Kwanini Elimu isitolewe kwa kiswahili mpaka PHD?

Kwanini Elimu isitolewe kwa kiswahili mpaka PHD?

Una uhakika kwamba kuendelea kwa hizo nchi kumetokana na wao kutumia lugha zao ?

Angalia sana hapa badala ya kutatua tatizo unaweza kutengeneza tatizo.., fahamu kwamba lugha ni njia ya mawasiliano tu.., badala ya kuanza kungangania watu watumie kiswahili kufundishia ungeimiza watu wajifunze na lugha nyingi kadri wawezavyo ili kuwaze kuwasiliana na wengi ipasavyo..

Kama point yako ni kwamba mother tongue inaeleweka zaidi kwanini wasukuma, wasifundishiwe kisukuma, wachagga kichagga na wahaya kihaya..., natumaini hapo hawa watu wataelewa zaidi na haya makabila yatakua kiuchumi zaidi.., husasan wagogo na watu wa kusini wajaribu hii njia


kuendelea kwa nchi kuna sababu nyingi na lugha ni mojawapo, tena kubwa tu. hapo kwenye red inatakiwa tushangilie sana kwa kiswahili kuweza kueleweka na watanzania wengi.
 
umenena vema mkuu. watu wanasema kiswahili hakijitoshelezi, inamaana kikorea, kinorway, kirusi,kigiriki,kipoland,kisweeden, kidanish,kidutch, kijapan na kichina ni bora kuliko kiswahili?.juzi kati nilikuwa nacheki muvi ya mr.peabody and sherman (animation). kiswahili kimetajwa humo. hii ni lugha kubwa yenye wazungumzaji karibu millioni 100. wazungu walitufundisha kwa lugha zao ili watutumie cha ajabu tunaendeleza huo mfumo. tatizo la lugha ni kubwa kuliko tunavyofikiri.

ahsante kwa kunielewa kaka. Tumekosa maamuzi japo tatizo twalifahamu.
 
Mbona hatujapishana. Kama hutegemei kutoka nje ya TZ au hutegemei kuwasiliana na wasiojua kiswahili, ni vema kuendelea na kishwahili. It depends on your aspirations. Vyuo vya Veta darasa la saba wanasoma kiswahili, hawahitaji kiingereza maana wao ni wa humu humu au nchi za kiswahili. Lakini kama unategemea kwenda Oxford, Cambridge, UN, AU and the like, fikiria mara mbili kusoma swahili as a medium of instructions at all levels of schooling.
kiingereza tutasoma kama somo la kutuwezesha kuwasiliana kimataifa. unafikiri wajapan, wachina au warusi huwa hawaendi kusoma au kufanya kazi uingereza na marekani?
 
Kiongozi, mimi na wewe tupo pamoja sana. Ninachosema, tusisingizie kwamba, kwa kuwa hatutumii kiswahili kufundishia ndiyo maana walimu na wanafunzi wote hawaelewi wanachokifanya ni hivyo anguko la elimu Tanzania. Lazima tufanye utafiti wa kina wa sababu za kushuka elimu kwa kuwa hata wakati elimu iko juu (kabla ya wamu hii), lugha ya kufundishia ilikuwa ni kizungu.

Nilisema nchi alizozitaja kama japan, china, rusia sijui na wapi kuwa zinatumia lugha yake na zimeendelea, nimesema hazikuendelea kwa ajili ya kutumia lugha. Zichunguze utaona ziko katika daraja gani kwa maswala ya uvumbuzi na ukuzi wa Sayansi na Techdnolojia.

Elimu ya Tanzania haitakua kwa kubadilisha lugha ya kufudishia kwa sababu hat idadi ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi ( ambayo inafundishwa kwa kiswahili) wakiwa hawajui kusoma wala kuandika inazidi kukua. Hapo tatizo ni lugha?

Utafiti umeonyesha kwamba katima masomo ya Lugha Secondary kwa maana ya Kiswahili na Kiingereza, wanafunzi wanafaulu zaidi somo la kiingereza kuliko kiswahili.

Bado natoa wito kwamba suala la elimu Tanzania si la kupapasa papasa na kutoa masuluhisho ya kubuni. Tunahitaji kuangalia kwa kina mizizi ya anguko hili na kukubali gharama za kurekebisha badala ya kukimbila kisingizio cha lugha ambacho scientifically si kweli.

ok mkuu nimekupata sasa tunaenda sawa
 
kiswahili ndiyo kinaongoza kwa ufaulu.
Mimi bado sijashawishika kwamba eti kiingereza ndio sababu ya kufeli.
Hivi kwa mfano somo la hisabati ambalo ni miongoni mwa masomo yanayoongoza kwa kufelisha, kiingereza kinasababishaje?
 
ahsante kwa kunielewa kaka. Tumekosa maamuzi japo tatizo twalifahamu.
ni kama watu tuliopotea nnjia lakini tunaona uvivu kurudi kuanza upya kisa tumeshafika mbali.
 
Mimi bado sijashawishika kwamba eti kiingereza ndio sababu ya kufeli.
Hivi kwa mfano somo la hisabati ambalo ni miongoni mwa masomo yanayoongoza kwa kufelisha, kiingereza kinasababishaje?
mkuu hata tukifundisha kwa kiswahili lazima kunasomo litakuwa linaongoza kufelisha na bila shaka litakuwa hisabati. hisabati sio somo la number tu lisilokuwa na maana. hiyo maana ndiyo tunaikkosa kwa kufundishwa kwa kiingereza. wengi wetu tumekariri tu earth as a sphere sijui caliculus na kinematics lakini practical applicatiions zake hatuelewi sawasaawa. watu wanakariri haadi formula derivation?
 
Maendeleo kupitia sayansi yanahitaji kufahamu lugha ya sayansi; hisabati hiyo ndio itakayokupa mawe ya kuvukia mtoni. Nchi nyingi zilizoendelea zilihimiza umahili wa hisabati kwanza mengine yalikuwa ziada.
 
kiingereza tutasoma kama somo la kutuwezesha kuwasiliana kimataifa. unafikiri wajapan, wachina au warusi huwa hawaendi kusoma au kufanya kazi uingereza na marekani?

Hao uliowataja wanajua kiingereza, wasiojua hawatoki nje kufanya kazi zinazohusus interaction/communication na watu.
 
Umenikumbusha kitabu cha roots cha Kiswahili, nilikisoma nikiwa mdogo.

Kiswahili inabidi kikue katika jamii kwanza kabla ya kutumika masomoni, ama sivyo Kiswahili cha masomoni kitakuwa tofauti na cha mtaani kama Kiingereza kilivyo tofauti na Kiswahili halafu tutarudi square one bila ya kuwa na faida katika nyanja za kimataifa.

Ningependa kukisoma kitabu hiki. Nitakipata wapi? kimetafsiriwa na nani na kilichapishwa nchi gani?
 
Ningependa kukisoma kitabu hiki. Nitakipata wapi? kimetafsiriwa na nani na kilichapishwa nchi gani?

Muda mrefu sana umepita hata sikumbuki aliyetafsiri na kilipochapwa. Nakumbuka nilikisoma darasa la nne au la tano mwanzo.

Jaribu kwenda kwenye bookshop kubwa kama ile ya hapa Samora Avenue karibu na Askari Monument.

Pia angalia contacts za Mkuki na Nyota Publishers hapa http://www.mkukinanyota.com/
 
Back
Top Bottom