Kuanzia leo tar 25 February 2021ukizungumzia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam unazungumzia Wilaya ya Ilala pekee,Ila ukizungumzia mkoa wa Dar es Salaam unazungumzia muunganiko wa Wilaya za Temeke, Ubungo, Kigamboni, Kinondoni na Ilala.
Kabla ya leo Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam liliongoza Halmashauri 6 huku ikiwa haina kata wala mtaa na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam aliongoza Halmashauri zote 6;-
1.Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
2. Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
3. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
4. Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
5. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
6. Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni
Kuanzia leo tar 25 February 2021, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam itajiongoza yenyewe kama Ilala,na Mayor wa Ilala anakuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam mwenye mamlaka kwa Halmashauri ya Ilala na atakuwa na mamlaka kwa Halmashauri ya Jiji la Ilala tu ambayo inabeba "title" na hadhi ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,kabla ya leo Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na ma-Mayor 6,watano kutoka kila Manispaa na wasita kutoka Halmashauri hewa ya Jiji la Dar es Salaam.
-Halmashauri hewa ya Jiji la Dar es Salaam.
Sasa Ukiangalia hapo juu kulikuwa kuna chombo tu kinaitwa Halmashauri ya Jiji la Dar es,lakini chombo hicho hakikuwa na eneo rasmi la kiutawala kwa maana nyingine halmashauri ya jiji haina kata wala mtaa inayoitawala,kwa maana hiyo inategemea vyanzo vya mapato kutoka halmashauri za manispaa ya Ilala, Kinondoni,Temeke,Kigamboni na Ubungo, Halmashauri hiyo ilikuwa kama kupe,kwa hiyo ilikuwa ni kama halmashauri hewa.
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilikuwa ina Meya wake na baraza lake huku halina vyanzo vya mapato wala haina kata wala mtaa inayotawala,lakini cha ajabu walikuwa na bajeti yao ya kuhudumia miradi hewa ambayo miradi watayoitaja utaikuta kwenye Halmashauri ya Ilala, Kinondoni, Kigamboni,Temeke na Ubungo,
Hivyo kulikuwa na matumizi mabaya ya pesa kwa kuwa ni kama unampa mtu pesa wakati hana matumizi nayo,Sasa alichofanya Rais Magufuli ni kuivunja Halmashauri hiyo kupe na kuichukua Halmashauri ya Ilala na kuiita Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,na Manispaa za Kigamboni, Kinondoni,Ubungo,Temeke zitabaki kama Manispaa.
Nimalizie kwa kusema japo vigogo wawili jana wamekosa kazi Mayor wa Jiji la Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam,awa kijiografia na kuitawala walikuwa na mamlaka ya Halmashauri 6 za Mkoa wa Dar es Salaam wakijihusisha na kushughulikia Serikali za Mitaa,huku Mkoa wa Dar es Salaam ukijihusisha na kushughulikia masuala ya Serikali Kuu,niwaombe wakubaliane nasi kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar ilikuwa kama urembo tu kwani haikuwepo kiuhalisia,haina tofauti na wafanyakazi hewa kwani wafanyakazi na wanasiasa walikuwa wanafaidi mihela,Kwa hiyo ile ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya zamani itavunjwa na itakuwa chini ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala,hii itapunguza hela zilizokuwa zinatumika hovyo.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Jiji la Ilala.
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.