"Pia kitu kingine, GPS haizuii gari kuibiwa. Ilq Inaweza kukusaidia kulipata baada ya kuibiwa. Kama unataka lisiibiwe funga Kill switch iwe ya wireless au manual. At least mtu anaweza akashindwa kuliwasha na kuondoka nalo labda alivute."
GPS iliyokamilika lazima ije na relay yake ya kuzima na kuwasha, pasipo kujua wengi wanafungiwa GPS without relay.
All in all thanks for sharing this article.
GPS is also my area of expertise.
Is also area of my proffesional
Watu wengi wanataka huduma ya location tu hawataki immobilizer.
Nimefunga sana hizi ndude kabla wachina hawajaja enzi hizo tunatumia galool triton H, na triton K2 za Israel na omnicom
Nowdays yamekuja matakatala kibao hata sijui mnafanyaje kazi yani
Anyway, anachosema jamaa ni ukweli mtupu watu hawataki kuumiza kichwa ni kumaliza kazi na kchukua pesa.
Enzi zangu wakati nafunga GPS tracker tena nikikuta mtu anahitaji location tuu bila immobilizer yaaani naifunga mahali hutakaa uione hata unye
nikimaliza nampa mteja print out ya mchoro wa mahali ipokiwa installed kwa ajili ya reference huko mbeleni hata kama sipo.
Things went good na magari yaliyo ibiwa tuliyakamata kama kuku bandani kwa kushirikiana na jeshi la polisi.
Ilikuwa inafika kipindi GPS tracker tunaifungua kwenye housing yake inakua circuit tuu, tunaforge Resistance ya antenna ngoma inafichwa hakuna wa kuiona labda uwe na instrumentation.
Now day mtu anafunga GPS ukifuatilia antenna unaikuta, Shenzi kabisa.
Enzi hizo tulikuwa tunafanya kama mtoa mada Jitu alivyosema, Kwenye gari kuna sensor kibao, unaiunga immobilizer unafuatilia waya unaoenda kwenye gas pedal/ Accelerator (ya umeme)
Gari inawaka poa lakini haipigi race hivyo huwezi endesha.
Anyway sisi wengine tumeamua tuangalie maisha upande mwingine.