Kwanini haiitwi Vatican Country badala yake inaiwa Vatican City?

Kwanini haiitwi Vatican Country badala yake inaiwa Vatican City?

Ngoja nikujibu mimi si muhaya bwana......Ili sehemu iweze kuwa nchi kwa maana ya dola (state) lazima ikidhi vigezo vilivyotanabaishwa na mkataba wa Montevideo wa mwaka 1933.Vigezo ambavyo Vatican imevikizi

1.Idadi ya kudumu ya watu(permanent population) Vatican ina watu 800+

2.Mipaka inayoeleweka ,Vatican ina Hekari 129.

3.Kutambulika na mataifa mengine kama taifa, Vatican inatambulika na ina mahusiano na mataifa mengine ndo maana ina balozi nchi mbali mbali (Nuncios) na pia japo haina kiti umoja wa mataifa(Sio member) ila UN iliamua kuipa uwezo wa kushiriki shughuli za umoja wa mataifa bili kuwa mwanachama ikitambuilika kama (Holy see).

Baada ya kusema hayo sasa nikurudishe kwenye desa kamili, kwa nini inaitwa City na sio nchi well, tunarudi nyuma kwenye mapatano ya Laterano 1929 (Lateran Treaty) ambapo bwana yule mwenye mawaa na Mfashisiti Benito Musollini aliamua kuigawa baadhi ya sehemu ya Italia(mji) kwa papa ajitawale kwa raha zake, Kwenye sheria ya kimataifa mji ukishakua na uwezo wa kujitawala wenyewe basi utaitwa City State, ni kama alivyosema jamaa yangu bwana Waterloo nami bila tashiwiti nikaamua kumzodoa sababu aliandika kama juha, ni kweli kimantiki alikua sawa ili kiuwasilishaji alipuyanga Jina hilo likaendelea kutumika hata baada ya Umoja wa mataifa kuitambua Vatican kama nchi jina la Vatican City limeendelea kutumika.

*Ikumbukwe City state ni ndogo kwa state kwa muktadha wa eneo, Mussolini aligawa hekari 109 kwa papa na ikawa CITY state ila sasa Vatican ina Hekari 129 *
Safi mkuu nimeelewa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Umepuyanga na magoogle yako, We si mtu mzima kabisa! Sasa magoogle ya nn kama first year pathetic
Mbona wewe huleti majibu yako? Halafu punguza dharau mdogowangu wengine baba zako humu JF
 
Ukumbuke Rumi zaman ilitawala kama Mamulaka NASIO DINI.

baadae wakaingiza Dini ndani ya Mamulaka yao ivo RUMI IKAWA INATAWALA KISIASA NA KIDINI.

Mwaka 1798 , Papa alivyochukuliwa mateka nakuuwa, RUMI ilipoteza mamulaka yake ya Kisiasa na Kidini ila Dini ikaendelea kukua nakukuaa

Baada ya vita ya kwanza ya Dunia kuisha, MUSOLIN kwa sababu ya msaada alopewa na Dini ya kirumi. Aliingia mkataba nao ambao Aliwapa WARUMI. MAMULAKA YAO YA KIDINI NA KISIASA.

Toka huo mwaka ,Rumi ikajitawala Kisiasa( mamulaka) na Kidini .

Ila kwakua Nchi inabaki kua ITALIA , basi Rumi ya Vatican wanabaki kua sehem ya nchi hiyo lkn yenye kujitawala , mamulaka waloipata kupitia Dini .
Mamlaka na sio Mamulaka
 
Umepuyanga na magoogle yako, We si mtu mzima kabisa! Sasa magoogle ya nn kama first year pathetic
Kirasmi Vatican inajulikana kwa jina la "The State of the Vatican City"
 
Halafu ni dokta!!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Yaan nae amends shule jiulize wale wengine???

Sasa mbona na wewe yale yale tu “amends shule” au kwakuwa wewe yako ina swagger ya kizungu [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mkuu wangu sikuhizi kuna vitafasiri lugha ..

Ila siunajua Rumi Ilitawala ?? Kipindi kile Yesu anazaliwa Rumi ndio ilikua ikitawala Dunia .

Ikaendelea kutawala ivoivo kwa staili ya Udini na Siasa mpaka 1798 ndio ukawa mwisho wao .

