Kwanini hatuna maeneo ya kupumzikia katika mitaa yetu?

Shida sio kuanzisha sehemu za namna hiyo,shida ya nchi yetu ni poor management

maeneo ya hivyo yakianzishwa usimamizi utakua mbovu,wafanyakazi hawatolipwa na hela

ikipatikana itakua inaenda mifukoni mwa watu end of the day eneo linauzwa kwa mwenye pesa zake

nina plan ya kutengeneza kitu ya namna hii nnje ya mji huko,nishapata heka 50 zangu kazi ya kupanda miti

inaendelea huko,kamradi kangu ka uzeeeni maana hizi nguvu najua kuna muda zitakata,1 ya miradi yangu ya uzeeni,n huo.
 
Miji ya slums hii ambayo kila mtu anafanya analojiskia ndio iwe na park?

Hayo mambo huwa yanaendana na elimu, ustaarabu na maisha mazuri, haiwezekani kwenye Nchi zilizojaa maskini hivi na watu wanaoamini kwenye witchcraft.
 
unaleta uzungu uswazi.😂😂😂
mnaweza plan hvyo kesho mnakuta mtu anapandisha nyumba anasema kauziwq kesi mahakamani.😀
 
Bora wewe umewaza mbali.Hakuna kitu kizuri kuishi maisha katika sehemu ya kupendeza.
 
Naungana nawe katika hili..kila sehemu ya wazi kama sio bar, basi ni garage au kituo cha mafuta nk
labda tukianza kwa kujitolea vikundi mbalimbali kila weekend tunaweza kubadilisha hizi sehemu zikawa za kistaarabu.
 
Watu wetu wa urban planning sio wanao enda na wakat na naona wengi ni conservative sanaa,

Mfano iyo dodoma inayo tajwa sasa as jiji jipya ingependeza ktk master plan yao jiji ilo lijumuishe vitu vya burudan mfano sport tourism, michezo kama racing e.g magari mfano wale wa formula 1, horse racing,

Ninacho kiona ni kizazi cha baadae kitataka ku experience michezo tofauti tofauti sio.kila siku watoto wetu wakute vichaka vya kucheza kombolela tu

To.me, nafikiri itakuwa poa sanaa tuki fikiria kutenga maeneo kama hayo then tuka ruhusu investors waka inveat ktk izo michezo kama ya rcing hakika itleta impact kubwa sanaa baadae ktk.uchumi wa taifa
 
Mawazo mazuri sana haya,ila kama hujaish nnje ya Tanzania huwezi kuyaona umuhimu wake,kwa hakika inasikitisha namna ujenzi wetu ulivo,wenye akili walituachia,walipo ondoka viongozi wasiojitambuwa wamejenga kila sehemu hata viwanja vya kuchezea watoto... Angalia Shaulimoyo walivoicha wenye akili na hali ilivo leo?
 
Bora wasiweke na wakiweka kuwe na viingilio kuanzia teni kwenda juu, jobles wasije wakageuza makao yao ya kuzugia watz wengi ni wavivu wavivu ndio mana likitokea tukio utawakuta wamejazana kumbe lengo wapate pakupotezea muda shenziiiii kbs
Kuwaita watized wavivu ni kuwakosea sio kweli hatakidogo kazi hamna. Wapi kuna kazi na malipo japo iwe alfu 20 tu kwa siku uone watakavomiminika. Au unataka walime mahindi Dar?
 
Kuwaita watized wavivu ni kuwakosea sio kweli hatakidogo kazi hamna. Wapi kuna kazi na malipo japo iwe alfu 20 tu kwa siku uone watakavomiminika. Au unataka walime mahindi Dar?
Ila Mkuu kuna aina sita za uvivu mi naongelea ile ya sita[emoji12][emoji12][emoji12]
 
Ishu mbona ndogo. Nunia nyumba ya mtu kisha uibomoe alafu apo upafanya Park, wewe na familia yako pamoja na watu wengine mpumzikie.

Bingo[emoji39][emoji39]
Brainless skull... cha ajabu wamekupa likes kwa huu ugoro wako
 
Zanzibar wanajitahidi sana katika hili. Japo kuna kiingilio kidogo ila hukosi sehemu za kuchill na familia na kula upepo zinazomilikiwa na serikali
Huku bara sehemu za ku chill ni Bar, yaani imefikia wazazi wanaenda bar na watoto...
 
Kweli mkuu kama mtaani kwetu kuna maeneo mazuri sana tengefu kwa kupumzika lakini yoote yamegeuzwa garage!
Huwa naamini ni rushwa tu ndio inayo sababisha iwe hivyo kwasababu kama maeneo yako kwa kila mzunguko wa nyumba 10 katikati ni eneo la mapumziko au kucheza watoto lakini ndo hivyo gereji hata ukisema nani atakusikiliza???
 
Mkuu niliwahi kushughulikia maeneo ninapoishi Diwani akaniijia juu " nitakuhamisha mtaa" nika muuliza na nyumba utanibebea? Nikapiga mkwara mzito kuwa KUANZIA SASA SITAKI KUONA CHUMA LA MTU MBELE YA NYUMBA YANGU MITA 6 NA NJIA YA KUTOKEA BARABARANI IWEPO ! Katii gereji ipo ila ni umbali wa mita 6 toka kwangu na barabara ipo wazi ikilenga nyumba yangu.
Wengine wamejaziwa machuma hata pakutokea ni shida!
 
Ukisikia Siasa za Mvurugano ndo hizo. Kisebusebu na kiroho papo. Maeneo wazi wanayataka lakini maslahi binafsi yanawekwa mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…