Faka25
JF-Expert Member
- Sep 14, 2021
- 1,738
- 1,134
Naomba niongee kidogo kuhusu suala la vyuo na Technology tunayo itaka, kiukweli tanzania ya sasa tumesha haribiwa kiakili, sio kwamba elimu tunayopewa haifai la hasha ila wanaopewa elimu ndio matatizo, dronedrake nadhani utakuwa shahidi kwa upande wa career ambayo upo ni wanafunzi wangapi wanamaliza hawajui hata resistor na nini na wanatoa pesa kufanyiwa projects za mwaka wa mwisho. Kingine nimeshiriki sana baadhi ya mashindani ya Makisatu, Feed the Future na mengine na ni watu kibao wanapewa mapesa kibao lakini after hapo wanapotea na hawasikiki tena, kikubwa kwa upande wangu ninachokiona ni vijana hatutaki kujishughurisha na wazee hawataki tujishughulishe na wanafunzi hawataki kujifunza wao wanachotaka ni cheti tu. Kuna watu ukiwaambia wanasingizia vifaa ila kiukweli uzembe wa kujifunza na kufatilia ndio unafanya tuone upatikanaji wa vifaa ni mgumu. Ila vifaa upatikanaji ni rahisi na wa gharama nafuu kama una nia na unachotaka kukifanya. Hayo ni maoni yangu tu
Serikali haijaweka mazingira mazuri, wanawaza uchaguzi.