Kwanini filamu zetu (Bongo) hazigusi hisia za watazamaji kikamilifu? Changamoto ya cultural immersion katika Bongo Movie

Kwanini filamu zetu (Bongo) hazigusi hisia za watazamaji kikamilifu? Changamoto ya cultural immersion katika Bongo Movie

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069

KWA NINI FILAMU ZETU HAZIGUSI HISIA ZA WATAZAMAJI KIKAMILIFU? BONGO MOVIE NA CHANGAMOTO YA CULTURAL IMMERSION​

Anaandika Robert Heriel Mtibeli.
Mwanasaikolojia Mtunzi.

Leo Mtibeli nitaleta mjadala kuhusu Tasnia ya filamu. Ambapo Tasnia hii ni moja ya Tasnia iliyoajiri vijana wetu wengi sana. Na kama mjuavyo, siku hizi kuna DSTV, Azam, Startime, na online media kama Netflix.

Vijana wapate ajira lakini lazima watoe kazi nzuri ambazo wao wenyewe watajivunia kazi zao. Kiasi kwamba heshima ya kazi ya sanaa ya uigizaji na tasnia ya filamu kwa ujumla wapate ile Heshima.

Mtibeli ni kama mwanasaikolojia bobevu, mwanafalsafa, mwanasosholojia na pia mtunzi leo tutajadili ni kwa nini Filamu za kibongo nyingi hazigusi kikamilifu hisia za watazamaji.

Mtu akizoea kuangalia filamu za hollywood, korea, Kisauzi afrika, kizungu n.k kisha ukamletea filamu za kibongo anaweza asimalize dakika 10 akitazama.

Ipo sababu. Sio kwa sababu ya bajeti ndogo, sio sababu ya vifaa duni. Nope! Hizo ni sababu ndogo saba.

Filamu ni tasnia inayotegemea saikolojia ya watazamaji. Saikolojia unazungumzia Hisia na akili za watazamaji.

Saikolojia ya watu huathiriwa na Utamaduni. Saikolojia ya Kibongo ni tofauti na saikolojia ya wakorea au wachina.

Hivyo Mtunzi, Muongozaji na mtayarishaji wa filamu pamoja na mchukua kamera lazima wajue hisia na akili za watazamaji.

Kwa kujua hilo;
Filamu ni zaidi ya kamera nzuri, waigizaji wazuri au picha zenye ubora wa juu. Filamu bora ni ile inayomzamisha mtazamaji ndani ya ulimwengu wa simulizi kiasi kwamba anasahau kuwa anaangalia maigizo. Hali hii kwenye saikolojia huitwa Cultural Immersion yaani uwezo wa filamu kumfanya mtazamaji ahisi kuwa yupo ndani ya utamaduni, mazingira na maisha ya wahusika. Maisha halisi.
Hata sisi watunzi wa riwaya na tamthilia. Moja ya mambo tunayocheza nayo ni pamoja na hii kumzamisha msomaji kupitia saikolojia yake au saikolojia ya mwanadamu(Cultural immersion).

Pamoja na maendeleo makubwa ya Bongo Movie katika miaka ya hivi karibuni, bado kuna changamoto kadhaa zinazofanya baadhi ya filamu kushindwa kugusa hisia za watazamaji kwa kiwango kinachotarajiwa. Changamoto hizo ni kama

1. Muziki Usioendana na Mazingira ya Simulizi​

Unapoangalia filamu kuna sauti za muziki, zinaweza kuwa ala za muziki au wimbo unaimba kwa sauti ya chini. Hizi huitwa backsound.

Moja ya changamoto kubwa kwenye filamu zetu ni matumizi ya backsound zinazofanana na filamu za Hollywood hata pale simulizi linahusu maisha ya Kitanzania.

Kwa mfano, tukio la kijijini cha Makanya, wilaya ya Same huko kwetu upareni linaweza kupewa muziki wa Magharibi au marekani ambao hauna uhusiano wa karibu na mazingira ya Kipare. Matokeo yake, macho yanaona Tanzania lakini masikio yanasikia Hollywood.
Kisaikolojia hiyo inapunguza hisia kwa Mtazamaji. Inakata.
Ilitakiwa backsound ipigwe kulingana na eneo la wahusika walioko kwenye filamu.

Mfano; Series ya Kombolela inayorushwa Azam wao wamefanya vizuri sana na inaakisi maisha halisi ya uswazi na kitanzania. Filamu ya Siri ya Mtungi halikadhalika.

Filamu kama ya Shaka Ilembe, ni filamu ya kisauzi, zulu. Inakuingiza kwenye uhalisia kwani muktadha umezingatiwa.

2. Lugha na Mazungumzo Yasiyo Halisi​

Wakati mwingine wahusika huzungumza kwa mtindo ambao si wa kawaida katika maisha halisi ya Watanzania. Lugha ya filamu inapaswa kuakisi jamii inayowakilishwa.

Unakuta mhusika anaongea sio kwa sauti halisi. Unamuona kabisa anaigiza. Filamu haihitaji waigizaji. Filamu inahitaji wasanii wanaoishi maisha halisi kwenye movie kiasi kwamba mtazamaji aone ni tukio la kweli kabisa.


3. Kuiga Badala ya Kujenga Utambulisho​

Sekta nyingi za filamu zilizofanikiwa duniani zilianza kwa kujenga utambulisho wao wenyewe. Miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000 tulishuhidia utamaduni wa kihindi kupitia Filamu za India, kisha Nigeria kisha baadaye Korea Kusini na Afrika Kusini kote huko zimefanikiwa kwa sababu zinajivunia tamaduni zao.

