screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,857
- 15,866
GNAKO ni msanii mzuri sana kila mtu anajua hilo, na ni msanii ambaye amekaa kwenye game kwa mda mrefu, ameanza muziki akiwa kwenye group la N2N na baadae akajaribu kuwa solo kabla ya kuja kuungana na kina Joh Makini na Nikki2 kuunda kundi la WEUSI. Katika career yake ameshiriki katika hitsong nyingi sana za N2N, WEUSI na za kushirikishwa na wasanii wengine, na pindi akishirikishwa hakika huzitendea haki nyimbo hizo kiasi kwamba huonekana amezibeba. Pamoja na hayo yote cha ajabu huyu jamaa hajawahi kutoa wimbo wowote ambao it worth kuitwa 'hitsong'. Nikiangalia machorus killer wenzake waliowahi kutokea kwenye bongofleva kama Juma Nature, Dully Sykes, Qchillar, Belle9, Ben Paul, n.k walikuwa wakizitendea haki pia nyimbo zao, ila jamaa yangu GNako nyimbo zake hazieleweki. Hakika yeye ndio mnufaika mkubwa wa uwepo wa kundi la WEUSI, kwa maana ameprove kwamba hawezi kusimama yeye kama yeye. Hebu tumjadili kidogo anakwama wapi? Au ndo ananyota ya mshumaa kumulikia wenzake?[emoji54][emoji56]