Lugha ina mchango mkubwa ktk kuelimika na kujielimisha hasa inapotumiwa km njia ya kufundishia. Tatizo sio kingereza ama kiswahili tunaweza tukatumia hata kifaransa ama kisukuma. Tatizo ni lini tunaaanza kujifunza lugha hio.
Tunajifunza lugha na kuimudu vzr tukiwa chini ya miaka kumi. Hivyo km tutaamua kutumia kiingereza km njia kufundishia basi tuanze kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu na km itakuwa ni kiswahili basi tufanye hivyo2. Uganda, Kenya, India, Zambia nk wamefanya hvy na hawana matatizo km ya kwetu. Kumbukeni waafrika kusini enzi za utawala wa ubaguzi wa rangi walikataa kutumia lugha zao mama km njia za kufundishia.
Elimu ya Tanzania ina matatizo mengine mengi lkn lugha ni kubwa zaidi.
Haitoshi kuendelea kiuchumi na kiteknilojia km tu tutakuwa na njia muafaka ya kufundishia ila itatusaidia kama inavyowasaidia wenzetu. Kuna vitu vingine vya kufanya ili kuweza kujitegemea kiuchumi na kiteknolojia.
Njia na namna tunavyofanya sasa kutumia kiswahili na kingereza inatuathiri kwa kiasi kikubwa sana. Inafikia hatua kingereza hatukifahamu vzr na kiswahili hatukifahamu kwa ufasaha hata kwa ngazi ya mawaziri, wabunge na wengineo.
Kuna matatizo mengine ktk elimu ya Tanzania lkn la lugha ni kubwa zaidi.