Kwanini hakuna Kenyan high ranking official aliyemtembelea Tundu Lissu?

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Hapa Bongo tunaambiwa kwamba Dunia nzima inamjua na kumjadili Tundu Lisu, kwa kuwa kuna Wakenya hapa JF ningependa kufahamu kwa nini hakuna mkubwa yoyote si wa Serikali wala Chama cha Siasa wa nchi ya Kenya aliyefika kumjulia hali mgonjwa namba 1 Duniani, Tundu Lisu kwa miezi 4 aliyokuwa amelazwa Hospitalini hapo Nairobi?

Msiniambie hawamjui Tundu Lisu ni nani? Hilo sitaamini, sasa hivi tunaambiwa Mkuu wa EU, Spika wa Bunge la EU wanafahamu uwepo wa Tundu Lisu mjini Brussels na amepewa na EU ulinzi mkali na kwamba punde watafika kumjulia hali, lkn nirudi Afrika, Kenya kwa nini hawakufika Hospitalini?
 


Ndo tunavyoambiwa hivyo, kwamba EU president anafahamu uwepo wa mgonjwa namba 1 Duniani, Tundu Lisu na kwamba atafika kumjulia hali, lkn huko ni mbali ningependa kujua kwa nini Kenya hakuna mkubwa wa Kenya aliyefika kumuona?
 
Hakuna Serikali inayotaka matatizo na nchi zingine kwa sababu ya mtu mmoja aliyeondoka kwao (iwe kwa sababu yoyote ile) na kutumia jukwaa la nchi nyingine kuikosoa nchi yake. Watu wa jinsi hiyo hupata shida kupata hifadhi ya kisiasa. Wakikupa wanakwambia: "Na ukae kimya tusisikie chochote". Na ujue Kenya na Tanzania sio maadui. Sisi ni marafiki. Mtu mmoja hawezi kuvuruga uhusiano wetu wa miaka mingi
 
..mzee kibaki, kalonzo musyoka, chief justice mutunga[rtd], ni baadhi ambao nimesikia walikwenda kumjulia hali.
 
Charity begins at home
 
Ni vizuri kumuombea apone haraka lakini si vizuri kuongea ongea habari za mgonjwa na kuzidisha chuki kwa wabaya wetu kwani mpaka sasa hawajakamatwa na mgonjwa wetu hapewi matibabu ya kubadili nyama kuwa chuma kwasasa nikubadili uelekeo kutoka siasa za mihemuko na harakati kuja kwenye siasa shirikishi sisi sote ni mashahidi tukio hili lilistahili kuwa fundisho kwa wauaji ili wasirudie tena lkn ni kinyume chake bado tunaendelea kuweka mpendwa wetu kwenye hatari na kuwafundisha wabaya wetu kutumia mbinu nyingine tusiyoifahamu ili kutekeleza azma yao ambayo haikukamilika.
 
Labda walienda kimyakimya. Kuna wengi tu hapa Tz kutoka ccm pia walienda kimyakimya kwa kuhofia kumgusa vibaya mfalme.

Kina Ole Sendeka wapo wengi tu ndani ya CCM.
 
Ni wale wale tu. Kwanini waende kumuona wakati wao pia wanawafanya hivyo watu wao.
 
..mzee kibaki, kalonzo musyoka, chief justice mutunga[rtd], ni baadhi ambao nimesikia walikwenda kumjulia hali.


Siamini hilo, CJ wa Kenya aende kumtembelea Tundu Lisu halafu tusirushiwe selfie? Hii ni kama ile tulioambiwa First Lady wa Kenya amemchangia Tundu Lisu matibabu lkn hkn mahali popote palioandikwa!
 
Huyo labda angetembelewa na type ya kina masakuu, mama kayai, ojwang na kina MWALLA.

R.i.p to the deceased.
 
Jamani, hakuna majitu mavivu ya kufikiri tena yenye akili za wastani kama machadema!
 
..mzee kibaki, kalonzo musyoka, chief justice mutunga[rtd], ni baadhi ambao nimesikia walikwenda kumjulia hali.
Kalonzo Musyoka ni mwanachama wa muungano wa NASA na majibu raisi mgombea wa Odinga. Ambacho ni chama kilichokua hakiungwi mkono na Chadema. Sidhani habari zako zina ukweli
 
Niliona picha moja ya uhuru alipomtembelea lisu nipe muda mfupi jitakupatia
 
Kalonzo Musyoka ni mwanachama wa muungano wa NASA na majibu raisi mgombea wa Odinga. Ambacho ni chama kilichokua hakiungwi mkono na Chadema. Sidhani habari zako zina ukweli
Labda alienda kumuomba mawaidha ya jinsi atakavokwepa risasi ikifika siku yake. Hahaha.
 
Suala la ulinzi walilotoa serikali ya Kenya kwenye hospitali ya Nairobi ni muhimu kuliko yote ambayo mtu mwingine angependa viongozi wa Kenya wafanye.

By the way, Chama chake Lissu na familia hakijawahi kusikika popote wakisema wanashindwa kupata matibabu kwa sababu ya fedha. Walifanikiwa kujichanga na kulipia matibabu ambayo ni ya msingi pia baada ya ulinzi kuimarishwa pale.
 
JANA MLIKUJA NA UZI KUWA HAKUNA PICHA ZA LISSU AKIWA MATIBABU MAJUU. BAADA YA KUANZA KUMIMINIKA KWA FUJO SASA MMEHAMIA KUTAKA KUJUA VIONGOZI WA KENYA WALIOMTEMBELEA LISSU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…