Kwanini Elimu isitolewe kwa kiswahili mpaka PHD?

mi nafikiri uchumi unategemea sana elimu na elimu ili iwe bora inabidi lugha ya kufundishia ieleweke vizuri kwa anaefundisha na anaefundishwa. naona kwa connection ya mbali uchumi wa nchi ni function ya lugha (uelewekaji wake kwa watumiaji wake). ila kama ulivyosema kusambaa kwa lugha ni function ya uchumi wa nchi ilikoanzia. ishu ya kukosa viwanda vya uchapaji ni tatizo tutakalo tatua tutakapoamua kuanza kutumia lugha yetu kujifunzia.
 

Address uchumi, weka a good political framework, mengine haya yatajiset yenyewe.

Ukianza na lugha bila kuwa na uchumi, utafanya mbio za sakafuni.

Ndio hapo utakuta unahitaji kuchapa vitabu halafu hata printing presses huna.

Ukiwa na uchumi mzuri utaweka printing presses shule etc, hata watu wa nje watakuja kusoma, maana una uchumi.

Kama kujua lugha yako mwenyewe ndiyo deal the indigenous people of the Congo and Amazon rain forests would have been the most advanced.
 
kujifunzia lugha mama ni kichocheo cha ubunifu. chukulia mfano biblia ilivyotafsiriwa na watu wakawa na uwezo wa kuchallenge baadhi ya mambo na kuzaliwa kwa madhehebu mbalimmbali. ingekuwa haijatafsiriwa tungekuwa tunafuata kama maroboti.
 
Mimi siyo mama kijana wangu. Nimeandika kutokana na combination ya urguments kwamba lugha inafanya mtu aelewe vizuri na kwamb lugha inaleta maendeleo ya haraka. Uko sahihi kwa upande wako. Nimetoa mfano, ikiwa sasa mtu anasoma kwa kiswahili hadi anamaliza elimu ya msingi hajui kuandika, tatizo la lugha linaingiaje hapo. Elimu ya Tanzania inatia huruma kwa sababu kama ni kwenye scale, trend sasa iko nyuma ya sifuri. Lugha gani iliyokuwa ikitumika wakati elimu ilipokuwa na kiwango kizuri, ambayo sasa haitumiki elimu imeshuka? Tusikimbilie kutoa majibu mepesi kwa masuala magumu yanayohitaji tafiti za kisayansi na nia za kweli. Suala la ubovu wa elimu ya Tanzania lina mizizi na wala si sababu ya lugha. NINAKATAA

Majibu mepesi yasiyofanywa kwa umakini ndiyo hayo ya kuanza kufundisha watoto kujibu maswali. Maswali yenyewe ni multiple questions, true or false na matching items ambazo hazimpi mtoto nafasi ya kukua kiakili. Na huwezi kubisha kwa hili kwa sababu pamoja na mitihani ya ovyo ovyo hiyo bado wanafunzi wanafail. hadi sasa kina mlugo wakadhani kuongeza division na kushusha marks za kufaulu kutapandisha kiwango cha elimu!. Hili siy balaa? Bila kuaddress hili suala critically, mtaaanza kusema kila kabila wafundishe kikwao na kusiwe na mtaala rasmi.

Lugha haijakuzuia wewe kubuni technologia yako kwa sababu hulazimishwi kuiita jina la kigeni. Wewe kama ni mbunifu, buni na uone kama kuna mtu atakulazimisha atakupangia jina la technolojia yako.

Tatizo letu ni kubwa na tusisingizie lugha.

kujifunzia lugha mama ni kichocheo cha ubunifu. chukulia mfano biblia ilivyotafsiriwa na watu wakawa na uwezo wa kuchallenge baadhi ya mambo na kuzaliwa kwa madhehebu mbalimmbali. ingekuwa haijatafsiriwa tungekuwa tunafuata kama maroboti.
 
Elimu inazidi kushuka kwa ajili ya lugha? Lugha hii imetumika tangu nchi hii izaliwe na ilikuwa ikielewaka kwa wafundishaji na wafundishwaji na kiwango cha elimu kilikuwa juu. Nini kimeingilia kati sasa lugha hiyo hiyo haieleweki tena kwa wafundishaji na wafundishwaji? Ni kutu gani sasa idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika japo wamemaliza elimu ya msingi inayotolewa kwa kiswahili imeongezeka?

