Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
- Thread starter
- #61
Una uhakika kwamba kuendelea kwa hizo nchi kumetokana na wao kutumia lugha zao ?
Angalia sana hapa badala ya kutatua tatizo unaweza kutengeneza tatizo.., fahamu kwamba lugha ni njia ya mawasiliano tu.., badala ya kuanza kungangania watu watumie kiswahili kufundishia ungeimiza watu wajifunze na lugha nyingi kadri wawezavyo ili kuwaze kuwasiliana na wengi ipasavyo..
Kama point yako ni kwamba mother tongue inaeleweka zaidi kwanini wasukuma, wasifundishiwe kisukuma, wachagga kichagga na wahaya kihaya..., natumaini hapo hawa watu wataelewa zaidi na haya makabila yatakua kiuchumi zaidi.., husasan wagogo na watu wa kusini wajaribu hii njia
kuendelea kwa nchi kuna sababu nyingi na lugha ni mojawapo, tena kubwa tu. hapo kwenye red inatakiwa tushangilie sana kwa kiswahili kuweza kueleweka na watanzania wengi.