Kwanini Elimu isitolewe kwa kiswahili mpaka PHD?

Kwanini Elimu isitolewe kwa kiswahili mpaka PHD?

nakumbuka wakati nipo kidato cha pili kwenye somo la chemistry tulikuwa tunafundishwa na mkorea. Alikuwa hajui english vizuri,tulipo muliza alizema kwao kuanzia awali mbaka wanaingia chuo wanasoma kwa kutumia lugha ya kwao. english wanatumia kidogo sana.

Hofu yangu itakuja sehemu moja. tutakapo anza kutumia kiswahili kuwa kama lugha rasmi ya kufundisha. kwa ninavyo jua mimi kiswahili kina ugumu wake. tukitaka iwe hivyo kwanza tujiulize Je watanzania tupo sawa kwenye misamiati ya miswahili? japo uchunguzi kidogo tu nilio gundua lugha yetu bado haija jitosheleza kimisamiati
Hiyo ndio changamoto mkuu ukichanganya na watu kukichukulia poa hasa vyombo vya habari kwa kuendekeza kuweka maneno yao yasiyo rasmi kwenye habari ambazo ni serious na mwisho wa siku na wananchi wanazidi kuwa wachovu kwenye matumizi ya kiswahili
 
Lugha ina mchango mkubwa ktk kuelimika na kujielimisha hasa inapotumiwa km njia ya kufundishia. Tatizo sio kingereza ama kiswahili tunaweza tukatumia hata kifaransa ama kisukuma. Tatizo ni lini tunaaanza kujifunza lugha hio.

Tunajifunza lugha na kuimudu vzr tukiwa chini ya miaka kumi. Hivyo km tutaamua kutumia kiingereza km njia kufundishia basi tuanze kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu na km itakuwa ni kiswahili basi tufanye hivyo2. Uganda, Kenya, India, Zambia nk wamefanya hvy na hawana matatizo km ya kwetu. Kumbukeni waafrika kusini enzi za utawala wa ubaguzi wa rangi walikataa kutumia lugha zao mama km njia za kufundishia.

Elimu ya Tanzania ina matatizo mengine mengi lkn lugha ni kubwa zaidi.

Haitoshi kuendelea kiuchumi na kiteknilojia km tu tutakuwa na njia muafaka ya kufundishia ila itatusaidia kama inavyowasaidia wenzetu. Kuna vitu vingine vya kufanya ili kuweza kujitegemea kiuchumi na kiteknolojia.

Njia na namna tunavyofanya sasa kutumia kiswahili na kingereza inatuathiri kwa kiasi kikubwa sana. Inafikia hatua kingereza hatukifahamu vzr na kiswahili hatukifahamu kwa ufasaha hata kwa ngazi ya mawaziri, wabunge na wengineo.

Kuna matatizo mengine ktk elimu ya Tanzania lkn la lugha ni kubwa zaidi.
 
Hela yenyewe ya kutafsiria kwa hisani ya wamarekani?

Kukua kwa lugha ni zao la kukua uchumi, kama vyandarua tunahitaji wamarekani, sijui kama tunaweza hili.

inabidii tuanze sasa kutafsiri. nguvu=kani x umbali uliosafiriwa kwenye uelekkeo wa kani. see! siio hata ngumu
 
Kiongozi, mimi na wewe tupo pamoja sana. Ninachosema, tusisingizie kwamba, kwa kuwa hatutumii kiswahili kufundishia ndiyo maana walimu na wanafunzi wote hawaelewi wanachokifanya ni hivyo anguko la elimu Tanzania. Lazima tufanye utafiti wa kina wa sababu za kushuka elimu kwa kuwa hata wakati elimu iko juu (kabla ya wamu hii), lugha ya kufundishia ilikuwa ni kizungu.

Nilisema nchi alizozitaja kama japan, china, rusia sijui na wapi kuwa zinatumia lugha yake na zimeendelea, nimesema hazikuendelea kwa ajili ya kutumia lugha. Zichunguze utaona ziko katika daraja gani kwa maswala ya uvumbuzi na ukuzi wa Sayansi na Techdnolojia.

Elimu ya Tanzania haitakua kwa kubadilisha lugha ya kufudishia kwa sababu hat idadi ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi ( ambayo inafundishwa kwa kiswahili) wakiwa hawajui kusoma wala kuandika inazidi kukua. Hapo tatizo ni lugha?

Utafiti umeonyesha kwamba katima masomo ya Lugha Secondary kwa maana ya Kiswahili na Kiingereza, wanafunzi wanafaulu zaidi somo la kiingereza kuliko kiswahili.