Ni vizuri kuangalia suala hili kwa macho ya utafiti badala ya kukimbilia majibu yasiyothibitika. Elimu ya Tanzania haiadhiriki kwa sababu ya lugha. Hata siku moja!. Lugha ni kisingizio tu.

 
mmkuu umenielewa vibaya, nilikuwa nazungumzia lugha mama/ya kuzaliwa nayo. ni kweli usemayo elimu yetu inachangamoto nyingi na nyingi zinasababishwa na uzembe. pia sisemi kuwa elimu yetu imeshuka kwa sababu tunatumia lugha ya kigeni. mi naona tulikosea uchaguzi wa lugha mwanzoni kabisa mwa mfumo wetu wa elimu.
 
Red Giant Soma historia ya how the Italian City States influenced Europe and started the Renaissance mpaka leo tunaishi kwa kufuata concepts zilizoanzishwa enzi hizo.

Hawakuanza kwa kusema "tutilie mkazo watu kuongea Kitaliani", actually the respectable language back then was Latin. Latin ndo ilikuwa kama Kiingereza na kiitaliano kilikuwa parochial kama Kiswahili.

Lakini wali embrace trade, mpaka customs zao na mambo yao yakatambaa Europe nzima. Mpaka patrons wakaanzisha vyuo vikuu na ku patronize art na kuleta usomi ambao eventually ulileta the inventions of machinery Industrial Revolution.

Hawakuanza kwa kusema tukifanya Kiitaliano kiwe prominent zaidi ya Kilatini.

It was trade that elevated them, not language.
 
lakini utakuzaje uchumi ukiwa na mainjinia, wahasibu na wataalamu wa kilimo ambao sehemu kubwa ya elimu yao wameekariri na wanapata ugumu kuihusianisha na mazingira yao?
[SIZE=+1]The results of the study indicate that there is a considerable difference between the two groups of students: those who studied the science course in the native language (Ss2) and those who studied in a foreign language (Ss1). Findings showed that Ss2 gave more scientifically acceptable answers to the questions than did Ss1. Besides, Ss1 had more difficulties in explaining the reasons for their answers; presumably because of the scientific language they used in their written explanations.[/SIZE]
[SIZE=+1]Abundance of scientifically unacceptable responses by Ss1 identifies a close relationship between the language and conceptual understanding in the science course. In other words, foreign language used in the science course becomes a barrier for students. Science is a discipline in which experiential and concrete examples should be presented as an in-class process in order to improve the level of students' conceptual understanding. Thus, if students are exposed to everyday concepts by using their native language, it will be easier for them to understand scientific concepts in a classroom setting. This will take the load off the students and will give more time to present experimental examples to comprehend scientific ideas more efficiently. From the teachers' point of view, it will also be easier to diagnose scientific misconceptions by asking students to give everyday examples for the topic taught. Briefly, misconceptions in "The Energy Unit" may be overcome by encouraging students to talk about them. The more students express their own ideas about those concepts, the more they will be aware about the limitations and problems in their understanding the concepts. Therefore, the scientific language which mediates the meanings of the concepts is important and the native language should be preferred for such purposes.[/SIZE]
[SIZE=+1]The ideas which students bring into the science classroom may originate from their early experiences with the physical world. These ideas may include, for example, the knowledge that motionless objects do not have energy or that objects cannot continue moving if there is no frictional force. It may be that such intuitive ideas can be developed towards more formal scientific ideas throughout teaching about energy. The role of the teacher may be considered to be that of helping students to modify their intuitive ideas to relate them to the formal scientific ideas. This can be done by encouraging students to talk about their own intuitive ideas either in small groups or as a whole class. This may serve two purposes: firstly when students talk through their own ideas, they may use the ideas in familiar situations and thus consolidating the relationship between science theory and the experiences with which they are familiar, students' confidence in theory can be increased by using ideas to make sense of a wider range of tasks. Such tasks may involve language activities, such as explaining an industrial process or writing an imaginative piece of prose. Secondly, and perhaps more important in the case of energy, students may become aware that different people think differently, and this could provide a useful foundation upon which to introduce the scientific ideas about energy.[/SIZE]
[SIZE=+1]As stated by Vygotsky (1978), language accommodates a medium for learning and is a tool to construct a way of thinking. Learning takes place in a social context through language and students need to internalize knowledge in a related context using language. If students are not competent in that language, they may come up with misconceptions in understanding. Thus, the results of this study are consistent with several studies (Cummins, 1989; 1992; Rosenthal, 1996; Spurlin, 1995) conducted in the field in terms of the effect of teaching in a foreign language on conceptual understanding in science courses. Teaching the main courses such as mathematics and science through a foreign language may lead to misconceptions in understanding.[/SIZE]
[SIZE=+1]Consequently, students should be well informed about the different uses of words in different contexts, so that they can better understand the concept of "energy". However, this process requires time for students to investigate and discuss the related ideas in a language in which they can express themselves without any difficulty. No matter how good they are at foreign language in terms of grammar and vocabulary, language competence in a foreign language may be a handicap while expressing their own ideas for students. As the findings of the study indicate, ideas for the construction of energy conservation need to be restructured carefully and analogically. This process could be done through the native language by discussing forms of energy in relation to physical systems, investigating more novel phenomena which are related to the topic and contextualizing the concept of energy.[/SIZE]
[SIZE=+1]New regulations about teaching the academic courses in native language will help students' conceptual understanding. For further studies, it is suggested to conduct research at English medium universities in different departments such as engineering and business administration, with a wide range of samples and to come up with different ideas[/SIZE]
 

