Kwanini filamu za bongo hazina mvuto kama miaka ya nyuma wakati wa Kanumba?

OCCID Dominik

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2024
Posts
218
Reaction score
395
Wakuu hongera kwa wikiendi ya leo glories and praise to the LORD:

Wakuu kuna jambo linanitatiza kitambo kidogo na sijawahi kuona kama limewahiletwa mezani kujadiliwa,ama mara nyingi mitaani ndio utasikia swala hili na kila mmoja analizungumzia ila chanzo haswa hakijulikani.

Wakuu ni kwann movie za KIBONGO hazipendwi na hazina mvuto kama enzi za Kanumba? Maana ukifuatilia movie za KIBONGO kuanzia miaka ya tisini(j plus,shumileta,nsyuka) mpaka 2012 pale zilikua za moto sana,wakati teknolojia na uwekezaji wa kipindi kile nadhani ulikua mdogo ila story zilinoga kweli lakini miaka hii waigizaji ni wengi sanaa imekua, teknolojia imekua,wadhamini kibao ila bado tasnia na soko bovuuu.

Tangia afe Kanumba ni kama jamaa aliondoka na tasnia,hatujapata mkali wa kusumbua huko uafrikani then to the world.Walikuwepo wakina CLOUD,RICHIE,MTITU,MAYASA,RAY KIGOSI nk baada ya mwamba kufa hata nao hawaonekani maana ndio walikua maproducer,madirector Mahiri sasa sijui wameona nini kuendelea kusupport tasnia.

JAPO kuna mtakaosema pengine ni majukumu ya hawa watu kifamilia ila haiingii sababu ile ni kazi yao pia tena ikiwalipa kwa namna moja.
Leo tupo vizuri katika upande wa commedy kuliko serious stories film maana wakina MKOJANI wanafahamika mpaka congo,Nigeria japo Atleast huku kwenye serious story kuna GABO amekua kama mrithi wa Kanumba japo kuna viasilimia hatoshi.

Wakuu,sasa nini kinafanya filamu za bongo zidumae kadiri miaka inavyokwenda wakati actors ni wengi na teknolojia ni kubwa kama kuna ajuaye sababu haswa aweke hapa tuokoe sanaa.

more_than_pain.jpg
cloud_112.jpg
 
Nani ataangalia upuuzi wa mapenzi, hawana ubunifu ni guigana maudhui yaleyale tu. Kibaya zaidi eti filamu nzima inachezwa na watu wanne mwanzo hadi mwisho. Unakuta director, producer, editor ni mtu mmoja anahodhi kila kitu. Cha mwisho ni teknolojia ya kutengeneza sinema zao ni ya chini sana. Waende hollywood wakatengenewe sinema zao huko
 
Wenzetu wanaijeria ubunifu mzuri sana,muvi inakua kama ina uhalisia,hv kinashindikana nn kwetu,mfano ile edition yao tofauti na ss,sisi uhalisia hua hamna
 
Hata hao kina kanumba walikuwa wanaiga wanaijeria
 
Wanyonge wanyongeni ila haki yao wapewe , Sababu ni miingiliano ya tamthilia za nje ya nchi kama Uturuki ,ufilipino na kwingineko zimefanya Tamthilia za Bongo zichuje hata Movie za Kinaijeria siku hizi zimekosa.mvuto sababu ni kuzidiwa na nchi zingine
 
Wakuu hongera kwa wikiendi ya leo glories and praise to the LORD:

Wakuu kuna jambo linanitatiza kitambo kidogo na sijawahi kuona kama limewahiletwa mezani kujadiliwa,ama mara nyingi mitaani ndio utasikia swala hili na kila mmoja analizungumzia ila chanzo haswa hakijulikani.

Wakuu ni kwann movie za KIBONGO hazipendwi na hazina mvuto kama enzi za Kanumba? Maana ukifuatilia movie za KIBONGO kuanzia miaka ya tisini(j plus,shumileta,nsyuka) mpaka 2012 pale zilikua za moto sana,wakati teknolojia na uwekezaji wa kipindi kile nadhani ulikua mdogo ila story zilinoga kweli lakini miaka hii waigizaji ni wengi sanaa imekua, teknolojia imekua,wadhamini kibao ila bado tasnia na soko bovuuu.

Tangia afe Kanumba ni kama jamaa aliondoka na tasnia,hatujapata mkali wa kusumbua huko uafrikani then to the world.Walikuwepo wakina CLOUD,RICHIE,MTITU,MAYASA,RAY KIGOSI nk baada ya mwamba kufa hata nao hawaonekani maana ndio walikua maproducer,madirector Mahiri sasa sijui wameona nini kuendelea kusupport tasnia.

JAPO kuna mtakaosema pengine ni majukumu ya hawa watu kifamilia ila haiingii sababu ile ni kazi yao pia tena ikiwalipa kwa namna moja.
Leo tupo vizuri katika upande wa commedy kuliko serious stories film maana wakina MKOJANI wanafahamika mpaka congo,Nigeria japo Atleast huku kwenye serious story kuna GABO amekua kama mrithi wa Kanumba japo kuna viasilimia hatoshi.

Wakuu,sasa nini kinafanya filamu za bongo zidumae kadiri miaka inavyokwenda wakati actors ni wengi na teknolojia ni kubwa kama kuna ajuaye sababu haswa aweke hapa tuokoe sanaa.

View attachment 2993900View attachment 2993901
Hata za Kanumba zilikuwa sio nzuri.
 
Back
Top Bottom