Bado natoa wito kwamba suala la elimu Tanzania si la kupapasa papasa na kutoa masuluhisho ya kubuni. Tunahitaji kuangalia kwa kina mizizi ya anguko hili na kukubali gharama za kurekebisha badala ya kukimbila kisingizio cha lugha ambacho scientifically si kweli.

mkuu unatakiwa uelewe ili kitu kieleweke kinatakiwa kiwasilishwe kwa lugha chanzo ambayo ilitumika kugudua somo husika, mathalani lugha ya kiingereza kuna wataalamu wengi mfano sir isaac newton,kwa hiyo kama na sisi tutagundua nadharia mbalimbali kwa lugha yetu hapo nitakuunga mkono hivi kitaka kuamini maneno yangu katumie facebook kwa kiswahili ndo utaona tatizo lilipo kuna kiswahili kigumu ni ya heri ingetumika tu lugha husika:cool2::A S wink:
 
Bora kukariri lugha kuliko kukariri dhana.

Ukikuza uchumi utatengeneza mashine zako kulingana na mahitaji yako, ambazo Uingereza pengine hazipo, utazipa majina yako.

Ukikuza lugha utazipa mashine za muingereza majina ya Kiswahili.

Unataka kipi kati ya viwili hivi?
ni vigumu sana kujenga uchumi na kutoa wataalamu wabunifu wa machine mpya wakati lugha unayo fundishia haileweki ipasavyo kwa wanafunzi. juzi tumepigiwa kelele na UN kwa kuleta mainjinia toka N.korea kututengenezea ndege za kijeshi. hao wameelimika vya kutosha kwa sababu ya wanatumia lugha wanayoielewa vizuri. pia nchi nyingi mara zilipoanza kutumia lugha zao hazikuwa na uchumi mkubwa. nyingi zilikuwa hohehahe kama sisi.
 
Una assime kwamba uvumbuzi ni lazima uje kwa kufundishwa.

I am not talking about aping others technologies here, or merely improving them, since we are challenging ourselves, how.about a paradigm shift?

What you are trying to.achieve is parrot existing technologies under the guise of innovation.

We can do better, without needing to invent words first.
 
Lugha ina mchango mkubwa ktk kuelimika na kujielimisha hasa inapotumiwa km njia ya kufundishia. Tatizo sio kingereza ama kiswahili tunaweza tukatumia hata kifaransa ama kisukuma. Tatizo ni lini tunaaanza kujifunza lugha hio.

Tunajifunza lugha na kuimudu vzr tukiwa chini ya miaka kumi. Hivyo km tutaamua kutumia kiingereza km njia kufundishia basi tuanze kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu na km itakuwa ni kiswahili basi tufanye hivyo2. Uganda, Kenya, India, Zambia nk wamefanya hvy na hawana matatizo km ya kwetu. Kumbukeni waafrika kusini enzi za utawala wa ubaguzi wa rangi walikataa kutumia lugha zao mama km njia za kufundishia.

Elimu ya Tanzania ina matatizo mengine mengi lkn lugha ni kubwa zaidi.

Haitoshi kuendelea kiuchumi na kiteknilojia km tu tutakuwa na njia muafaka ya kufundishia ila itatusaidia kama inavyowasaidia wenzetu. Kuna vitu vingine vya kufanya ili kuweza kujitegemea kiuchumi na kiteknolojia.

Njia na namna tunavyofanya sasa kutumia kiswahili na kingereza inatuathiri kwa kiasi kikubwa sana. Inafikia hatua kingereza hatukifahamu vzr na kiswahili hatukifahamu kwa ufasaha hata kwa ngazi ya mawaziri, wabunge na wengineo.

Kuna matatizo mengine ktk elimu ya Tanzania lkn la lugha ni kubwa zaidi.
umenena vema mkuu. watu wanasema kiswahili hakijitoshelezi, inamaana kikorea, kinorway, kirusi,kigiriki,kipoland,kisweeden, kidanish,kidutch, kijapan na kichina ni bora kuliko kiswahili?.juzi kati nilikuwa nacheki muvi ya mr.peabody and sherman (animation). kiswahili kimetajwa humo. hii ni lugha kubwa yenye wazungumzaji karibu millioni 100. wazungu walitufundisha kwa lugha zao ili watutumie cha ajabu tunaendeleza huo mfumo. tatizo la lugha ni kubwa kuliko tunavyofikiri.
 
Una assime kwamba uvumbuzi ni lazima uje kwa kufundishwa.

I am not talking about aping others technologies here, or merely improving them, since we are challenging ourselves, how.about a paradigm shift?

What you are trying to.achieve is parrot existing technologies under the guise of innovation.

We can do better, without needing to invent words first.
hatuwezi kusema tuanze from scratch kama wao. pia hatuwezi kwenda mbele na kuwa innovative bila kuipata elimu iliyopo ipasavyo. ilikuipata elimu iliyopo ambayo wenzetu wanayo inabidi tufundishwe kwa lugha tunayoielewa vizuri. hakuna nchi iliyo endelea kwa kutegemea tecknolojia yake yenyewe. wote wamedokoa huku na huko na kumodify. sisi lugha inatuzuia kudukoa huku na huko in effective way.
 
