Kwanini Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imevunjwa?

Kwanini Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imevunjwa?

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2016
Posts
250
Reaction score
409
KWANINI HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM IMEVUNJWA Ni Mawazo Yangu #Joseph #Yona

Kiutawala Jiji lilikuwa limegawanyika katika Halmashauri sita za Serikali za mitaa ambazo ni:-

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni.

Sasa Ukiangalia hapo juu kulikuwa kuna chombo tu kinaitwa HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM, Lakini chombo hicho hakikuwa na eneo rasmi la kiutawala kwa maana nyingine Halmashuri ya jiji haina ARDHI inayoitawala, kwa maana hiyo inategemea vyanzo vya mapato kutoka halmashauri za manispaa.
Manispaa zijichange Ili Jiji lisonge.

Chombo hiki yaani HALMASHAURI YA JIJI ilikuwa ina Meya wake na baraza lake huku halina vyanzo vya mapato, LAKINI WALITENGA BAJETI, SASA SWALI UNAPEWAJE BAJETI HUKU MIRADI INAWEZA KUHUDUMIWA NA MANISPAA ZENYEWE? Hivyo kulikuwa na matumizi mabaya ya pesa kwa kuwa ni kama unampa MTU pesa hana matumizi.

SASA kilichofanyika nikuvua KOFIA ya HALMASHAURI YA JIJI na kuipa ILALA.
Na manispaa za KIGAMBONI, KINONDONI, UBUNGO, TEMEKE Zitabaki kama manispaa.

IMG_20210225_071433_418.jpg
 
Si mnajitia Hamnazo!.

NOTE: Vaa barakoa na unawe mikono kwa sabuni na maji tiririka pia ukae mbali na mikusanyiko.
 
Watu walipokuwa wanaongelea demokrasia watu hawakuelewa wengine , demokrasia ikibakwa kwa wapinzani baadaye huhamia ndani ya chama tawala .

Uamuzi wa kufanya anavyotaka kwenye serikali za mitaa ndio uliokuwa unafanya alazimishe madiwani wote wawe wa kwake. Ni wazi kungekuwa kuna madiwani wa vyama vingi barazani hangethubutu kufanya hivyo kwakuwa malalamiko yangekuwa mengi, kama tu wakati ule kuweka meya wake alikuwa anashindwa ,kwa kuhofia vurugu.

Leo sasa ccm wameona huyu mtu alivyokuwa na dharau. Unavunja halmashauri hata bila kushauriana na meya wahusika. Dharau sana ,anajua hawana la kumfanya na hawana pa kwenda kulalamika au kungekua na wapinzani barazani wangeungana nao ,hawapo.

Na huu ni mwanzo tu wa uvunjaji wa demokrasia ndani ya chama chake mwenyewe.Hata mkapa alipovunja halmashauri hakukurupuka alifanya utafiti na aliwashirikisha un-habitat.

Watu wanasema hata mameya hawaheshimiki tena anawaona kama madiwani tu .. Mnaona hata alivyomtukana meya wa morogoro hadharani.

Unajua mtu akikupa kitu bure lazima akusimange. Kama pia wabunge wanavyosimangwa bila magufuli hawangefika bungeni hivyo wafunge midomo.
 
Kwahiyo hayo mmeyaona jana?tangu miaka ya 1960 hadi leo hii ndiyo mnayaona?
Ccm must go
 
Kwa hyo kutakuwa na jiji la Ilala? Bado sijaelewa huu ukurupukaji... Au walipokuwa wanaita jiji la Dar es salaam walimaanisha ni hao madiwani na mkrugenzi wao and nothing else
Kwa sasa tunataka kuwaaminisha watu kuwa Dodoma lilikuwa chaguo sahihi
 
Ngoja nitafute uelewa wa hilo jambo kwanza na namna lilivyokuwa linafanya kazi, nitapata chakusema
 
Mgawanyo unafanyika kupigiana mapande ! Vingine ni viinimacho tu
 
Hii sio kitu kipya,ni sawa na jiji la mwanza,kuna manispaa ya ilemela na nyamagana na manispaa ya nyamagana ndio city council
 
Ukiwa mtanzania na Unataka kuishi maisha marefu basi jitahidi kadiri inavyowezekana usiyajue yanayoendelea au yanayofanyika ndani ya nchi hii inaitwa Tanzania
 
Huyu jamaa anakuja kubadilisha katiba na kuitawala TANZANIA milele
Kabisa ....kumbuka Serikali za Mitaa zina hadhi yake na ni kama kamuhimili kadogo.....huwa wanaachwa wajiamulie maendeleo , sasa kawapora vyanzo vya mapato , sasa anawapora hata heshima mbele ya jamii,alianzia Morogoro kamtukana Meya hadharani ..yote hii kwakuwa anajua aliwasaidia kuiba kura ....sasa mbona yeye anataka aheshimiwe wakati na yeye kura anajua aliiba zake na za wabunge na madiwani .....aidha awaheshimu wenzake au akae kimya ....maana kama kuiba wameiba wote ....lakini haina maana kuwa wote walitegemea kura za wizi ..hata kama wangefanya kihalali ccm haingekosa wabunge na madiwani asilimia 50% hivyo sio wote wameingia kwa fadhila zake ...sema sasa kwakua uchaguzi ulivurugwa inaonekana ni wote ....
 
Back
Top Bottom