Mzee Kijana
JF-Expert Member
- Nov 25, 2011
- 1,442
- 1,140
Wale watoto uliokuwa unawaona anazurula nao ni watoto wa majenerali wa Wehrmacht lazima awapende. Watoto wa Joseph Goebbels na Heinrich Himmler angewachukia vipi wakati baba zao ni marafiki zake wakubwa na washirika wake, na hao wazazi wao waliwapenda sana.
Walikuwa wanakuja nao kwenye parties, aliwaona wazazi wao wakati wanafunga ndoa, alilazimika apende sana kile wazazi wao wanapenda, hakuwa na sababu ya kuwachukia. Hakuna sehemu inaonesha alifanya juhudi za ziada kupenda watoto. Tatizo ni pale alipotumia Hitler's Youth kwenye frontline. Vitoto vidogo vinaenda kupigana na wanajeshi wa Canada waliokomaa vinashinda kwenye ruins za miji mazingira magumu sana.
Yeye alitoa kile Wajerumani wanapenda: ajira, superiority, chuki dhidi ya Wayahudi, kisasi dhidi ya kuonewa baada ya WW1, uchumi mkubwa, jeshi imara baada ya kupigwa vitani na kulazimishwa wawe na kajeshi kadogo.
Hitler hakuwa rude kama Stalin ambaye hata wanae alikuwa anawachukulia kama raia wa kawaida. Mmoja alijipiga risasi, mwingine alikamatwa vitani frontline, mkewe naye sijui alijiua. Hitler hakupenda watoto ila hakuwa mtu wa kuchukiza watu wake wa karibu. Na alikuwa mstaarabu sana mbele ya Wajerumani waliokuwa mlengo wake. Hata mtu kama Field Marshall Erwin Rommel aliyeshiriki kupanga kumuua Hitler alipewa option na Hitler kwamba kwa sababu ya heshima na sifa kubwa alizonazo kwenye jeshi, akubali ajiue ili azikwe kwa heshima ya kijeshi na familia yake ipewe stahiki zote. Angekuwa Stalin pale angeua familia nzima kwa fujo.
Kwanza story nyingi tunazopewa za Hitler zimejazwa uongo ili kumuonesha mbaya sana zaidi ya alivyo. Pale Ujerumani kuna mchanganyiko wa asili nyingi za watu kutoka Poland, Austria (kama Hitler mwenyewe), UK, France. Kwa nini awachukie Wayahudi na apate kuungwa mkono sana, kwa nini hakuchukia wenye asili ya Poland. Ukiuliza maswali kama aya utaitwa Holocaust synthesizer.
Hata Waingereza waliwatumia watoto vitani. Mimi babu yangu alipenlekwa Burma akiwa na miaka 14 tu!