Badala ya kujaribu kuwa Hollywood ya Afrika Mashariki, Bongo Movie inaweza kuwa Bongo Movie yenye utambulisho wake wa kipekee.

Tanzania inavitu vingi vya kutambulisha, tuna jamii mia kidogo. Kuna wamasai, kuna wasukuma, kuna wamwera n.k.
Unaigiza unaongea kimarekani kwa kiswahili. Haiwezi kuleta msisimko.

Msanii Gabo Zigamba aliwahi kuigiza kwa lafudhi ya kimakonde, ile filamu ni moja ya filamu za wakati wote. Na itakumbukwa miaka mingi kwa sababu ina connect hisia za mtazamaji moja kwa moja na uhalisia.

4. Kutotumia vya Kutosha Sauti na Utamaduni wa Mahali​

Utamaduni haupo kwenye mavazi pekee. Upo kwenye muziki, methali, lafudhi, sherehe, mila na hata sauti za mazingira.

Mtazamaji wa Kitanzania ataguswa zaidi anaposikia vitu vinavyomkumbusha maisha anayoyaishi kila siku. Hapo ndipo filamu huonekana kuwa ya kweli zaidi.

Wengi wetu tunaijua ile Filamu ya Apocalypotle. Moja ya filamu bora ya wakati wote.
Ile filamu imetambulisha himaya ya Maya, backsound, mavazi, lugha, utawala n.k.

Angalia filamu za Uchina, nyingi hata kwenye mambo ya kula wanaweka vyakula vya kichina.

Lakini bongo ni nadra sana mtunzi kuonyesha na kutambulisha utamaduni wetu.

Fikiria sauti za ndege lazima ziwe za afrika, maji kutiririka, mivumo ya bahari na maziwa, milio na sauti ya wanyama wa kufugwa kama ng'ombe, mbuzi, na wanyama wa mwituni.
Hizo ni tamaduni ambazo filamu zetu wanazipuuza lakini zinanguvu sana kwenye kuteka hisia za watazamaji.

5. Hisia za Wahusika Kutokupata Msaada wa Mazingira​

Katika filamu bora, kila kitu hufanya kazi pamoja; mwigizaji, kamera, muziki na mazingira. Mhusika akilia lakini muziki, sauti na mazingira havisaidii kuonyesha uzito wa tukio, hisia za mtazamaji hupungua.

Hisia hazijengwi na mwigizaji peke yake, bali na ulimwengu mzima wa filamu unaomzunguka.

​

Nikimalizia kwa sababu hamtakagi niandike mambo mengi. Bongo Movie imepiga hatua kubwa katika ubora wa picha, majukwaa ya kuonyesha kazi na teknolojia. Hata hivyo, hatua inayofuata ni kujenga Cultural Immersion yenye utambulisho wa Kitanzania. Watazamaji wa Tanzania hawahitaji kuona nakala za Hollywood; wanahitaji kuona Tanzania yao, kusikia Tanzania yao, na kuhisi Tanzania yao. Filamu itakapofanikiwa kufanya hivyo, itaacha kuwa burudani tu na kuwa uzoefu wa kihisia unaokumbukwa kwa muda mrefu.

Mtu unaangalia filamu inaitwa kidawa alafu nyuma unasikia backsound ya Game of Thrones, heee! Yaani inakata sana.

Taikon nimemaliza.
Mtibeli katika moja na mbili
Kwa sasa Dar es salaam
 
Hawana ubunifu na uwekezaji ni mdogo

Yani mtu anawekeza 2m anataka avune 200m
 
Mimi kama mpenzi wa filamu umenigusa sana na hili andiko lako, zamani nilikuwa natazama bongo movie ila baada ya kuonja Korea aisee nashindwa kabisa ingawa siku hizi kwa upande wa tamthiliya wanajitahidi.
Suala la bajeti huwezi kulitoa kwenye changamoto ndio maana tunakuwa na maudhui yaleyale miaka nenda rudi, visa vingi ni vya mapenzi.. bodyguard katembea na mke wa boss, wale wanagombea bwana/mwanamke wakati ukienda kwa wenzetu wanagusa kila engo ni wewe tu kuchagua unataka nini
 
Mimi kama mpenzi wa filamu umenigusa sana na hili andiko lako, zamani nilikuwa natazama bongo movie ila baada ya kuonja Korea aisee nashindwa kabisa ingawa siku hizi kwa upande wa tamthiliya wanajitahidi.
Suala la bajeti huwezi kulitoa kwenye changamoto ndio maana tunakuwa na maudhui yaleyale miaka nenda rudi, visa vingi ni vya mapenzi.. bodyguard katembea na mke wa boss, wale wanagombea bwana/mwanamke wakati ukienda kwa wenzetu wanagusa kila engo ni wewe tu kuchagua unataka nini

Kwenye bajeti baadhi ya tamthilia nitakukatalia.

Angalia tamthilia za kituruki.
Hakuna bunduki, hakuna mabomu, hakuhitaji edit kubwa. Lakini bado zinafanya vizuri sana.

Mfano, tamthlia ya Golden Boy, Assery, hizi ni zakituruki.
Bajeti ya Huba na Juakali inatosha kabisa kutoa kitu chenye mvuto kama hizo
 
Ilikua movie nzuri sana, hivi utaratibu wa kushirikiana na kampuni kubwa kubwa kama Netflix , emc na nyingine kutoa movie kama SA wanavyofanya upoje

Ni kweli.
Niligundua tatizo sio waigizaji. Ishu ni Directors, watunzi, wachukua kamera na waongoza filamu.

Maana Siri ya mtungi walifanya vizuri
 
Back
Top Bottom