Bora kukariri lugha kuliko kukariri dhana.

Ukikuza uchumi utatengeneza mashine zako kulingana na mahitaji yako, ambazo Uingereza pengine hazipo, utazipa majina yako.

Ukikuza lugha utazipa mashine za muingereza majina ya Kiswahili.

Unataka kipi kati ya viwili hivi?
 

[TD="width: 3%"]1.1[/TD]
[TD="width: 97%"]Educational research worldwide and in Hong Kong have shown that students learn better through their mother tongue. The educational benefits of mother-tongue teaching include :[/TD]





[TD="width: 100%, colspan: 2"] Mother-tongue teaching has positive effects on students' learning;
[/TD]

[TD="width: 100%, colspan: 2"] Most students prefer learning in the mother tongue;
[/TD]

[TD="width: 100%, colspan: 2"] Students learning in the mother tongue generally perform better than their counterparts using English as medium of instruction (MOI); and
[/TD]
articles kama hizi ziko nyingi sana google.
 
Kuna kitu kimoja cha kushangaza kidogo, uchunguzi unaonesha, kati ya somo la lugha ya kiingereza na lile la kiswahili kule sekondarini, wanafunzi wanafeli zaidi la kiswahili kuliko la kiingereza.
 
nafikiri ntapenda kusoma kitabu jinsi europe ilitoka ujingani. unaweza kunipa jina?. kuna post niliona umepost the fate of africa cha Meredith. nimekimalza hivi majuzi. yametajwa mambo kadhaa yaliyo sababisha africa kuwa hivi. kitu nilichotamani ni kitabu hiki kingekuwa kimetafsiriwa ili watu wengi wapate kukisoma lakini language barrier imelinyima taifa na watu wengi elimu hii na nyingine nyingi.
 
Kuna kitu kimoja cha kushangaza kidogo, uchunguzi unaonesha, kati ya somo la lugha ya kiingereza na lile la kiswahili kule sekondarini, wanafunzi wanafeli zaidi la kiswahili kuliko la kiingereza.
hii sio habari ya kweli.
 

mkuu unatakiwa uelewe ili kitu kieleweke kinatakiwa kiwasilishwe kwa lugha chanzo ambayo ilitumika kugudua somo husika, mathalani lugha ya kiingereza kuna wataalamu wengi mfano sir isaac newton,kwa hiyo kama na sisi tutagundua nadharia mbalimbali kwa lugha yetu hapo nitakuunga mkono hivi kitaka kuamini maneno yangu katumie facebook kwa kiswahili ndo utaona tatizo lilipo kuna kiswahili kigumu ni ya heri ingetumika tu lugha husika:cool2::A S wink:
 
Kiswahili kimekosa hata maneno na majina yanayotumika kila siku kama vile Receipt = risiti, spanner = spana, corner = kona, motor car = motokaa, Lorry = lori... list ni ndeeefu sembuse kuwa na majina ya kisomi???
Kukidharau kiingereza ni katika mambo ya kijinga kabisa.
 
recept ni stakabadhi na siio risiti. maneno mengine tututohoa.
 
