka ligi ya epl na ufaransa ni marufuku kupiga salute ya nazi
Saluti ya nazi ilipigwa Ugiriki. Na kuna kipindi Vieira alishangilia katika mtindo ambao ulilalamikiwa kua ni another version of Salute.

Huko huko Ujerumani wanapomuona shujaa umewahi sikia mtu mwingine anayeitwa Hitler?
 
Mkuu umesema kweli kabisa, kasoro point namb 2 hapo nabisha hoja yako, Hitler alipenda sana watoto na hata ushahidi wa videos upo,wanasema alikaribisha sana watoto nyumbani kwake na alifurah kuwaona
Sababu ambayo hakuwa na mtoto haijulikani haswa,ila amewahi kusikika akisema kitu kama "sihitaji kuleta wa kwangu kwenye hii dunia" aliona dunia kama vile pahala pasipofaa, lakini baadhi ya wanahistoria wanadai korodani zake zilipasuka wakati wa WW1
Wale watoto uliokuwa unawaona anazurula nao ni watoto wa majenerali wa Wehrmacht lazima awapende. Watoto wa Joseph Goebbels na Heinrich Himmler angewachukia vipi wakati baba zao ni marafiki zake wakubwa na washirika wake, na hao wazazi wao waliwapenda sana.

Walikuwa wanakuja nao kwenye parties, aliwaona wazazi wao wakati wanafunga ndoa, alilazimika apende sana kile wazazi wao wanapenda, hakuwa na sababu ya kuwachukia. Hakuna sehemu inaonesha alifanya juhudi za ziada kupenda watoto. Tatizo ni pale alipotumia Hitler's Youth kwenye frontline. Vitoto vidogo vinaenda kupigana na wanajeshi wa Canada waliokomaa vinashinda kwenye ruins za miji mazingira magumu sana.

Yeye alitoa kile Wajerumani wanapenda: ajira, superiority, chuki dhidi ya Wayahudi, kisasi dhidi ya kuonewa baada ya WW1, uchumi mkubwa, jeshi imara baada ya kupigwa vitani na kulazimishwa wawe na kajeshi kadogo.

Hitler hakuwa rude kama Stalin ambaye hata wanae alikuwa anawachukulia kama raia wa kawaida. Mmoja alijipiga risasi, mwingine alikamatwa vitani frontline, mkewe naye sijui alijiua. Hitler hakupenda watoto ila hakuwa mtu wa kuchukiza watu wake wa karibu. Na alikuwa mstaarabu sana mbele ya Wajerumani waliokuwa mlengo wake. Hata mtu kama Field Marshall Erwin Rommel aliyeshiriki kupanga kumuua Hitler alipewa option na Hitler kwamba kwa sababu ya heshima na sifa kubwa alizonazo kwenye jeshi, akubali ajiue ili azikwe kwa heshima ya kijeshi na familia yake ipewe stahiki zote. Angekuwa Stalin pale angeua familia nzima kwa fujo.

Kwanza story nyingi tunazopewa za Hitler zimejazwa uongo ili kumuonesha mbaya sana zaidi ya alivyo. Pale Ujerumani kuna mchanganyiko wa asili nyingi za watu kutoka Poland, Austria (kama Hitler mwenyewe), UK, France. Kwa nini awachukie Wayahudi na apate kuungwa mkono sana, kwa nini hakuchukia wenye asili ya Poland. Ukiuliza maswali kama aya utaitwa Holocaust synthesizer.
 
Back
Top Bottom