Kwanini GPS trackers zinaondolewa baada ya vyombo vya moto kuibiwa?

Kwanini GPS trackers zinaondolewa baada ya vyombo vya moto kuibiwa?

hapa ndipo pa kujazia nyama, sababu GPS zishakuwa nyoso.!wabongo hovyo sana, wanasubiri ununue gari waibe.
Kill switch unatafuta wire ambao ukiukata gari haitawaka. Huo wire unaukata halafu unafunga switch ukitaka kuwasha gari itabidi uwashe kwanza hiyo switch otherwise gari haitawaka.

Kama unahisi hilo la kufunga switch ni gumu, zipo wireless kill switch, switch itajiwasha automatic remote ikiwa karibu na kujizima remote ikiwa mbali
 
Kill switch unatafuta wire ambao ukiukata gari haitawaka. Huo wire unaukata halafu unafunga switch ukitaka kuwasha gari itabidi uwashe kwanza hiyo switch otherwise gari haitawaka.

Kama unahisi hilo la kufunga switch ni gumu, zipo wireless kill switch, switch itajiwasha automatic remote ikiwa karibu na kujizima remote ikiwa mbali
Ubarikiwe sana....Nitakwenda na WIRELESS KILL SWITCH.
 
Kumekuwa na cases nyingi za watu kuibiwa vyombo vya moto na GPS trackers kuondolewa, mpaka kupelekea watu kuona kama kufunga GPS trackers hakuna umaana wowote.

Hii thread sitazungumzia kabisa detectors na jammers km watu wengi wanavyodhani kuwa wezi wanakuwa na tools hizo ambazo zinawasaidia kudetect mahali GPS tracker ilipokuwa installed.

Nitaeleza experience yangu kuhusu kile nilichokiona kwenye magari ya watu na ambacho kwa namna nyingine nimeona ni kama hakipo sawa.

Labda kwa kifupi tu niseme, nilichokiona ni kwamba ufungaji wa mifumo ya ulinzi mathalani GPS trackers na Alarms umekuwa ni wa kufanana, its like mwalimu/walimu wanaofundisha ufungaji wa mifumo hii wanafundisha kitu cha aina moja au wamewaaminisha wanafunzi wao kwamba GPS trackers lazima ifungwe kwa mtindo fulani.

Its sad kwamba gari nyingi GPS trackers/Alarms zimefungwa chini ya usukani, mathalani gari za kijapani ambazo siyo push to start. Mtu anafunga hiyo sehemu akiamini kwamba atatumia waya wa switch on kuzimia gari. Lakini kiuhalisia gari inazo waya nyingi sana ambazo ukizikata gari inazima. Hivyo kufunga maeneo tofauti tofauti inawezana.

Kwanza hili jambo la mtu kwenda kusomea kufunga GPS au Alarm halijakaa poa, huenda ndio matokeo ya huku kufanana. Its better kufunga GPS kwa mtu mwenye uelewa na umeme wa chombo husika. Kwa sababu huyu anakuwa na options.

Nowadays GPS trackers are tiny, kwa mfano kwenye magari sehemu za kuficha ni nyingi mpaka ndani ya modules huko na electronic devices zingine kama radio n.k.

Kutokana na hicho nilichokiona imenipelekea niamini kwamba ufungaji wa GPS trackers wa aina hiyo umepelekea hata wezi kukariri kwamba zinafungwa wapi hivyo kuwa rahisi kuzitoa wakiiba vyombo hivyo.

Sisemi kwamba hakuna njia nyingine inayotumika kuzitoa hapana zipo pia njia zingine lakini hii ya ufungaji wa kufanana tena mahali peupe kama chini ya usukani imepelekea utoaji uwe rahisi sana.

Pia kitu kingine, GPS haizuii gari kuibiwa. Ila Inaweza kukusaidia kulipata baada ya kuibiwa. Kama unataka lisiibiwe funga Kill switch iwe ya wireless au manual. At least mtu anaweza akashindwa kuliwasha na kuondoka nalo labda alivute.

Ni hayo tu kwa leo.
Hyo kill switch inafanyaje kazi mkuu
 
uwekaji wa GPS ni wakizembe ndio ni rahisi kujua imefungwa sehemu gani.

kama GPS itawekwa ndani ya chuma si rahisi kufahamu au itachukua mda kukata icho chuma.

Na swala jingine kuna vifaa hapa tanzania vinaingia hata watu kufahamu au serikali ila ndio vinatumika kutafuta gps hipo wapi.
Rahaa sana kuishi nje mpaka wizi wa kiteknolojia navo ufahamu.
ila JF wanafuta sana nyuzi zangu napo sema ukweli haya.itakuwa moderator ni mwizi
IMG_0400.jpg
 
zinasaidia vpi ? ilihali mpaka kulipata hilo gari unakuta ni chesis imepaki ?

wezi wako smart , hizo GPS hakuna kitu, wanaruka ukuta wanang'oa kila kitu wanakuachia mifupa pamoja na GPS yake

unaamka asubuhi unatoa macho
Ukiwa na mali kama hiyo, basi weka angalau ulinzi wa mbwa. Hata wakusaidie kukuamsha!
 
Back
Top Bottom