Hizi ndizo factors za kujiuliza na kutupa mwongozo sahihi kwamba lugha si suluhisho la kuinuka kwa elimu ya Tanzania. Ni visingizio tu vinavyoasisiwa na ukosefu wa nia wa serikali wa kuinua kiwango cha elimu ili tuzidi kuwa na taifa la watu wapumbavu. Unajua mtu mjinga akienda shule na akamaliza shule bila kuelimika anakuwa mpumbavu kabambe!.

Ndio hao kina mulugo na mashangingi wanaopewa nafasi za uongozi bila sifa. Kwa sababu elimu sahihi hawana, na kujifunza hatawatki, wanaogopa hata kutumia wataalam sahihi, wanapobaki kuumba umba tu mikakati vioja kama kuongeza madaraja, kutunga maswali ya mitihani yasiyohitaji mtu kufikiria katika kuyajibu, ili kumpa kila mtoto nafasi ya kubahatisha majibu,, kushusha alama za kufaulu, kuchakachua matoke. Baada ya kuona shida iko pale palei, wanaanza kusema lugha bila kufikiri kwamba hii lugha ndiyo imetumika miaka yote na ni ya kimataifa na elimu ilikuwa safi tu. Na kumbe kwenye language exams, wanafunzi wanafaulu zaidi English kuliko kiswahili.


Aibu kwa j.k na serikali yake.
Kuna kitu kimoja cha kushangaza kidogo, uchunguzi unaonesha, kati ya somo la lugha ya kiingereza na lile la kiswahili kule sekondarini, wanafunzi wanafeli zaidi la kiswahili kuliko la kiingereza.
 
nakumbuka wakati nipo kidato cha pili kwenye somo la chemistry tulikuwa tunafundishwa na mkorea. Alikuwa hajui english vizuri,tulipo muliza alizema kwao kuanzia awali mbaka wanaingia chuo wanasoma kwa kutumia lugha ya kwao. english wanatumia kidogo sana.

Hofu yangu itakuja sehemu moja. tutakapo anza kutumia kiswahili kuwa kama lugha rasmi ya kufundisha. kwa ninavyo jua mimi kiswahili kina ugumu wake. tukitaka iwe hivyo kwanza tujiulize Je watanzania tupo sawa kwenye misamiati ya miswahili? japo uchunguzi kidogo tu nilio gundua lugha yetu bado haija jitosheleza kimisamiati
 
Kama hutegemei kutoka nje ya Tanzania, au kufanya kazi na wageni katika managerial position/technical positions, go on with Kiswahili to university level
Nadhani hapa tunachanganya kitu, kuna kupata maarifa kwa kutumia lugha ya kiswahili mfano mdogo mtu aliesoma umeme wa magari kwa kiswahili, mwingin kwa kiingereza na mwingine kwa kirusi wanatofauti gani kama wote wamepata practical training ya namna ya kutengeneza gari ila kila mmoja kwa lugha yake na hasa ukizingatia mfumo wa gari ni ule ule? Changamoto hapa ni kwamba tunategemea kwa asilimia karibu zote vitabu na reference mbalimbali kutoka nje ambazo nyingi zimeandikwa kwa lugha za kiingereza hivyo kwa nchi kama yetu kidogo inatakiwa muda wa kutosha kurasimisha hili pia lazima tujiandae pia kwa kukipa kipaumbele Kiingereza kama somo la muhimu sana kwa kuwaandaa walimu wa kutosha wenye uwezo wa kuzungumza na kukitumia kiingereza kiufasaha ili kwa wale wataobahatika kuwa wa kimataifa wataendelea na kithungu.

Kwa ujumla kinachotangulia kwanza nadhani ni KUJENGA UCHUMI IMARA then suala la lugha kufundishia darasani linafuata, mbona tunapokea wataalamu wa Kirusi, Kijapan, Ufaranswengine toka Africa magharibi hawajui kithungu wala kiswahili lakini wanapiga kazi kama kawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…