Hela yenyewe ya kutafsiria kwa hisani ya wamarekani?

Kukua kwa lugha ni zao la kukua uchumi, kama vyandarua tunahitaji wamarekani, sijui kama tunaweza hili.
ni kweli, ukuaji wa lugha hutegemea uchumi wa nchi kama ambavyo kichina kinakua kwa kasi. lakini wachina hawakusubiri uchumi wao ukue ndio waanze kufundisha kwa kichina.
 
Jamani, huna hata hela ya vitabu kwa kiswahili unasema China walianza tu? Labda walianza lini, na uchumi wao ukiwaje?

ni kweli, ukuaji wa lugha hutegemea uchumi wa nchi kama ambavyo kichina kinakua kwa kasi. lakini wachina hawakusubiri uchumi wao ukue ndio waanze kufundisha kwa kichina.
 
Kwa nini lugha ya matumizi mahakamani isiwe Kiswahili kuanzia mahakama za mwanzo hadi ya rufaa?

Tunashindwa hata kuandika sheria zetu wenyewe kwa kutumia lugha yetu wenyewe kama vile hizo sheria si za kwetu wenyewe!
 
umeona tulivyo vilaza! mi nilitafuta sheria ya ardhi ya kiswahili niliambulia bilabila. nilipata ya kiingereza,lakini sheria sio gazeti au kitabu cha hadithi. inahitaji uielewe kikamilifu.
 
umeona tulivyo vilaza! mi nilitafuta sheria ya ardhi ya kiswahili niliambulia bilabila. nilipata ya kiingereza,lakini sheria sio gazeti au kitabu cha hadithi. inahitaji uielewe kikamilifu.

Sawa, sheria siyo gazeti wala kitabu cha hadithi lakini pia si rocket science kiasi kwamba isieleweke kirahisi. Au unataka kunambia sheria ni ngumu kuliko rocket science?

Hivyo uwezekano wa kueleweka vizuri katika lugha ya Kiswahili ni mkubwa kushinda uwezekano wa kueleweka kwa Kiingereza.

Una uhakika kwamba kuendelea kwa hizo nchi kumetokana na wao kutumia lugha zao ?

Angalia sana hapa badala ya kutatua tatizo unaweza kutengeneza tatizo.., fahamu kwamba lugha ni njia ya mawasiliano tu.., badala ya kuanza kungangania watu watumie kiswahili kufundishia ungeimiza watu wajifunze na lugha nyingi kadri wawezavyo ili kuwaze kuwasiliana na wengi ipasavyo..

Kama point yako ni kwamba mother tongue inaeleweka zaidi kwanini wasukuma, wasifundishiwe kisukuma, wachagga kichagga na wahaya kihaya..., natumaini hapo hawa watu wataelewa zaidi na haya makabila yatakua kiuchumi zaidi.., husasan wagogo na watu wa kusini wajaribu hii njia
 
Ukitaka kujua uzuri au ubaya wa lugha yetu jiunge na ile Facebook ya kiswahili ya Tigo...uwiiiii!
 
Mimi nimetupa line yangu ya Tigo niliyokuwa natumia kwny tablet yangu maana niliona kinachoandikwa sielewi kabisaaa...kwa hapa jamaa wamechemka...lugha yetu bado misamiati mingi ni migumu haieleweki
 
Mbona hatujapishana. Kama hutegemei kutoka nje ya TZ au hutegemei kuwasiliana na wasiojua kiswahili, ni vema kuendelea na kishwahili. It depends on your aspirations. Vyuo vya Veta darasa la saba wanasoma kiswahili, hawahitaji kiingereza maana wao ni wa humu humu au nchi za kiswahili. Lakini kama unategemea kwenda Oxford, Cambridge, UN, AU and the like, fikiria mara mbili kusoma swahili as a medium of instructions at all levels of schooling.
 
Sawa, sheria siyo gazeti wala kitabu cha hadithi lakini pia si rocket science kiasi kwamba isieleweke kirahisi. Au unataka kunambia sheria ni ngumu kuliko rocket science?

Hivyo uwezekano wa kueleweka vizuri katika lugha ya Kiswahili ni mkubwa kushinda uwezekano wa kueleweka kwa Kiingereza.

ninachomaanisha ni kuwa watanzania tutaelewa vizuri sheria zingetafsiriwa kwa kiswahili. sidhani kama sheria za china, korea, ujerumani,jaapan na vietnam zinakosekana katika luha zao(unthinkable). uingereza wangekuwa na mawazo kama yetu leo wangekuwa wanaandika sheria zao kwa kilatin.
 
Back
Top Bottom