( kwenye maandiko, hapo ndipo biblia ilisema "ana Jeraha la mauti".....

Baada ya Musolin kuwarudishia hadhi yao ya kidini na kiserikali,...... ( kwenye biblia imeandikwa "Jeraha la umauti LIKAPONA)....
Gud
 
Ukumbuke Rumi zaman ilitawala kama Mamulaka NASIO DINI.

baadae wakaingiza Dini ndani ya Mamulaka yao ivo RUMI IKAWA INATAWALA KISIASA NA KIDINI.

Mwaka 1798 , Papa alivyochukuliwa mateka nakuuwa, RUMI ilipoteza mamulaka yake ya Kisiasa na Kidini ila Dini ikaendelea kukua nakukuaa

Baada ya vita ya kwanza ya Dunia kuisha, MUSOLIN kwa sababu ya msaada alopewa na Dini ya kirumi. Aliingia mkataba nao ambao Aliwapa WARUMI. MAMULAKA YAO YA KIDINI NA KISIASA.

Toka huo mwaka ,Rumi ikajitawala Kisiasa( mamulaka) na Kidini .

Ila kwakua Nchi inabaki kua ITALIA , basi Rumi ya Vatican wanabaki kua sehem ya nchi hiyo lkn yenye kujitawala , mamulaka waloipata kupitia Dini .
Nachanganyikiwa naposikia Rumi, Roma, Vatican, na pia nilisikia Yesu alipoondoka duniani aliliacha kanisa la Roman Catholic, je nini uhusiano wa Rumi na Roman na je Yesu alikwenda Rome? Ilikuwaje yeye myahudi akaenda kuwakabidhi dhehebu watu wa Roma?
 
Usichanganye mambo;Rumi ni kwa kiswahili na Roma ni kiingereza
 
Mahakama inazo na majaji kabisa wanao na sheria wanazo na magereza wanayo ila ni ya kuwafunga mapadri,masisita na maaskofu tu wakikosea waweza fungwa ndani ya majumba yao hatoki humo hadi miaka ya jela iishe aweza fungwa nchini au nje ya nchi kwenye monastery zao
Kweli kwa waliofatilia kisa Cha Archbishop Miringo na kitabu chake Cha "Fish drawn out of the mud wataelewa hili Jambo. Ila hiki kitabu kiliondolewa kwenye Catholic bookshops Mara baada ya Miringo kurudia yaleyale yaliyompeleka kwenye retreat centre kule Brazil kwa miaka mitatu.
 
Kiuhalisia kabisa hiyo si nchi kabisa kama inavyotajwa. Ni kama nchi ya kufikirika ata uki gugo map sasa ivi ukaweka ramani yote ya dunia. Unaweza kuona kila sehemu kila nchi na mipaka yake ila uwezi kuiona Vatican kama nchi sana sana utaambulia kuiona Vatican city katikati mwa nchi ya Italy tena ikionekana kama mji tu.

Nchi ya Vatican au Vatican city
ni dola-mji lenye eneo la kilomita za mraba 0,44 tu. Raia wake ni 565 na wageni ni 232 jumla ina wakazi 791 na Hivyo ni nchi ndogo kuliko zote duniani. Ni nchi ya Papa ambaye ni askofu wa Roma na mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kote.

NB: kumbuka ni nchi ndogo kuliko yoyote duniani yaani ata huu mji wetu wa dar es salaam ni mkubwa kuipita Vatikani.
Kwa mantiki hiyo nafikiri ndiyo mana ikawa Vatican city na si Vatican country
 
Strategic city/country. Kuna mengi sana yamejificha..
He who claims must prove...haisaidii kupiga ramli...eleza hiyo strategic city/country ikoje na hayo mengi yaliyojificha yakoje.
 
Hiyo Ni Nchi Ya Kimkakati Wa Mambo Mengi Sana Kwenye Hii Dunia, Wanaoishi Humo Ni Idadi Maalum
Ina kuwa na watu wengi mchana tu. Jioni ikiingia wengi wanajisogeza Roma. Nimesema 'wanajisogeza' maana Vatican City iko within Roma. Na mchana watu wengi wolioko Vatican City ni watalii. Wenyeji hasa wa Vatican City hawazidi 800 kama sikosei.
 
Back
Top Bottom